Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Kauli ya Kiongozi wa Kikundi (Isaac Ibrahimu Timbanda)
Akizungumza kwa niaba ya kikundi hicho, Isaac Ibrahimu Timbanda alieleza kuwa walifuata taratibu zote za kisheria kabla ya kujenga mabanda hayo:
Ukaguzi wa Mara kwa Mara: Wakati wanaendelea na ujenzi, maofisa wa TANROADS na Halmashauri ya Jiji walikuwa wakifika mara kwa mara kukagua na kujiridhisha na vibali vyao kabla ya kuondoka.
Kushitukizwa na Uharibifu: Pamoja na kufuata taratibu zote hizo, walishangazwa na hatua ya mabanda yao kuandikwa alama za "Ondoa" na baadaye kubomolewa usiku/asubuhi na mapema na kuwaachia hasara kubwa ya fedha na vifaa walivyokopa.
"Tumefuata taratibu zote, tumelipia ada za serikali TANROADS na Jijini. Lakini ghafla tunakuta mabanda yetu yamebomolewa na kutuachia hasara kubwa sana. Tumeingia gharama kubwa na wengine tumekopa fedha hizi." — Isaac Ibrahimu Timbanda.