Wasanii wa bongo wapeni haki zao ma-producers kabla hawajafa

joseph1989

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2014
Posts
17,420
Reaction score
35,765
Wasanii wakibongo wengi wamekuwa mstari wa mbele sana kulilia haki zao kuwa wanaibiwa (kweli wanaibiwa sana),lakini hivi nyinyi wenyewe hamuoni mnavyowaibia na kuwadhulumu maproducer.Ukienda mbele mtu kama Swizz ,Dr dree mpaka kesho bado wanakula hela ya nyimbo walizo zalisha lkn kwa bongo tofauti maproducer wengi wa zamani wameacha kuzalisha nyimbo.Sio kwamba hawajui au labda wavivu bali music kwao hauwalipi,sababu wanawatajilisha wasanii wao wanakufa masikini.

Wasanii wengi wabongo fleva wakimwona producer anachipukia wanamkimbilia huyo ili kumlalia ,eti wanaamini kupitia wao wanamtangaza huyo producer,baadaye producer akitaka apate maslahi mapya kwa ajili ya kuboresha maisha yake na studio yake wasanii wengi humkimbia mf tumeiona hii kwa Nareel baada ya kutaka kila ngoma atakayo izalisha basi,lazima awe na mgao wake endapo nyimbo ikitumika kuingiza pesa matakeo yake WEUSI wamekimbia,sasa hivi wapo kwa S2KIZZY.AY na Mwana FA wanaidai Tigo zaidi ya bil 2 ,lkn katika bilioni hizi mbili wamemsahau Harmy B ambaye ndiye aliitengeneza Habari ndio hiyo na wao walimkimbia Harmy B baada yakuweka mikataba ili alinde maslai yake ,Mabeste pamoja na Ve money nao wakamkimbia Harmy B.Hivyo hivyo kwa Macko Chali,Master Jay,P-Funk,Manecky ,Lamar nk hawa wote wametengeneza hit nyingi sana lakini mwisho wa siku wasanii wameishia kuwadhulumu.

Haya Pancho kafa nimemuona ndugu yangu Shetta anasema watz ni wanafiki kisa hawamjali mtu akiwa hai (kweli ndio tabia zetu sisi watanzania),lkn Shetta leo hii nikikuuliza hivi Pancho alingiza Tsh ngapi wakati wewe ukiingiza hela kupitia nyimbo ya mdananda ,ninauhakika jibu huna zaidi utasema nilimlipa studio session,kumbe hujijui wewe mwenyewe ni bonge la manafiki.Nikimuuliza Chid Benz moja ya ngoma zake kubwa kuliko zote zisizochuja na ilimpa show nyingi,je Pancho aliingiza Tsh ngapi ninauhakika jibu litakuwa lile la Shetta ,nikimuuliza Mabeste nae jibu lake litakuwa lile lile .Matokeo yake mnawafanya maproducer wengi waachane na mziki kwani nyinyi wasanii hamuwaheshimu wao ,vipaji vyao pamoja na ubunifu wao wakutengeneza biti ambao unawafanya nini mng'ae.

Sheddy Clever amaproduce hiti tatu za Diamond ambazo zilishika karibia Africa nzima Number 1,Nitampata wapi,Marry me (imegonga 6xplatnum=zaidi ya kopi 180000 ),lkn leo nikimuuliza Chibu je Sheddy alipata Tsh ngapi,jibu litakuwa lile lile kama la Shetta.Abby daddy nae ameproduce ngoma nyingi za Kiba na moja ya beef lao (inasemekana),baada ya Abby kuweka viwango vipya vya studio na mikataba ya nyimbo anazozalisha, ndugu yangu Kiba akaondoa kwa Abby,lkn nikimuuliza Kiba je Abby alipata Tsh kupitia nyimbo ya Aje,Cheketua nae jibu lake lile lile,eti bila yy abby asingekuwa maarufu (upuuzi).

Wasanini mjifunze kuheshimu vipaji na ubunifu wa maproducer wanaowatengenezea beat,kwani bila wao hamna hiti songs,hamna show,wala hela kupitia hizo digital platforms na mjifunze kwathamini pindi wawapo hai kwa kuwapatia haki yao wanayostahili.

