Kwa taarifa yako. Yote mabango ya Chagua JK yametolewa Mbeya nzima
sugu chonde chonde nenda ukawatetee wenzako na uache kuwa na visirani nao.
Kumbuka to forgive and forget
Akihojiwa na Bongo Radio msemaji wa Joseph Mbilinyi a.ka Mr. Sugu(MB elect) ndugu G. Solo amesema kuna baadhi ya wasanii waliokuwa wakimpiga vita Sugu kwenye majukwaa ya CCM wameanza kujipendekeza, amesema wengine walikuwa wanakwenda Mbeya kufanya Shoo makusudi ili kumchafulia Sugu bila hata kumsalimia leo wameanza kumpigia simu. Lakini anawapa live kuwa wao waendelee kutumiwa tu na CCM kama mipira na baadaye kutupwa na yeye anaenda bungeni kuwatumikia wananchi ikiwa ni pamoja na masilahi yao(wasanii).
Unamaanisha ile ya kiume ?
Hahahahaha! Mimi namkumbuka Nakaya tu! Lol masikini ya Mungu!
Nakaya ni mnafiki wa kutupwa na nimeapa kamwe sitosikiliza nyimbo zake wala kumpa sapoti ya aina yoyote ile, Mr. Politician kumbe ilikuwa ni kwa manufaa yake binafsi, shame on you Nakaya tulijua tumepata binti jasiri mwenye msimamo na uchungu wa nchi yake kumbe hovyooooooo mbinafsi mkubwa. Wewe na wengine wote ya aina yako ni kichefuchefu kwa watanzania.