Kwa asili, kazi kuu ya msanii ni kutoa burudani. Na walaji wakuu wa kazi hizi kwa asilimia kubwa ni wananchi wa kawaida, watu wa mtaani, vijana, akina mama, na wapiga kura wa taifa hili. Hawa si serikali, si viongozi, bali ni watu wanaohitaji sauti, matumaini, na faraja kupitia sanaa.
Lakini kwa kipindi cha hivi karibuni, tumeanza kushuhudia mabadiliko yanayotia mashaka: wasanii wengi wa Tanzania wamekuwa wakijihusisha moja kwa moja na chama tawala. Kikatiba, hii ni haki yao. Hakuna anayeweza kuwazuia kushiriki siasa au kuunga mkono chama chochote wanachotaka.
Hata hivyo, kinacholeta taharuki ni namna wanavyoshiriki, si kama raia huru wanaotoa maoni yao, bali kama "vijakazi wa propaganda", wakigeuka vipaza sauti vya serikali inayolaumiwa na wananchi kwa kukandamiza haki za msingi.
Tofauti ni kubwa ukilinganisha na wasanii kutoka mataifa kama Kenya, Afrika Kusini, Nigeria au Marekani, ambao mara kwa mara hutumia jukwaa lao kupaza sauti dhidi ya udhalimu, kupinga sera kandamizi, na kusimama na watu wa kawaida. Wasanii wa Tanzania, badala ya kuwa kioo cha jamii, wanaonekana kupoteza mwelekeo, wakifanya "spinning" ya kisiasa, wakitumiwa kuwahadaa wananchi kupitia kiki, video za utupu, bifu za kutengenezwa, na matamasha yenye ajenda fichu za kisiasa.
Katika kipindi hiki nyeti cha kuelekea uchaguzi, ambapo wananchi wanatafakari mustakabali wao wa miaka mitano ijayo, ni jambo la kusikitisha kuona wasanii wakitumika kama njia ya kuwatoa watu kwenye fikra sahihi za kujitathmini na kufanya maamuzi yenye uzito. Badala ya kuelimisha au kuburudisha kwa uwazi, baadhi yao wamejigeuza kuwa njia ya kuendesha propaganda. Sio kwamba hawaruhusiwi kushiriki siasa, lakini hata wale waliopata nafasi bungeni kama wawakilishi wa sanaa akina Babu Tale, Mwana FA, Jokate, Nikki wa Pili n.k, wameshindwa kusimama imara kwa ajili ya wananchi waliowachagua.
Huu ni wakati wa kujiuliza: 'msanii unamtumikia nani?' Serikali au wananchi? Wanasiasa wamekuwa wakiwatumia wasanii kwa zaidi ya asilimia 80 kwenye mikutano ya kisiasa, huku asilimia ndogo ya muda ikitumiwa kutoa ujumbe wa sera kwa wapiga kura. Huu ni ujanja wa kisiasa unaolenga kupumbaza akili za watu kwa njia ya burudani.
Tunawaambia wasanii: kama hamwezi kusimama upande wa wananchi, basi angalau fanyeni kazi yenu ya burudani kwa heshima na utu. Msigeuke chombo cha propaganda. Mwananchi ni mlaji wenu namba moja. Acheni kupoteza imani yao kwa kutumiwa kisiasa. Ni wakati wa kila mmoja kutafakari wajibu wake kwa taifa, na kwa upande wa wananchi, huu ni wakati wa kutafuta utulivu wa kiakili, kutathmini kwa kina, na kuamua: "je, twahitaji kupiga kura kwa mfumo huu huu, au ni wakati wa kudai mabadiliko ya kweli?"