Wasanii wa kibongo na fasheni

vikosi makuruti

Senior Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
192
Reaction score
68
kwa kweli bado najiuliza,kwamba ni ulimbukeni au ukosefu wa elimu? Zimepita fasheni nyingi, lakini hii ya wanaume kuvaa sketi jamani twende nayo taratibu. Nasema hivi kwa sababu juzi tulimshuhudia Diamond Platnam, msanii ambaye tunasema ni kioo cha jamii akipanda jukwaani akiwa amevaa sketi.

Sawa lengo kuleta utofauti lakini sio kwa staili hii, kumbuka kuwa vijana wa kibongo especially this dot com generation hawaishi kuiga kila kitu wanachofanya mastaa. Sasa kama wataiga huu uvaaji wa sketi hamuoni kama ni hatari kwa taifa ambalo tunapinga mapenzi ya jinsia moja?
 

Mimi sikuona hiyo sket ila niliona suruali na juu yake ni kitambaa kimezunguka kiuno. Kama ukisema hiyo hivyo.. Hata suti sio asili ya mtanzania.
 
Kwa taarifa yako,ulimbukeni wa mzungu ni fasheni kwa mweusi!ni tatizo la wengi sema kwa wasanii ulimbuken uko waziwazi
 
ulimbukeni uelewa wa mambo kutokuamini culture ya Kitanzania na kukumbatia u western ndo tatizo sio lazma kila kitu uige ili kutafta attention zisizo na maana
 

Kadri anavyozidi kufanya vizuri na maadui wanaongezeka!.. wewe ni adui yake mwingine...
 
sipo akilini mwake,ila nadhani hata kujadiliwa huku kwake anaona amefanikiwa,kuna wakati hawa tunaowaita mastaa huwa wanafanya kitu ili watengeneze stori
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…