Wasanii wa Bongo nani kawaroga?

Wasanii wa Bongo nani kawaroga?

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,700
Reaction score
3,921
Wote wamekalilishwa neno "kimataifa" utacheka sana namna wanavyokazania huu ujinga... Madee katoa nyimbo mpya kamshirikisha Tekno wa Nigeria alooo nyimbo ni mbaya dunia nzima, shishi kamshirikisha mdada wa Nigeria asee nyimbo ukiidownload unaifuta saa hio hio baada ya kumaliza kuiskiliza, yote tisa joh makini ndio kachekesha sanaa, katoa nyimbo na davido ni mbaya ukiiskiliza mpaka unaweza kuumwa kichwa, nyimbo nzima unaskia tu kataa kataa leetaa hawa nani kawaroga?

Mbaya zaidi wanatumia mamilioni kuwalipa wasanii hao wanaowaita wa kimataifa na utengenezaji wa videos ambazo hakuna anaejisumbua ata kuziomba kwenye TV stations.

Tulitegemea labda wasanii wetu hawa watakua wajanja na wabunifu kidogo labda, ila wao wameimba kama wanaija tu hali inayopelekea kupoteza muda na fedha.

Kujua ni kujua tu, hakuna aja ya kupoteza muda kwa watu ambao ata nao hawajatoboa kimataifa kama uyo sijui IYO nk., sasa hawa wanao jiupgrade na kujiita wa kimataifa ila wanategemea show moja ya fiesta maishani wanajiskiaje wakiona mtoto mdogo kama Aslay tu ambae video Zake uenda ni za elf 50 tu ila uswahilin kote nchini zinapigwa kama nyimbo za taifa na youtube ngoma zake zinatoboa views million Mpaka 2+, lazima watajidharau tu ila na kwa vile wasanii hawa ni mbumbumbu Hawawezi kureason hapo.

Sasa unakuta msanii chege alishafanya nyimbo mpaka na run town ila sasa nna uhakika hata malawi hawajui kama kuna mbumbumbu anaitwa chege, huyu simlaumu kwakua amekua akilazimisha fani, ila sana wale wenzake daaah hasa joh maskini huyu yeye tulijua anatoboa maana davido huyu huyu kabisa? Davido kaishika africa kwa sasa unapata bahati adhimu alaf unaimbaa kataa kataa leta wewe umerogwa au? Hio hela ya mavideo ya gharama ya nyimbo mbaya kama hio si bora uyo msanii angeenda kununulia ng'ombe tu zikaja kumsaidia maishani.

Anyway, wasanii wetu bado hawajajua kua wanapoteza muda na fedha kutafuta vitu wasivyovijua, big up diamond wasaidie ndugu zako.

Mjumbe wa kihenga hauwawi.
 
utaonekana una wivu ila huo ndo ukweli wasanii wengi was bongo wanahisi ngoma kubamba lazima ufanye mavideo ya gharama....Roma kapigia porini tena location moja lakini ngoma imebamba kinoma.Wasipofungua akili wataendelea kusubiri huruma ya Ruge fiesta.

Delta Force

Mkuu nimependa hapa......

Davido kaishika africa kwa sasa unapata bahati adhimu alaf unaimbaa kataa kataa leta wewe umerogwa au? Hio hela ya mavideo ya gharama ya nyimbo mbaya kama hio si bora uyo msanii angeenda kununulia ng'ombe tu zikaja kumsaidia maishani.
 
Kwanza ni Wimbo siyo nyimbo pia naona hauujui muziki kama ulivyoandika.

Aslay nyimbo zote anaimba kwa melody ile ile na mixing ni ile ile ndani ya miezi miwili ametoa nyimbo zaidi ya 14 huyu siyo msanii wa kawaida, hao wanaomsikiliza hawajui muziki kama wewe tu.

Ninavyojua Shilole kaimba na Iyo remix ya Kiki, ule wimbo siyo sawa na za kipindi kile anashindana na Snura ambaye kwa sasa ni utumbo mtupu. Hatua ya sasa ya Shilole yule mpinzani wake haiingii.
Wimbo wake mpya najua unaitwa Kigoli sijui huo unaousema wewe ni upi.

Joh Makini na Davido na Madee na Tekno wamezingua, kwa kua Joh anaendekeza mistari ya kitoto sawasawa na mdogo wake Niki wa 2. Kati ya Madee na Joh ni bora wimbo wa Joh utausikiliza na usingizi utakuja.

