Wasanii, Waandishi kushuhudia ujenzi wa Standard Gauge Railway(SGR)

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368


WASANII wa fani tofauti na waandishi wa habari Alhamisi wiki hii watafanya ziara kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC). Mratibu wa safari hiyo, msanii wa lamu Steve Mengele 'Nyerere' ameupongeza uongozi wa TRC kwa kutambua mchango wa wasanii katika jamii na kuwapa fursa.

Nyerere amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kufanikisha safari hiyo itayojumuisha waimbaji wa muziki wa bendi, bongo eva, taarabu, singeli, waigizaji wa lamu, bongo movie, komedi, wachezaji wa zamani wa mpira wa miguu na waandishi wa habari wa vyombo wakiwemo wa mitandao ya kijamii.

Wasanii na waandishi wa habari wameelezwa jijini Dar es Salaam kuwa, safari hiyo itaanza saa moja asubuhi kwa treni ya TRC kutoka eneo la Kamata jijini Dar es Salaam na kupitia maeneo yote ambayo mradi huo unatekelezwa. Wakati wa safari wahandisi wa reli watakuwa wakitoa maelezo kuhusu ujenzi wa mradi huo mkubwa.

Nyerere pia amewaeleza wasanii kuwa, kuna mikopo inayotolewa kwa wasanii kupitia Halmashauri za mkoa wa Dar es Salaam kutekeleza sera ya Serikali inayoziagiza mamlaka hizo kutenga asilimia 10 ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya mikopo ya vijana, walemavu na wanawake. “Mkuu wa Mkoa Paul Makonda anakaribisha maombi ya mkopo kwa wote wanaohitaji mikopo aliyohaidi wakati wa mkutano wa wasanii wa maigizo waimbaji wa muziki wa bendi, bongo eva, taarab, singeli, waigizaji wa lamu, bongo movie, komedi , wachezaji wa zamani wa mpira wa miguu na waandishi wa habari nchini kuweza kupata mkopo huo utakaowezesha kufanya kazi kwa weledi na kukuza kipato kwa tasnia zote nchini.” amesema Nyerere.

Kaimu Mkuu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TRC Jamila Mbarouk amesema safari hiyo ni fursa kwa wasanii na waandishi wa habari kwenda kuona mradi wa ujenzi wa SGR unavyotekelezwa. Mbarouk amesema Safari hiyo itasaidia kutangaza utalii uliopo ndani hasa kuwepo kwa treni hiyo ya umeme ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo ya tani elfu 10 huku spidi yake ikiwa ni kilomita 160 kwa saa.

“Shirika la reli (TRC) limewapa kipaumbele wasanii ,wacheza mpira, ma MC ,waimbaji, wachekeshaji, waigizaji wa lamu na wengine ambao wanaweza kuwa mabalozi wazuri katika kuutangazia umma kuhusu mradi huo wa treni mpya ya umeme itakayotoka Dar es Salaam -Morogoro hadi Dodoma ” amesema Mbarouk. Amesema, reli hiyo inajengwa kwa fedha za Watanzania kutokana na kodi. Ametoa mwito kwa wafanyabiashara kulipa kodi kwani mradi huo ukikamilika utasaidia kukuza uchumi pia kwa wafanyabiashara kwa kusarisha bidhaa zao na mizigo kwa haraka zaidi.
 
Kuna watu wanaishi mjini kiujanjaujanja sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumekupata TIVU ake! [emoji4]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Muda muafaka kaka ndo huu/ stuka masista duu wanang'aka taka vya juu.

Eti huyo wa katikati nae anaenda kukagua SGR
 
People are not interested anymore, Yaani wanapoteza wese ili wakashangae tu
 
hao wanaoenda kukagua huo mradi hata ukiwauliza SGR kirefu chake ni nin hawajui.
 
Steve Nyerere ni genius huyu jamaa.
Hawezi kulala njaa kiboya anazijua fursa na anajua muda sahihi wa kuzichangamkia.

Siku upinzani ukishika nchi utashangaa atakavyobadiri gia angani ili apige fursa za utawala mpya.

Watu kama hawa unaweza kuwachukulia easy lkini ndio wanaosurvive hata vita vya nuclear..

Maana akili na ujasiri wa kupiga hela za rambirambi sio za kawaida...jamaa IQ yake ya kusurvive ni kama 120+

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana wasanii kwa uzalendo..
Safi sana Steve hahahaha
 
Kwa aina hii ya wasanii tuliokua nao, bora niendelee tu kuwa mtumwa wa Korean drama! Yeeh Pehaa!! Hatari sana.
 
Kuna ile katuni ya masoud kipanya aliunga na caption kuwa mjinga wa kwanza na mjinga wa mwisho nani ni mjinga zaidi
Hao ndio wasanii wa movie na vijana wanaojiita wa ccm [emoji40]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…