Wasanii walioathiriwa na Diamond

Wasanii walioathiriwa na Diamond

Belle wimbo wake wapili ni masogange,mbona ilikuwa kali tu.Na ametoa ngoma nyingi tu kali baada ya hapo but still raia wanazichukulia kawaida, mfano hizi alizoachia hivi karibun 'Listen' na 'Wanitaka' zote kali

Duuh listen wimbo wa siku nyingi sana, unamiaka miwili sasa. Huo wanitaka sawa japokuwa nao unamiezi ya kutosha.
 
Hivi speaking of marlow where the hell is besta. Yule mke wake
 
Linex anaimba kwaya siku hizi wimbo wake mpya ni kama pambio. Na kwenye video ndio katokea kama mwanga.

Haha nimekumbuka Linex amewahi kukuchana kwamba hakujui thats y unamchukia hehe
 
Tathimini yako ya uongo kila mtu ana fans wake hiyo yakusema kama sio diamond wangewika ni uongo asilimia 100%
 
Hawa ni baadhi ya wasanii ambao kwa mtazamo wangu wana bahati mbaya kwa kuvuma kipindi ambacho anavuma Diamond,i mean isingekuwa uwepo wake kwenye game kwa wakati huu wangepata attention/tuzo nyingi but uwepo wa jamaa umekuwa tatizo kwao coz akili za watanzania wengi kwa miaka hii zimetekwa na Diamond kwa either mziki wake or habari zake, (mfano hai humu JF kwenye hili jukwaa utakuta thread nyingi kadominate yeye).Ni kama kwenye kabumbu kuna kamsemo,'Asingekuwepo Messi tuzo zote za uchezaji bora angekuwa anazichukua Ronaldo'.Kwa vipaji na ukali wa nyimbo zao hawa nahisi wangekuwa mbali zaid ya walipo sasa (kwenye kivuli cha Diamond);

1. Belle9
2. Rich Mavoco
3. Barnaba
4. Ben Pol
5. Linex

Asee ningependa na kijana wa nakshi nakshi ally kiba awekwe hapo....maana toke Diamond katakeover hatumsikii
 
Asee ningependa na kijana wa nakshi nakshi ally kiba awekwe hapo....maana toke Diamond katakeover hatumsikii

Ila kipindi kile anahit sana Diamond hakuwepo kwenye ramani so ashukuru Mungu kwa hilo pengine angekuwepo Diamond asingehit kabisa
 
Tathimini yako ya uongo kila mtu ana fans wake hiyo yakusema kama sio diamond wangewika ni uongo asilimia 100%

Inaathiri ndio, mfano hai kwenye tuzo za mwakahuu za Kili, Diamond kachukua kwenye categories zote alizowekwa kupitia wimbo mmoja tu, na sio kwamba nyimbo nyingine sio kali/hakuna wasanii wengine waliostahil miongoni mwa hizo tuzo alizochukua jamaa la,ni kwamba Diamond kadominate kwenye mioyo ya wapenz wengi wa muzik bongo kiasi kwamba mashabik/media haziwapi attention sana wasanii wengine hata kama wanatoa nyimbo kali. Jaribu kuzitafuta nyimbo zote za Rich Mavoko na uzisikilize vizuri, its a shame hana tuzo hata moja
 
Huu wimbo mimi ni mmojawapo ya watu tuliomshauri sana Marlaw haupeleke radio niliukuta studio Iringa tukasikilizishwa na mdau mmoja wa kuitwa Temi. Moja kati ya vitu navyojivunia kwenye tasnia.

Hapa napata shida kukuelewa, nyimbo aimbe Marlaw halafu wewe ndio ujivunie kazi yake? Bado sioni any connection, ungekuwa ni producer au DJ ningekuelewa.
 
Hapa napata shida kukuelewa, nyimbo aimbe Marlaw halafu wewe ndio ujivunie kazi yake? Bado sioni any connection, ungekuwa ni producer au DJ ningekuelewa.

hahaha!
 
Hapa napata shida kukuelewa, nyimbo aimbe Marlaw halafu wewe ndio ujivunie kazi yake? Bado sioni any connection, ungekuwa ni producer au DJ ningekuelewa.

Uwezi kunielewa sababu haya mambo ya muziki yana njia zake ambazo mtu asiyezijua ni ngumu kupata connection...maana wewe kwa iq yako unadhani mtu kutoka ni either kipaji chake,producer au dj anayecheza wimbo.

Njoo mitaa uhone talents halafu waulize kinachowashinda nn kutoka utapata jibu zuri sana.

Au uliza artists huwa wanampa Fella million 2 za nini awasambazie nyimbo wakati stations zote wanajua milango ilipo
 
Ruge aliusikia akiwa Morogoro huu Wimbo, moja kwa moja akatafuta mawasiliano yake na kumhamishia Dar. Bembeleza ni bonge la wimbo kwa miaka mingi zaidi. Ni mkono wa Tudd Thomas aliyenyonga ngoma ya Mdogomdogo ya Diamond.
Siasa ndio zilizomuangusha Marlaw, ila jamaa anasauti kama msasa laini unasuguliwa kwenye tikiti maji. Namheshimu sana.
Ova

Mkuu kuna mahusiano gan kati ya siasa na kushuka kwa marlow? Mbona diamond kafanya sana kazi na CCM na ndo huyu anawakimbiza wengine?
 
Mkuu kuna mahusiano gan kati ya siasa na kushuka kwa marlow? Mbona diamond kafanya sana kazi na CCM na ndo huyu anawakimbiza wengine?

Hakuna msanii aliyefanya kazi nyingi za CCM kama Marlaw na Bushoke (mtoto) ambao walitunga wimbo kabisa wa kusifia CCM na wote wakapotea. Diamond alitumbuiza tu, tena sio kwa matukio mengi kama ilivyokuwa kwa wasanii wengine wengi.
 
Back
Top Bottom