Wasanii wa hiphop hawana tofauti na wasanii wa taarabu?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Hii kitu niliiiona siku nyingi ila leo nimeona Afande sele akimchamba Gsolo nikaikumbuka.

Taarabu huwa ni nyimbo zilizojaa majisifu na kupakana maneno na Hiphop imejaa sana hizi ishu. Ukianza kwenye bifu la Tupac na BIG walikuwa wanapakana sana maneno. Tofauti ni kuwa kwenye hiphop maneno huwa makali sana. Pia wakati kwenye taarabu watu hujitamba kuchukuliana waume kwenye hiphop wao hujitamba kuchukuliana wake.

Pia wasanii wa taarabu hufuatiliana sana maisha hadi mtu anaimba siri za mwenzake unashangaa amejuaje?. Hivyohivyo kwenye hiphop, kwenye nyimbo za kudis watu hutoleana siri za ndani kabisa.
Hiphop haina tofauti na taarabu.
 
Kaa pemben na Uzi wako wa kishamba huko"
 
Hivi ile ya Afande Sele ni hip hop? Mi nilikuwa sijui.
 
Mgambo Sele alikuwa zamani kidogo, kizazi cha leo hakuna anayemjua wala kumkumbuka, kabakia na kula ndum tu.
 
Ungetupa mifano halisi kibongo bongo na huko ng'ambo ingeeleweka zaidi otherwise inabaki kuwa brah brah!
 
Taarab za kiume... Msikilize J. Makini, Ney wa mitego Fid Q and so on... Wao ni wao zaidi kuliko wengine, wao ni bora, wao ni super brands etc
 
mkuu hip hop wanavo dai ni kuusiana na naisha halisi yalio kwenye jamii ukweli ulio wazi sasa sijuii kuusu izi taarabu zina ukweli au ni majigambo na ukuzajibwa bifu-binafsi sio shabiki kindakindaki wa mziki wa aina yoyote
 
Ungetupa mifano halisi kibongo bongo na huko ng'ambo ingeeleweka zaidi otherwise inabaki kuwa brah brah!
Mshana kaweka mifano hapo. Kwa kuongezea kulikuwa ma bifu la Langa na Jmo wakitupiana maneno. Wakina Joe Makini , Nikki wa pili na wakina Ney wamejaa kuimba vijembe na Kujisifu.
 
 
Kunadog anaitwa [HASHTAG]#Eduboy[/HASHTAG] anasema "bongo bahat mbaya wakat unalala studio" yaan anajua ad mtu anapolala kwel hphpop n taarabu
 
Hip Hop muasisi ni Yesu Kristo sema hawa wa siku hizi wanafanya kijamii zaidi ndio maana wanahip-hop wengi ni wepesi kumsifia mwanamke au mama kuliko baba au kiongozi, hupenda kujisifu au kujinadi kwa maneno ya kubuni ila yesu hakujinadi bali alijitambulisha kwa ukweli tu
 
au sioo kwahiyo masihi alikua kwenye Nguzo ipi? maana wanasema HIP HOP inanguzo zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…