Wasanii wa Tanzania ni malimbukeni na sitakuja kusaidia hata mmoja!

muafi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
2,557
Reaction score
6,128
Habarini za wasaa huu, napanda jukwaa hill nikiwa na kero kubwa juu ya hawa wahuni wanaojiita wasanii Wa Tanzania

Nimeunganisha dots nikaibuka na conclusion kwamba 80% yw wasanii Wa TZ ni wapumbavu na malimbukeni

Wasanii hawa wanachafua taswira ya Sana'a mpaka inaonekana ni kazi ya kihuni
Tuachane na hayo mengine naomba Leo niongelee swala la ulimbukeni Wa fedha na kujifanya wana fedha sana

Imekua fasheni siku hizi hawa ma celebrity wetu wanajifanya wana hela sana kumbe ni makapuku wananuka vumbi tuu wakati Wa matatizo wanaanza kulialia bila aibu tuwachangie fedha mbw* wakubwa hawa

Wasanii wanajinasibu wanavaa Vito vya thamani kubwa sana utaskia cheni inathamani ya shilingi milioni moja,
Kuna msanii wa aliwai kusema amemhonga mpenzi wake SAA ya shilingi milioni hamsini, hivi kweli hawa watu kichwani kuna kitu kweli?

Kuna watu wanalalamika kitendo cha soudy brown na Maua sama kukamatwa kwa kosa la kuchezea pesa
Mimi kwa upande wangu naomba jeshi la polisi mzidi kuwashikilia hao malimbukeni mpaka watakapopata adabu
Hongereni sana jeshi la polisi na endeleeni kuwashikilia na msiwape dhamana ikibidi washikiliwe mwaka mzima

Hivi visanii vinajifanya kuwa na pesa sana vikipata matatizo vinaomba misaada kwa watanzania pumbavu kabisa

Mweshmiwa mwakyembe hawa wasanii Sio Wa kuchangia pesa hata mia waache wapambambane na halo zao

Juzi nimemsikia queen darlin anajinasibu kwamba nguo alizovaa gharama yake hata siku zetu haziingii,
Diva the bawse anajinasibu anapanga nyumba na analipa USD nyingi tu kwa mwezi, diva anajinasibu hawezi kuolewa na mwanaume asiye na mahali ya milioni 500 halafu diva huyuhuyu anaomba watanzania tumchangie pesa kapandikizwa mbegu, hivi huyu Dada kweli zinamtosha kichwani?

Rayvanny msanii Wa juzi tu saivi anaanza kupost video anafagia hela kana kwamba yeye anapesa nyingi mno halafu jitu kama hili baade lije kuomba msaada
Jeshi la.polisi
Naomba mkamate wote wanaodhalilisha pesa za Tanzania kuanza na diamond na kijakazi wake rayvanny na wengnine wengi tu

Mweshmiwa kangi Lugola a.k.a Ninja tunaomba sana hawa wote waliojirekodi wakifagia na kuchezea pesa tunaomba muwafanyie kitu wawe sampo ili watanzania wengine waone mfano kwao.
 
Msanii ni msanii tu.
Kama mwanasiasa alivyo mwanasiasa
Au mchungaji alivyo mchungaji.

Sio kwamba wanahubiri sanaa halafu wasiishi, wanaiishi pia.

Kijamjazacho mtu moyoni mwake ndicho kimtokacho, kwa hiyo kama sanaa imemjaa mtu moyoni na iko damuni, na kutwa anaigiza maisha kwenye sanaa huko, tegemea pia hata maigizo kwenye maisha yao.

Hili ni suala la dunia nzima sio bongo tu.

Bahati mbaya sana hata wao hawajui kama maisha yao ni maigizo.
 
Nchi inayokataza hata maigizo ya wasanii ni nchi hatari sana.
 

