Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Adam alikuwa mjuaji sana na alijiona perfectionist akasahau kuwa ubunifu ndio msingi wa kazi. Dharau nyingi ila mwisho wa siku kila jambo lina ukomo wake.Acha upotoshaji Adam Juma aliondolewa kwenye game, kitu kilichowagombanisha na Nisher ni pale kila Nisher alipokuwa akishoot video Adam anaikosoa hadharani facebook hadi Nisher siku moja akammaindi.
Kama alisema atakuwa anashoot bure mbona video ya Linex na Diamond aliishoot kwa ela na ikatoka mbaya hadi Linex akammaindi sana kuwa amechangia kuufanya wimbo usihiti kwa video mbaya wakati yeye ndiye mtu wa kwanza kumlipa ela nyignie kwenye ile video amemlipa milion4 na hakuna mtu aliwahi kumlipa mlioni 4.
Nikashangaa kumbe wasanii walikuwa wanaongopea mara video nimefanya kwa milion 10 visual lab kumbe hakuna lolote.
Adam akamjibu Linex kuwa yuko tayari kuirudia ile video bure kabisa kama anaona ameiharibu.
Any way Adam alichange mwelekeo wa video za bongo apewe heshima ila ilifika kipindi naye ubunifu wake ukafika kikomo akaondolewa kwenye game huo ndo ukweli.
Siwezi mtetea kama Legend ila namuona kama jamaa mmoja tu aliewahi kujua kutumia camera na software ya sony vegas kuunganisha scenes na effects. Video za Adam japo ziliitwa quality ila kwangu mimi it was the era ambayo nilikuwa sina time ya kuangalia video za kibongo kabisa ani. Video zilikuwa very low quality na chafu sana. Wakati ulaya ngoma zilikuwa zinashootiwa na kuhaririwa katika 480p ambayo ni Standard definition.
Alipokuja Karabani nikaanza kushawishika jamaa alikuwa vizuri sana ingawa hakudumu mda mrefu its like kazi alikuwa anafanya kitozi sana. Ndipo akaja Nisher na kuleta mapinduzi ya bongo flava video making nchini. High definition video ya frame ya 720p na Full Hd ya1080i zilianza toka kwa Nisher nakumbuka ilikuwa nyimbo ya DJ Choka nadhani. Adam Juma pamoja na kufyum kote kwenye interviews mbali mbali hakuwahi toa video ya HD nyingi ni 360p. Japo alipoanza kutoa zake za 480p alianzaga kuziita eti HD sijui kwa kutuona wabongo wote mafala.
Instead he started hating on Nisher's productions, badala ajiboreshe kikazi. Kuja kustuka after 2 years wakawa wameibuka Video producers kama uyoga wakali zaidi yake ye akiwa bado anapuyanga tu kina Nick Dizzo wakamkimbiza sana hadi leo ndio tuna kina hanscana, Adam amepotezwa kwenye game japo alifurukuta kujifanya kama Godfather anashutia South Africa video za HD wacha ajifanye kastaafu tu hahaha. Tujifunze kuwa humble wanangu, maisha ni safari ndefu!
Kwangu forever Legend ni P.Funk