Ndio maana leo hii wameibuka maproducer wa hovyo kabisa, wanatengeneza biti zinazofanana ,hamna ubunifu yaani nyimbo siku hizi unasikiliza kwa mazoea wala hushtuki,tofauti kipindi kile cha Majani,Master Jay,Lamar,Manecky ,Mack nk badilikeni mnapodai maslahi yenu mkumbuke kuna maproducer na nyie maproducer jaribuni kujenga umoja wenu ili muweze kutetea maslahi yenu bila hivyo mtaendelea kulalamika na kufa masikini. .
 
Wewe pia ni mnafiki, mafanikio ya Msanii na Purodyuza hayana uhusiano.

Kila mtu na kazi yake na msanii anaweza kufanya kazi na Purodyuza yeyote yule.
 
Una pointi lakini unazijua mikatamba wanazoingia na wasanii.

Ma-producer wengi wa bongo wanafanya biashara ya kuuza beat...anatengeneza unaipenda anakuuzia.

Au unaenda unaimba anakusikiliza anatengeneza. Baada ya kuingiza vocal na mastering msanii utajijua wewe.

Nadhani wabadili kwanza namna wanavyofanya biashara zao. Maana ukiniuzia beat mwisho wa siku inakuwa yangu japo mtengenezaji wewe.
 
Wewe pia ni mnafiki, mafanikio ya Msanii na Purodyuza hayana uhusiano.

Kila mtu na kazi yake na msanii anaweza kufanya kazi na Purodyuza yeyote yule.
Msanii na Producer ni sawa na Mpini na jembe wanategemeana, ndio ukweli mwenyewe ukatae ukubali,huwezi kutenganisha wasanii na maproducer .Ndio maana wenzetu ulaya kwa kulijua, nyimbo ikitumika kuingiza hela tu basi mule kuna mchnganua wa mapato,kwa kila aliye husika katika uzalishaji wa ile nyimbo.
 
Hakuna ulazima wa producer kubebwa na msanii. Kila mtu anafanya kazi yake hata kama wanategemeana.
 
Asante,kweli wengi wao wanafanya kwa mazoea na hawajui thamani ya kazi yao.
 
Ni kweli kabisa hakuna uwiano 'producer' unapata laki 5,msanii anatengeneza mamilioni kupitia mdundo wako unaoishi miaka na miaka; tatizo ma-'producer' hawana umoja.Anzisheni umoja...na muboreshe mikataba/makubaliano na wasanii lasivyo njaa itazidi kuwatembelea.
 
Kama Producers wanataka kufanikiwa kupata kipato stahiki kwa kazi zao......watengeneze Record lebal, waingie Mikataba ya muda mrefu na Wasanii wachanga ambao wanaona wana uwezo....!

Otherwise itakua ni sawa na habari ya ............Usiulalie nje mlango Wazi.
 
Hapo ndipo napokumbuka kisanga cha p. Funky dhidi ya chameleone, na ile beat ya nikusaidiaje, inasemekana p.funky alimlamba vibao kamelioni. Baada ya kuitumia kwenye wimbo wake. Sijui waliishianaje? Mikataba ni muhimu ili hata maproducer wanufaike na vipaji vyao.
 
P funk ana haki ya kumpiga vibao, kwani hata mara kwanza alipoitumia hii biti hakuongea na P wala kumlipa chochote, mara ya pili akala hela iliyolipwa na waandaji wa movie ya Queen of Katwe, walitumia biti kama sound track akaipiga nayo.
 
Tatizo ni umoja.. wasanii wanakimbilia kwetu sisi maproducer wadogo..na sisi hatuwezi kukataa...japo tunadhulumiwa.. halafu huu mtindo wa kuuza beat umeshapitwa na wakati...
 
r.i.p joshua magawa, hatimae umerudi msingisi nyumbani kwa pastor magawa kupumzika.
 
Yeap mkuu, umenena.
 
Hawauzagi beat ..wasanii wanalipia studio session then inatakiwa kupitiq hiyo nyimbo producer awe ananufaika kupitia. Shows,ring tones .n.k .ndo maana ikitokea labda kampuni flan inataka kufanya tangazo kwenye nyimbo ya msanii flan lazima na producer ahusishwe kwenye mapato ...tatzo LA producers hawana umoja na pia hawana misimamo juu ya haki zao so wanaendeshwa endeshwa tuu ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…