Wasanii wa Tanzania msione aibu kumtumia Kenny wa Zoom Production ku-shoot video zenu, eti kwa kuwa kampuni inamilikwa na Diamond !

Adam alikuwa mjuaji sana na alijiona perfectionist akasahau kuwa ubunifu ndio msingi wa kazi. Dharau nyingi ila mwisho wa siku kila jambo lina ukomo wake.

Siwezi mtetea kama Legend ila namuona kama jamaa mmoja tu aliewahi kujua kutumia camera na software ya sony vegas kuunganisha scenes na effects. Video za Adam japo ziliitwa quality ila kwangu mimi it was the era ambayo nilikuwa sina time ya kuangalia video za kibongo kabisa ani. Video zilikuwa very low quality na chafu sana. Wakati ulaya ngoma zilikuwa zinashootiwa na kuhaririwa katika 480p ambayo ni Standard definition.

Alipokuja Karabani nikaanza kushawishika jamaa alikuwa vizuri sana ingawa hakudumu mda mrefu its like kazi alikuwa anafanya kitozi sana. Ndipo akaja Nisher na kuleta mapinduzi ya bongo flava video making nchini. High definition video ya frame ya 720p na Full Hd ya1080i zilianza toka kwa Nisher nakumbuka ilikuwa nyimbo ya DJ Choka nadhani. Adam Juma pamoja na kufyum kote kwenye interviews mbali mbali hakuwahi toa video ya HD nyingi ni 360p. Japo alipoanza kutoa zake za 480p alianzaga kuziita eti HD sijui kwa kutuona wabongo wote mafala.

Instead he started hating on Nisher's productions, badala ajiboreshe kikazi. Kuja kustuka after 2 years wakawa wameibuka Video producers kama uyoga wakali zaidi yake ye akiwa bado anapuyanga tu kina Nick Dizzo wakamkimbiza sana hadi leo ndio tuna kina hanscana, Adam amepotezwa kwenye game japo alifurukuta kujifanya kama Godfather anashutia South Africa video za HD wacha ajifanye kastaafu tu hahaha. Tujifunze kuwa humble wanangu, maisha ni safari ndefu!

Kwangu forever Legend ni P.Funk
 
Adam yah alikuwa ana hate nakumbuka alikuwa haachi kupost ooh yeye ni legend eti akiamua afanye video hakuna atakayeweza kufanya mara sijui nini.
Hata hiyo video ya Linex ilikuwa poor quality sana yani sijui ilikuwa 360p maana ilikuwa ya kiwango cha chini kweli. Linex alilalamiaka sana mdogo wake Adam sijui naitwa Fatuma jina nishalisahau nidye akawa anajibizana na Linex ye Adam alisema yuko tayari kuirudia ndicho alichocommen tu.
Nisher nahisi naye kilichomtoa kwenye game ni kukaa kwake Arusha, na kuna muda alianza kuwa na nyodo nyodo flani akawa anachagua watu wakufanya nao kazi
 
Yah, Nisher was good but baada ya muda nilianza kuona walakini kwenye kazi zake. Color zake pamoja na texture ya video vilikuwa sharp sana. From there niliona kuwa hana mwendo mrefu endapo angetokea mtu wa kusahihisha makosa yake japo kwa effect alikuwa mzuri sana. Nick Dizzo alikuja vizuri sana katika kuziba hayo magepu.

 
Travellah sio mbaya sana , hatoshi kwenye mzani na Hansicana .labda umuwekee na kina Jowzey huko napo ajipange pia
Inamaana hamuoni kaz za Kwetu studio sio? Binafsi travellah ndio funga kazi kwa mwaka huu wote

Sent from my SM-G920P using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
msafiri wa kwetu studio anajua sana...

shida hakatai kazi.. anafanya kazi nyingi hadi zinamzidia ndani ya muda mmoja... kwaya, singeli, nyimbo za bei nafuu hadi za bajeti kubwa yeye anapokea tu...

ndio maana anakuwa kama analipua kazi..

kwa mwezi mmoja kwetu studio unafanya video hata 20.. bado harusi, bado vipindi vya tv.. yaani msafiri anazidiwa kazi...

ila ni anajua sana
 
Travellah sio mbaya sana , hatoshi kwenye mzani na Hansicana .labda umuwekee na kina Jowzey huko napo ajipange pia

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani travella umuweke na hansicana? Hans sjaona video ya maana aliyoshoot kumzid travellah..

Masafir anajua sana...na vifaa anavyo

Alaf jamaa hatabirik,,,kuna video huez jua kama ni travella had pale inapoisha

Ila hans video zake tu unajua ni yeye..mana znafanana tu..alaf quality sio nzur

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
 
Jamaa anashoot video kali sana..nashangaa kuna kuna watu wanataka mfananisha na hanscana...

Mi kwa mwaka jana had mwaka huu bado travella nasema mkali..chupa zake jamaa sio mchezo.

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
 
Tatizo ni bajeti!.. kwenda kushoot zoom production sio mchezo!.. kuna ile ngoma ya g nako arosto.. nisher alishoot vibaya.. ikabidi arudie hanscana ndo ikawa powa
 
Hanscana kazingua sana kazi ya Maua Sama ya - Iokote ,yaani kafanya mavongovongo kibao,location mbovu,waliomfanyia make up Maua Sama wamemuharibu,upande wa mavazi Maua sama na wenzake walivaa hovyo hovyo.
 
Tatizo ni bajeti!.. kwenda kushoot zoom production sio mchezo!.. kuna ile ngoma ya g nako arosto.. nisher alishoot vibaya.. ikabidi arudie hanscana ndo ikawa powa
Inamaana Zoom Production gharama zao ni kubwa sana kuliko Kampuni nyingine ?
 
Hanscana kazingua sana kazi ya Maua Sama ya - Iokote ,yaani kafanya mavongovongo kibao,location mbovu,waliomfanyia make up Maua Sama wamemuharibu,upande wa mavazi Maua sama na wenzake walivaa hovyo hovyo.

iokote bonge ya nyimbo ila video too local..

nazani hanscana aliwaza soko la ndani tu...

harmonise atarudi ni nyimbo ya kiswahili tupu ila video kali hadi soko la nje inauzika... iokote huwezi iona inasumbua trace, mtv etc
 
Inamaana Zoom Production gharama zao ni kubwa sana kuliko Kampuni nyingine ?
wengi bei ni zile zile.. ubora tofauti!.. mfano hanscana watu wanamlaumu video ya iokote alishoot vibaya.. ila ukweli ni kuwa bajeti ilikuwa ndogo ndo maana sallam sk alisemaga toa pesa ili uingize pesa!.. sasa Angelia video ya lavalava nitake nini.. ameshoot hanscana hiyo.. ndo uone alivyofanya powa!.. sababu??.. bajeti ilitolewa kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…