Uchaguzi 2020 Wasanii wameharibu sana kampeni za CCM, Wiki ya mwisho kuelekea uchaguzi inatia huzuni

Uchaguzi 2020 Wasanii wameharibu sana kampeni za CCM, Wiki ya mwisho kuelekea uchaguzi inatia huzuni

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Nimerudi safari na kupiga kambi kwenye jimbo langu la uchaguzi. Mambo niliyoshuhudia wiki hii ya mwisho hayakufikirika miaka ya nyuma na hata mwanzoni mwa kampeni za mwaka huu.

Vile vijembe vya CCM kwa nyimbo za John Komba vimebadilika sana.

Nimehudhuria mikutano kadhaa ya kampeni ya vyama vitatu hasa CCM, CHADEMA NA ACT Wazalendo.

Ukweli ni kuwa mahudhurio kwenye mikutano ya CCM ni dhaifu sana pamoja na kutumia kivutio cha midundo ya kizazi kipya.

Juzi moja nilishuhudia vumbi likitimka mwanzo mpaka mwisho watoto wakicheza ngoma na hata mgombea mwenyewe hakupata muda vizuri kuhutubia na kutaja sera za chama chake

Watu waliokwenda kumsikiliza wakapungua muda baada ya muda na mpaka muda wa kufunga kampeni walibaki wachache sana waliovalia kijani.
 
Back
Top Bottom