Kwa muda mrefu sana wasanii mbalimbali wwamekuwaa music, maigizo ulimbwende n.k wanapenda kujinasibu kuwa wao ni vioo vya jamii....
NDIYO! Wasanii wetu ni kioo cha jamii na wataendelea kuwa kioo cha kuonesha taswira ya Watanzania!
...kwa maana hiyo jamii inapaswa kuwaiga mambo yao
Inapaswa kuwaiga kivipi?! Kama ilivyo kwa wengi, nawe inaonesha hufahamu maana ya wasanii kuwa kioo cha jamii!
Narudia: NDIYO, wasanii ni kioo au wanapaswa kuwa kioo cha jamii! Hii haimaanishi uige wafanyacho wasanii bali wasanii hutoa taswira halisi ya jamii!
Hata wewe unapojiangalia kwenye kioo utaona taswira yako halisi lakini haujiangalii ili uige hiyo taswira!
Sasa basi, tumchukulie mtu kama Diamond... yule ni kioo cha jamii halisi ya Kitanzania! Mtu aliye Ghana anaweza kupata taswira ya Watanzania kwa kumwangalia Diamond!
Kiukweli kwa mambo ambayo wanayanya hawa wasanii mengi yao ni machafu kabisa. Mifano michache tu, wao ndo wamekuwa vinara wa madawa ya kulevya, ngono, picha chafu za ngono, uvaaji mbovu kabisa ambao watoto wetu wanaiga na mengine kibao.
Nimekuambiaje?! Si umeona sasa? Nini hapo ambacho hakifanywi na Watanzania tena kwa uwingi wao?
Kumbe Chid Benz awapo Mombasa na kuweka wazi uteja wake, hapo atakuwa anaonesha taswira (kazi ya kioo) halisi ya maelfu ya Watanzania ambao ni mateja.
Dada zetu wasanii wanapovaa nusu uchi; hapo napo hakuna jipya manake nao wanaonesha taswira halisi ya malaki ya wadada wa Kitanzania wanaovaa nusu uchi!!
Bila shaka ukikutana na Msanii mdada toka Zanzibar, most likely atakuwa amevaa vizuri na huenda hata kwa kujihifadhi kwa sababu yeye ni kioo kinachotoa taswira halisi ya Wazanzibari!