Nmeona list ndefu humu za wasanii wa muziki wametajwa kwa interest zetu tu.... Ndg zangu muziki ni sanaa km zilivyo sanaa nyingine km uigizaji, sarakasi nk, muziki una aina tofauti tofauti katika uimbaji wake km vile RnB, Hip Hop, dance, taarab nk(kwa hapa kwetu) hivyo tunapoanza kuwa kosoa wasanii wetu lazima tuangalie makosa ktk aina ya muziki anaouimba msanii husika.... Ni kweli kuna wasanii ambao hawafit kwenye aina yeyote ya muziki lakini ni mapenzi yao kufanya muziki so hatuwezi kumzuia mtu kufanya kitu anachokipenda.... Muhimu hapa ni kwamba km msanii flani humpendi au huelewi muziki wake achana naye wapo wanaopenda na kuelewa kazi zake, japo kukosoa, kupenda au kutokupenda ni haki yetu pia, sikiliza na fuatilia kazi za msanii unayempenda bt usiwakwaze watu wengine kwa mapenzi tu