Wasanii waliopotelea "Majuu" kuna faida yoyote?

Ngonepi

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2013
Posts
1,872
Reaction score
1,207
Kuna kumbukumbu za vijana mbalimbali ambao kutokana na maisha yalivyowaendea hapa nyumbani waliamua kutorokea ughaibuni.
Niwengi sana watu waliotorokea nnje.

Kwa kumbukumbu zangu nawakumbuka vijana au wasanii wetu kadhaa wa mmuziki wa kizazi kipya kama Balozi Dola soul, Solo Thang, Mad Ice, footballer Renatus Njohole na weengi wengine.

Vijana hawa wengi wao wakiwa huko hupata wanawake wa kizungu na kuanzisha maisha ya kifamilia ili kuweka uwepesi wa wao kuishi nchi ya ugenini.
Bahati mbaya watoto wanaozaliwa katika mahusiano haya huwa hawajui nchi alikotoka baba na mara chache hata wanawake zao hawa huwa hawataki kabisa kuja Afrika.
hii hupelekea kizazi kupotelea ughaibuni na vijana wetu kuwa kama wao ndio walioolewa huko Ulaya!!

Maoni yangu ni kwamba vijana tuwe wavumilivu na tukubali kupambana na maisha yetu hapa Afrika na kukataa kuolewa na wazungu ulaya na Marekani huku tukiachia familia zetu hali ya sintofahamu kuhusu kijana wao aliye ulaya ambae hawana faida nae wala undugu na kizazi anachoanzisha ulaya kikiwa hakina faida yeyote nyumbani!!!
 
Umeongea ukweli maana ndio inakuwa mwisho wa ukoo asa ukiwa mtoto wa kiume.

Watoto wanakuwa hawajui chochote kuhusu nyumban Afrika .Inabidi kuwaleta mara kwa mara waone maisha ya Afrika ata hapo baadaye wakiwa na uwezo wanaweza kusaidia na pato likakua.Kama wanavyofanya jirani zetu wa Kenya.

Zaidi ya Dollar Billion 1.5 zimetumwa na wakenya nje,wakati Tanzania tumetuma million 200 tu
 
hivi Sna Lee (Snop Lee) mdogo wake Baucha nilisikia alizamia Germany kipindi cha 2000's toka aondoke sijawahi kuskia hata fununu kama bado yuko hai
 
inasikitisha sana. pole rah p kwa yote yaliyokukuta ugaibuni.
 
Warudi bongo kufanyaje?? Nchi yenyewe hii rais kilaza unategemea atatufikisha wapi??

Uzalendo kafa nao Nyerere, wacha sie tugawane vilivyopo
 
hivi Sna Lee (Snop Lee) mdogo wake Baucha nilisikia alizamia Germany kipindi cha 2000's toka aondoke sijawahi kuskia hata fununu kama bado yuko hai

Alikuwa bongo juzijuzi nadhani hii july hata idd kalika kwao znz , mcheki kwenye profile lake facebook au angalia kwenye profile la yule anayejiita Ali Baucha yupo..!
 
Kuna yule DJ yusuph mzee wa mambo mazuri yako mbele kwa mbele Naskia sahizi kawa mujahidin yuko zake warabuni!
 
Mad ice ni mganda au mtanzania....??

Mad Ice ni mganda lakini naye ni mfano wa vijana ambao wamekimbia Afrika na kizazi chake hakitarudi tena Afrika kwa kuwa watoto wanaozaliwa kwenye ndoa zao hawafundishwi chochote juu ya Nyumbani kwa baba yao na wala kumjua Shangazi au baba mdogo wala mkubwa!!
 
Kwa katiba hii...mi mwenyewe nataka kutokomea mbali huuuukoooo....na nisipakumbuke kabisa

Hutakiwi kukata tamaa, pamoja na madhila meengi tufanyiwayo na viongozi walafi wa Afrika bado hapa ninyumbani na tusizikimbie koo zetu na kukubali kuurudia utumwa!!
 
Ok wazo zuri tunaifanyia kazi.
 
Solo Thang mtoto pori, kwao Mbagala!! Kajaribu mara kadhaa kwenda majuu lakini ilishindikana, niliposikia kafanikiwa nilijua tu hawezi kurudi tena!! Na ndiyo yalotokea

lakina haina faida kwao, ikitokea amefariki huko majuu mwili wake utachomwa moto na kuzikwa,
hapa bongo hatakuwa na alama yeyote ile!!
Kifupi hina faida kifamilia!!
 
Solo thang alijilipua kakaa sana hostel za liverpool now raia wa ireland
 
Asikwambie mtu unapaswa ujijenge kwanza Home huko unaenda tu kama kina Dangote, Dimpoz, Kiba wanavyoenda , Nyumbani mambo yote hawanaga uvumilivu tu .....siku hizi kwenda nje ni kama kwenda Kimanzichana tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…