Wasanii wa Tanzania msione aibu kumtumia Kenny wa Zoom Production ku-shoot video zenu, eti kwa kuwa kampuni inamilikwa na Diamond !

Wasanii wa Tanzania msione aibu kumtumia Kenny wa Zoom Production ku-shoot video zenu, eti kwa kuwa kampuni inamilikwa na Diamond !

kama harmonize angekuwa vizuri.. yeye harmonize ndie angekuwa bosi wa diamond.. harmonize kama ni mbwa basi diamond ndie mwenye mbwa.... kwa misaada anayotoa diamond.. kununua camera ni kitu kidogo sana..

mtaji wa vifaa vyote vya video .. haizidi milioni 100... diamond sumbawanga tu katoa msaada milioni 110, tandale katoa msaada zaidi ya milion 200...

mkataba wake wa kuitangaza bellaire.. ni unampa diamond hela nyingi sana na sana... bado show zake na za wasanii wake kina harmonize.. bado wasafi tv shares
Huyo anataka ligi ya kubishana ,achana nae,hao ndio wale Dada Mange Kasema.
 
Kiukweli huyu jamaa kwa sasa ni shida, Anashoot video zenye ubunifu mkubwa na bora sana.


Kumbuka miaka michache iliyopita tulikuwa na Adam Juma lakini kwa bahati mbaya wakati wasanii wakipiga hatua yeye akabaki vilevile, hatimaye akaondolewa sokoni na Nisher.

Nisher kawafundisha kazi kina Hanscana na Khalfan wakatumia nafasi ya kuhamia Dar kumwondoa sokoni Nisher aliyekuwa Arusha.

Miaka miwili nyuma Hanscana alikuwa anatamba kweli kweli, zaidi ya 98% ya video za wasanii ali-shoot yeye. Lakini mpaka leo naona anashoot vilevile sijui uwezo umefika mwisho.

Ssasa naona huyu Kenny video zake balaa lakini wasanii ni kama wanamkwepa fulani sijui kwa kuwa Zoom Production ni kampuni ya Diamond. Akili ya wabongo !!

Hebu tuachane roho za kwanini, ili tupige hatua.


Sample:

1.


2.

3.

Kuna dogo anaitwa Lucca Swahili ni tatizo
 
Mimi mwenyewe najua vizuri vyombo vyote alinunua Diamond SA,naona unataka ligi ngoja tuanze.

Ohooo!!.. 🤣🤣 Hizi ID fake zinafanya mpaka mtu utamani anayekubishia akujue hili aamini unachosema.

Haya baki na unavyoamini.
 
Huyo anataka ligi ya kubishana ,achana nae,hao ndio wale Dada Mange Kasema.

Hakuna aliyesema Diamond hana uwezo wa kumiliki Hiyo Production house.

Ninachokisema ni mmiliki halali 🤣 Mmiliki halali wa Zoom ni Harmonize baada ya kuwezeshwa na mkewe.
 
Okay basi body spray fyn by falsafa ni ya diamond manake umekariri watu wasanii wengine hawawezi fanya kitu
Umedandia treni kwa mbele ndugu yangu,hebu anzia mwanzo nilipoanza kubishana na huyo jamaa,yaani umekurupuka.
 
Naijua vizuri sana Zoom...Vyombo vyote hivyo Camera na vinginevyo Harmonize amepewa na mwanamke wake wa kizungu.

Kapewa pia vyombo vya band na studio ya muziki huyo Harmonize yupo vizuri sana.

Siyo kukremisha najua vizuri ninachosema.
Dah... aisee! Basi kweli Diamond ni mzee wa kiki! Yaani kampuni ya Harmonize halafu Diamond anaitangazia dunia kwamba yeye ndie Founder & Managing Director wa Zoom Production Company huku Harmo mwenyewe kanyuti tu!!!

Kwahiyo Diamond kaajiriwa na Harmonize sio?! Manake Mondi keshawahi kuipigia promo Zoom lakini sijawahi kuona mmiliki Harmonize akiipigia Zoom promo!!

Maisha bhana; yaani kutoka kuwa muuza mitumba ya jero jero na kahawa hadi kumtuma mtu aliyekuwa bosi wako miaka 2 tu iliyopita!!!
 
Okay basi body spray fyn by falsafa ni ya diamond manake umekariri watu wasanii wengine hawawezi fanya kitu
Body spray hiyo ni ya Mwana Fa sababu yeye mwenyewe Fa amesema yake na vile vile Zoom ni ya Mond sababu yy mwenyewe kaandika kwenye page yake ni MD, mbona simple au kama upo BRELA basi tuwekee Documents.
 
