Angalizo. Wajikite kwa kazi ktk mirindimo ya sauti waimbaji/sauti za ala Kikagera au ki-Tanzania ila watumie lugha ya Kiswahili maana wakija kilugha itakula kwao. Wajifunze Kiswahili ni lugha kubwa kitaifa na kimataifa.
Wasanii wengi wazuri wa "mikoani" mfano toka kanda za Ziwa, Nyanda za Juu Kusini wameshindwa hata kukubalika kitaifa kwa vile wanakuja kwa gia ya "kilugha" badala Kiswahili ingawa wangeweza kutumia "mirindimo/beats" za Kikabila lakini ktk lugha ya Taifa .
Hii ku-sample beats za kikabila lakini ktk Kiswahili pia itasaidia Tanzania kuwa na wasanii wanaotoa kazi zisizofanana na kutofanya masikio yetu kuchoka kusikiliza vitu vinavyofanana wimbo baada ya wimbo.