Madee na Tekno nakubaliana na wewe ni utumbo kuanzia Tekno mpaka Madee mwenyewe, Cabo Snoop katoa ngoma inaitwa Awaa huyu ni jamaa alikuja kufanya show Tanzania na mkalimani lakini kwenye huu wimbo kaimba Kiingereza, ameamua kubadilika na kufuata soko. Wasanii wetu bado wamelala.

Washauri wa wasanii wana mapengo kwenye ubongo.
 
- Unafanya kolabo na msanii mkubwa

- Unashoot video ya gharama

Mwishoe unategemea HURUMA ya show za FIESTA hapa hapa Kwa MAKONDA.

Mtu kama JOH MAKINI, Kagharamika sana, ila SHOW hata KENYA hapo ambapo ni MDEBWEDO Hajawahi KUPATA!

USHAURI WANGU.
- Wasimuige Dimond, hata yeye hakupata UKUBWA alionao kwa Kutumia PESA, KUFANYA KOLABO Kubwa na KUSHOOT Video kwa Madirector wakubwa.
 
Umeandika ukweli mtupu....mbona inawezekana wakafanya collabo za hapa hapa ndani na nyimbo zikabamba tu??

Tatizo wanatafuta shortcut za mafanikio wakati uwezo wao mdogo, Aslay anafanya poa sana nakubaliana na wewe!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nimependa hapa......

Davido kaishika africa kwa sasa unapata bahati adhimu alaf unaimbaa kataa kataa leta wewe umerogwa au? Hio hela ya mavideo ya gharama ya nyimbo mbaya kama hio si bora uyo msanii angeenda kununulia ng'ombe tu zikaja kumsaidia maishani.

Kabisa mkuu uyo msanii bora angenunua ng'ombe tu.
 
Kwanza ni Wimbo siyo nyimbo pia naona hauujui muziki kama ulivyoandika.

Aslay nyimbo zote anaimba kwa melody ile ile na mixing ni ile ile ndani ya miezi miwili ametoa nyimbo zaidi ya 14 huyu siyo msanii wa kawaida, hao wanaomsikiliza hawajui muziki kama wewe tu.

Ninavyojua Shilole kaimba na Iyo remix ya Kiki, ule wimbo siyo sawa na za kipindi kile anashindana na Snura ambaye kwa sasa ni utumbo mtupu. Hatua ya sasa ya Shilole yule mpinzani wake haiingii.
Wimbo wake mpya najua unaitwa Kigoli sijui huo unaousema wewe ni upi.

Joh Makini na Davido na Madee na Tekno wamezingua, kwa kua Joh anaendekeza mistari ya kitoto sawasawa na mdogo wake Niki wa 2. Kati ya Madee na Joh ni bora wimbo wa Joh utausikiliza na usingizi utakuja.

Madee na Tekno nakubaliana na wewe ni utumbo kuanzia Tekno mpaka Madee mwenyewe, Cabo Snoop katoa ngoma inaitwa Awaa huyu ni jamaa alikuja kufanya show Tanzania na mkalimani lakini kwenye huu wimbo kaimba Kiingereza, ameamua kubadilika na kufuata soko. Wasanii wetu bado wamelala.

Washauri wa wasanii wana mapengo kwenye ubongo.

Yaani umetumia nguvu kubwa kiasi iki kutetea ujinga mkuu? Hapa sina lengo la kuwapoint wasanii hao tu, hapana wako wengi tu, hao nimetolea mfano na swala sio kulinganisha et aslay sijui kafanya nin? Hell no, nimejaribu kubainisha namna wanavyozifanyia mzaha ndoto zao za kimataifa ktk hali ya ukichaa.
 
- Unafanya kolabo na msanii mkubwa

- Unashoot video ya gharama

Mwishoe unategemea HURUMA ya show za FIESTA hapa hapa Kwa MAKONDA.

Mtu kama JOH MAKINI, Kagharamika sana, ila SHOW hata KENYA hapo ambapo ni MDEBWEDO Hajawahi KUPATA!

USHAURI WANGU.
- Wasimuige Dimond, hata yeye hakupata UKUBWA alionao kwa Kutumia PESA, KUFANYA KOLABO Kubwa na KUSHOOT Video kwa Madirector wakubwa.

Yeah sure mkuu
 
Back
Top Bottom