Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wasanii Wa mbele pesa wanayo kweli sio hawa wasanii uchwara Wa bongo
Huwezi ukasikia lily Wayne anaomba achangiwe fedha akatibiwe
True✔✔Halafu wengi wanishi nyumba zá kupanga.
Maisha yao ni kula, kuvaa na starehe.
Binafsi huwa suspendi haya majitu yanavyo jishebedua utadhani majitu ya maana kumbe machimba chumvi.
Akili za msanii ziko upeo wa nyayo zake. Hawanaga vision ya kesho labda wachache chini ya asilimia 5.
Misifa misifa na kupenda kutambulika wakati mfukoni kapa.
Kifupi wasanii wakibongo hawanaga future plans. Maisha yao kama ng'ombe tu.
Ndio maana unapokua kazini kama wewe ni msanii igiza kwa scene unayoifanyia kazi, nje ya usanii jiweke kwenye maisha yako halisi ili watu wakuelewe. tatizo mademu wanajipaisha ili wapate mabuzi yenye hela, na mabishoo yanajipaisha ili yapate mademu wenye chati. Huku hawajui kwamba wabongo wote ni wasanii mpaka mtoto mdogo. Mimi kwa kweli hawa wasanii nitaendelea kufumua mpaka akili ziwakae sawa...!!! Na nitawaacha endapo tu akili zitawakaa sawa.Si umeshasema mbele mkuu??
Tatizo labda unasahau kuwa unaongelea msanii wa Bongo.
Ni kama kumkuta Mchungaji wa Kitanzania anahubiri mafanikio na kubarikiwa halafu yeye hana hata mia mfukoni huku akiwabana michango lukuki waumini wake.
Simply ni kwamba tatizo ni kuishi Bongo.
Maisha ya wabongo wengi ni ya kuunga unga tu, hata awe mwalimu au Daktari au Professor suala la kuunga unga na kuishi kwa mikopo huwa lipo tu .
Hayo ndiyo maisha yetu.
Kwa nini uwashangae wasanii wanaoomba pindi wanapopata matatizo??
Kwani hujui kuwa wao ni wasanii na maisha yao yamejaa maigizo??
Kwani hujui kwamba maisha ya bongo karibu 98% ya kipato chao kwa mwezi hakifiki Milioni 2??
Je utamshangaa mtoto anayetambaa kumkuta amechafuka na matope wakati unajua kuwa anatambaa?? Hujui matope ni sehemu ya maisha yake?
Utamshangaa mvuvi kukuta amelowana na maji wakati unajua kabia kucheza na maji ni sehemu ya maisha yake??
Utamshangaa mbwa kutotembea kwa utulivu wakati unajua kabisa kuwa yeye ni mbwa??
Utamshangaa msanii wa Bongo kwa kuishi kwa kuomba omba pidni apatapo shida wakati unajua kabisa yeye ni msanii maisha yake ni maigizo tupu na kipato chake kwa mwezi ni chini ya Milioni 2??
Kwani hujawaona waigizaji au waimbaji wa bongo wanarudia mpaka mavazi kwenye video zao??
Kama wanakosa tu mavazi mapya ya kwenda location kwenye kurekodi kwa nini ushangae wakikosa hela ya matibabu pindi wauguapo??