mayowela
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 2,125
- 1,753
Muziki wa singeli umeshika sana wakati huu hasa mikoa ya Pwani, na mikoani kila mtu alitaka kujua ni muziki wa aina gani, si kwamba haukuwepo zamani ila jitihada za Efm zilichangia ushike hatamu japo redio ilikuwa haijafika mikoa mingi na walienda mbali mpaka kuanzisha kipindi maalumu kw aajili ya singeli chini ya Kicheko Mtata.
Kila muwamba ngoma huvutia kwake, mziki ukapokelewa kwa nguvu zote wasanii wa singeli wakaanza ona matunda kwa kualikwa kwenye show za Efm, na wengine kufanya dili za matangazo, nakumbuka Man Fongo alishafanya tangazo la Kampeni ya Nitigo pesa kutoka Tigo, Kicheko akasajiliwa Clouds na kuna baadhi ya wasanii wakagawanyika beef zikaanza wengine wakaona upande wa pili ndio wa maana sana
Nakumbuka Kicheko alipofika Clouds kwenye kipindi cha leo tena ilianzishwa segment akawa anapewa muda wake na zinachezwa singeli, sijui hiyo program ilipotelea wapi na Kicheko mwenyewe hasikiki kama zamani, baadae akahamia Jumamosi jioni kabla ya Kipindi cha Peter Moe. Mkazo wa singeli kwa Clouds tena ukawa umeishia hapo.
Efm bado wanalisongesha kipindi cha singeli alichokiacha Kicheko bado kinaendelea na naona mbadala wa Kicheko usajili wake ulikuwa mzuri Semio na Fido wamerudisha hadhi ya kipindi pia wasanii wa singeli bado wanaendelea kufanya show zinazoandaliwa na Efm, mara ya mwisho kuona msanii wa singeli akifanya show iliyoandaliwa na Clouds ni Fiesta 2017, lakini ilikuwa tofauti kwa Fiesta 2016 wasanii wa singeli walikuwa wengi
Nnnachosema msizalau Nazi