Si umeshasema mbele mkuu??
Tatizo labda unasahau kuwa unaongelea msanii wa Bongo.
Ni kama kumkuta Mchungaji wa Kitanzania anahubiri mafanikio na kubarikiwa halafu yeye hana hata mia mfukoni huku akiwabana michango lukuki waumini wake.
Simply ni kwamba tatizo ni kuishi Bongo.
Maisha ya wabongo wengi ni ya kuunga unga tu, hata awe mwalimu au Daktari au Professor suala la kuunga unga na kuishi kwa mikopo huwa lipo tu .
Hayo ndiyo maisha yetu.
Kwa nini uwashangae wasanii wanaoomba pindi wanapopata matatizo??
Kwani hujui kuwa wao ni wasanii na maisha yao yamejaa maigizo??
Kwani hujui kwamba maisha ya bongo karibu 98% ya kipato chao kwa mwezi hakifiki Milioni 2??
Je utamshangaa mtoto anayetambaa kumkuta amechafuka na matope wakati unajua kuwa anatambaa?? Hujui matope ni sehemu ya maisha yake?
Utamshangaa mvuvi kukuta amelowana na maji wakati unajua kabia kucheza na maji ni sehemu ya maisha yake??
Utamshangaa mbwa kutotembea kwa utulivu wakati unajua kabisa kuwa yeye ni mbwa??
Utamshangaa msanii wa Bongo kwa kuishi kwa kuomba omba pidni apatapo shida wakati unajua kabisa yeye ni msanii maisha yake ni maigizo tupu na kipato chake kwa mwezi ni chini ya Milioni 2??
Kwani hujawaona waigizaji au waimbaji wa bongo wanarudia mpaka mavazi kwenye video zao??
Kama wanakosa tu mavazi mapya ya kwenda location kwenye kurekodi kwa nini ushangae wakikosa hela ya matibabu pindi wauguapo??