RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Mhadhara - 40:
Wakati ule tulikuwa tuna idadi kubwa ya wasanii waliopeleka ujumbe mzuri kwa jamii na serikali. Hakika walikuwa ni kioo cha jamii kweli kweli. Hawakupata hela lakini walituachia kitu maishani. Hebu tuwakumbuke baadhi;
1. AFANDE SELE - aliimba NAPENDA NDUGU ZANGU: Alituhamasisha sote tupendane. Kila mmoja ampende mwenzake kama Biblia isemavyo kuwa; mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuacha hapo aliimba DUNIA INA MAMBO na MALARIA.
2. WAGOSI WA KAYA - waliimba WAUGUZI: Walipeleka ujumbe mzuri kwa madaktari na wauguzi wafanye kazi kwa weledi na uadilifu. Hakika wasanii wa wakati ule wapewe maua yao.
3. WA2KU2 - waliimba WALIMU (Tuna hali ngumu): Walipeleka ujumbe kwa serikali na wadau wengine wa elimu wawakumbuke walimu wa shule na vyuo. Hakika wasanii wa wakati ule walikuwa ni kioo cha jamii kweli kweli.
4. PROF JAY - aliimba NDIYO MZEE & KIKAO CHA DHARURA: Aliwataka wananchi wasikurupuke kuchagua viongozi, wanapaswa kuchagua viongozi bora ambao watajali shida za wananchi. Sio viongozi ambao huonekana mwaka wa uchaguzi tu. Pia alitoa ujumbe kwa wanasiasa wakumbuke wapiga kura wao.
5. KALI POPOTE - aliimba IMEKAA VIBAYA & TUMBO JOTO: Aliwataka askari polisi wasijisahau sana pindi wanapotimiza majukumu yao. Lakini pia aliitaka jamii iheshimu Jeshi lao. Hakika hawa wasanii walikuwa ni kioo cha jamii.
6. KEISHA - aliimba USINICHEKE: Aliitaka jamii kuacha ubaguzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, na hata kwa watu wengine wenye uhitaji maalum. Hakika wasanii wa wakati ule wapewe maua yao.
7. FEROUZ - aliimba STAREHE: Aliwakumbusha vijana na watanzania wote ambao wana tabia ya umalaya waache tabia hiyo mara moja kwasababu UKIMWI unatesa taifa. Hakika wasanii wa kipindi kile walikuwa ni wasanii kweli kweli.
8. MANDOJO & DOMOKAYA - waliimba KAZI YAKE MOLA: Kufiwa ni jambo la huzuni sana, hata hivyo tumezaliwa ili tuishi, lakini pia tukumbuke kuna kufa (kifo). Hivyo wasanii hawa wametutia moyo pindi tunapowapoteza ndugu, jamaa na marafiki zetu. Hakika wapewe maua yao. R.I.P MANDOJO.
👁️ Wakati ule tulikuwa na idadi kubwa sana ya wasanii waliopenda kufikisha ujumbe mzuri wa maendeleo kwa jamii na serikali kupitia nyimbo zao.
ENDELEA KUTAJA WASANII WALIOIMBA NYIMBO ZA AINA HIYO ILI KUWAPA HESHIMA YAO.
Right Marker
Dar es salaam