Hanscana kazingua sana kazi ya Maua Sama ya - Iokote ,yaani kafanya mavongovongo kibao,location mbovu,waliomfanyia make up Maua Sama wamemuharibu,upande wa mavazi Maua sama na wenzake walivaa hovyo hovyo.
Maua sama hajawahi kujua kuvaa zaidi amezoea kuvaa mashela ya harusi tu.
 
Adam alikuwa mjuaji sana na alijiona perfectionist akasahau kuwa ubunifu ndio msingi wa kazi. Dharau nyingi ila mwisho wa siku kila jambo lina ukomo wake.

Siwezi mtetea kama Legend ila namuona kama jamaa mmoja tu aliewahi kujua kutumia camera na software ya sony vegas kuunganisha scenes na effects. Video za Adam japo ziliitwa quality ila kwangu mimi it was the era ambayo nilikuwa sina time ya kuangalia video za kibongo kabisa ani. Video zilikuwa very low quality na chafu sana. Wakati ulaya ngoma zilikuwa zinashootiwa na kuhaririwa katika 480p ambayo ni Standard definition.

Alipokuja Karabani nikaanza kushawishika jamaa alikuwa vizuri sana ingawa hakudumu mda mrefu its like kazi alikuwa anafanya kitozi sana. Ndipo akaja Nisher na kuleta mapinduzi ya bongo flava video making nchini. High definition video ya frame ya 720p na Full Hd ya1080i zilianza toka kwa Nisher nakumbuka ilikuwa nyimbo ya DJ Choka nadhani. Adam Juma pamoja na kufyum kote kwenye interviews mbali mbali hakuwahi toa video ya HD nyingi ni 360p. Japo alipoanza kutoa zake za 480p alianzaga kuziita eti HD sijui kwa kutuona wabongo wote mafala.

Instead he started hating on Nisher's productions, badala ajiboreshe kikazi. Kuja kustuka after 2 years wakawa wameibuka Video producers kama uyoga wakali zaidi yake ye akiwa bado anapuyanga tu kina Nick Dizzo wakamkimbiza sana hadi leo ndio tuna kina hanscana, Adam amepotezwa kwenye game japo alifurukuta kujifanya kama Godfather anashutia South Africa video za HD wacha ajifanye kastaafu tu hahaha. Tujifunze kuwa humble wanangu, maisha ni safari ndefu!

Kwangu forever Legend ni P.Funk
Watu MNA data za kufatilia watu wengine duuuuh[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] au we ndio nisher nini[emoji3] [emoji3] [emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu MNA data za kufatilia watu wengine duuuuh[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] au we ndio nisher nini[emoji3] [emoji3] [emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
Matukio yametokea nikiwa naona na nina ufahamu. Ni sawa na baba yako anapozungumzia unga wa Yanga enzi za 70's halafu uanze kusema baba ana data za kufuatilia ya watu.
 
Kenny naona ilikuwa nguvu ya Soda.

Ubunifu Umekwisha.

Siku hizi anashoot bora liende.

Video Kama Kainama Feat Ipupa kaacha Margin Nyeusi.

Yope Ndio Kabisaa, Low Quality.

Kiukweli kwa sasa Tanzania tuna washika Kamera tu.

Hanscana na Kwetu Studio Wameboresha Vifaa ila EDITING na UFUNDI bado hauna jipya.
 
Kalaghe video zake zilikuwa zina taste inafanana we video zote indoor na ma rangi rangi lazima ilikuwa zichokwe sema yeye alipoona game linachange akwa amepata deal sijui na shirika gani ya kutengeneza documentary.
Well said mkuu.
Naliona kosa kama hilo kwenye video za Nisher, na huyu Kenny wa Zoom Production.

Kenny anapenda sana rangi flani kwenye background ya vitaa kama vya x-mass au disco light kama hivyo kwenye wimbo wa Lava Lava.
Kenny kama hajaweka taa nilizosema ataweka mwanga au iite mionzi inayopita kwenye mabati meusi.
Amerudia sana hizo pattern kwenye video production zake.
Pia anapenda sana kuweka indoor played scenes.

Nisher alikuwa anapenda kuchoma matairi na kuwasha moto kwenye mapipa na dark /black background.
Nisher alikuwa anapenda sana indoor scenes au night mode scenes.

Mwisho wa siku Kenny anaweza kuchokwa kama hatabadili ubunifu wake.
So far so good hana mshindani bongo, yupo another level. Mwanzo nilidhania jamaa wa nje kama SA hivi kumbe ni local tu.
 
Kenny anajitahidi sana na atamwangusha hanscana si muda mrefu nisher bana sijui pepo gani lilimkumba yule dogo alikua vizuri sana natamani arudi kwenye peak na afanyie video nje ya tz
 
Back
Top Bottom