Wasanii Wa mbele pesa wanayo kweli sio hawa wasanii uchwara Wa bongo
Huwezi ukasikia lily Wayne anaomba achangiwe fedha akatibiwe
 
Ila hapo kwenye dhamana mzee upo chaka halafu umeongea kwa jazba sana kumbe yule unashambulia ni msanii ambapo msanii ndani yake kuna maigizo we iga maisha ya wasanii uone.
 
Tukiwasema humu kuwa msiwachangie mnapiga mayowe, Kuna watu wanahitaji misaada kweli ww siku amua kutembelea hospital walau na mfuko wa matunda ndio utajua kuwa kuna watu wanahitaji msaaada kweli zaidi ya hao wasanii
Umeongea point sana barikiwa sana
 
Kuna Mwingine Nimemsikia Kitenge Jana E FM jina limetoka aliyeitwa na Diamond ''Kama watoto wakinililia wapatie...na vibagia'' NITAREJEA anahitaji msaada
 
Sichangiagi msanii hata mia nilipo nimezungukwa na wenye uhitaji zaidi
 
Mm jamn niliishangaa et na marehemu mzee majuto nae alitaka tumchangie huko tulokuwa tunamuona kwny majukwaa ya ccm anacheza mziki.
 
Wasanii Wa mbele pesa wanayo kweli sio hawa wasanii uchwara Wa bongo
Huwezi ukasikia lily Wayne anaomba achangiwe fedha akatibiwe
Si umeshasema mbele mkuu??

Tatizo labda unasahau kuwa unaongelea msanii wa Bongo.
Ni kama kumkuta Mchungaji wa Kitanzania anahubiri mafanikio na kubarikiwa halafu yeye hana hata mia mfukoni huku akiwabana michango lukuki waumini wake.

Simply ni kwamba tatizo ni kuishi Bongo.

Maisha ya wabongo wengi ni ya kuunga unga tu, hata awe mwalimu au Daktari au Professor suala la kuunga unga na kuishi kwa mikopo huwa lipo tu .

Hayo ndiyo maisha yetu.

Kwa nini uwashangae wasanii wanaoomba pindi wanapopata matatizo??
Kwani hujui kuwa wao ni wasanii na maisha yao yamejaa maigizo??
Kwani hujui kwamba maisha ya bongo karibu 98% ya kipato chao kwa mwezi hakifiki Milioni 2??

Je utamshangaa mtoto anayetambaa kumkuta amechafuka na matope wakati unajua kuwa anatambaa?? Hujui matope ni sehemu ya maisha yake?

Utamshangaa mvuvi kukuta amelowana na maji wakati unajua kabia kucheza na maji ni sehemu ya maisha yake??

Utamshangaa mbwa kutotembea kwa utulivu wakati unajua kabisa kuwa yeye ni mbwa??

Utamshangaa msanii wa Bongo kwa kuishi kwa kuomba omba pidni apatapo shida wakati unajua kabisa yeye ni msanii maisha yake ni maigizo tupu na kipato chake kwa mwezi ni chini ya Milioni 2??

Kwani hujawaona waigizaji au waimbaji wa bongo wanarudia mpaka mavazi kwenye video zao??
Kama wanakosa tu mavazi mapya ya kwenda location kwenye kurekodi kwa nini ushangae wakikosa hela ya matibabu pindi wauguapo??
 

Halafu wengi wanishi nyumba zá kupanga.

Maisha yao ni kula, kuvaa na starehe.

Binafsi huwa suspendi haya majitu yanavyo jishebedua utadhani majitu ya maana kumbe machimba chumvi.


Akili za msanii ziko upeo wa nyayo zake. Hawanaga vision ya kesho labda wachache chini ya asilimia 5.

Misifa misifa na kupenda kutambulika wakati mfukoni kapa.


Kifupi wasanii wakibongo hawanaga future plans. Maisha yao kama ng'ombe tu.
 
AISEEE POVU KAMA LOTE VILE.
 
Ujumbe mzuri

ILA


Kama Rroteehh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…