Wasanii wa Kitanzania na siasa

Wasanii wa Kitanzania na siasa

Ma-chemist

Member
Joined
May 11, 2020
Posts
36
Reaction score
15
Kama kichwa ha habari kinavojieleza hapo juu, msaada tafadhali.

Tunaeleka mwaka wa uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge pamoja na madiwani. Ipo haja sasa kwa Watanzania kukaa na kupima licha ya kwamba Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka wazi kabisa katika Ibara zake kuwa kigezo cha mtu kugombea nafasi yeyote ya kuwa kiongozi katika nchi, kubwa kabisa ni ile inayosema lazima ajue kusoma na kuandika. Lakini sasa, wakati umefika kwa Watanzania wenzangu kuangalia na kulinganisha kuwa tuko katika Karne ya ngapi, na sheria hii ilitungwa Karne ya ngapi.

Hatuwezi kuwapa ridhaa watu ambao wanataka kutumia kigezo cha umaarufu walio nao kutaka kuungwa mkono katika hatakati zao za kisiasa na kupata ridhaa ya kuwa akilisha wananchi ndani ya Bunge. Hoja kubwa apa kuna baadhi ya Wasanii kama vile Shilole, Harmonize, Steve Nyerere kutaka kutangaza nia ya kugombea nafasi za ubunge katika majimbo yao.

Watu hawa ambao wanataka kutumia kigezo cha umaarufu wakati hata elimu zao hazijavuka kidato cha nne, wengi wao ni Darasa la Saba, na sina hakika kama walipata cheti, narudia kusema sina hakika kama walipata cheti cha kuhitimu elimu ya msingi maana kigezo cha kupata vyeti vya baraza vipo, lazime uwe umehitmu kikamilifu na kupata alama stahiki.

Watanzania, angalau mtu anaetaka kutangaza nia ya kugombea katika nafasi hizi awe na Elimu isiyopungua angalau kidato cha sita na kuendea kama shahada, shahada za uzamili na shahada za uzamivu katika nyanja yeyote. Hatutaki kuona Bunge la wabunge wa kutuonesha vituko na kiki ndani ya Bunge. Tunataka maendeleo chanya (+) katika karne hii ya 21.

Watanzania wenzangu, kwa hiyo awa wasanii waliochukua hatua ya kutangaza nia ya kugombea nafasi yeyote lazima wajitathmini mara tatu; wasitumie upendeleo wao wa kuwa wasanii maana kipindi hiki cha 2020 haitawezekana. Na ushauri wangu kwao wasije wakaendelea kuhamasisha watu kuwaunga mkono🎓📝
 
Watawapiga swaga watu wa vijijini walipokulia huko wawape kura.Sio majimbo yalioendelea.
 
Tatizo siyo wao. Tatizo ni kuwa na jamii ambayo haiandai watu kuja kuwa viongozi ama wenye sifa za uongozi hawataki uongozi.

Kungekuwa na watu makini wenye ushawishi mkubwa kisiasa katika maeneo yao, leo hii wasingekuwa mada. Badala yake wangeonekana wasanii wanaotaka kufanya sanaa kupitia siasa.

Hata hivyo wasomi(baadhi) wameonesha usomi si kitu linapokuja suala la uongozi thabiti.

Ni HAKI yao, wacha wananchi wenyewe waamue
 
Uko sahihi ila tatizo mwandiko tu kaka
 
Rais ana Ph.D lakini kila siku anajiharishia.

Tupime elimu kwa uwezo wa mtu, tusipime elimu kwa makaratasi.

Hao uliowataja wasanii hawana elimu ya makaratasi wala uwezo. Hawana track record.

Ila, hili halimaanishi haiwezekani akawepo mtu mwenye uwezo bila ya kuwa na elimu ya makaratasi.

Na pia, hilo halimaanishi mtu mwenye elimu ya makaratasi ndiye mwenye uwezo.
 
Umati unaokusanyika kwenye kampeni za wagombea sio wa watu wajinga, wanatumia body language kuelezea Jambo na hisia zao. Iko siku wasanii watakuja kueleweka vibaya kwa kuunga mkono upande mmoja wa sakata.

Historia za akina Mbega, Isike, Mkwawa, Rumanyika, Kinjekitile, Karl Peters, Shamte, Okelo, Richard Turnbull, Kambona, Rupia, Chipaka, Zuberi Mtevu, ZPPP, nk na tabia zao ziko vitabuni hadi leo. Hata historia za wasanii na tabia zao kwa wanasiasa lazima zitakujakusomwa na wajukuu zao.

Mbaya zaidi Mali za wasanii wa aina hii iko siku zitakuwa mashakani kama vurugu za kisiasa zikitokea Kama Sanaa yao haitakuwa neutral. Mimi nawaonea huruma kwakuwa hawajui walitendalo. Ni kweli wanatafuta riziki lakini wanajiingiza kwenye hatari ya muda mrefu na faida ya muda mfupi.
 
Back
Top Bottom