Wasanii wanaodaiwa kutumia madawa ya kulevya, ni yupi anayekusikitisha?

Kwenye kipindi cha Friday night live kinachorushwa na East Africa Tv kuanzia saa tatu mpaka saa tano usiku ..Blue alipokua anahojiwa na Sam Misago kuhusu
matumizi ya madawa ya kulevya alidai kua hapa namnukuu "kukaa miaka miwili mitatu bila kupiga picha na mtu au kusalimiwa unapata stress babaa"
Means sababu ya wasanii wengi wa bongo kutumia "ngada" ni stress za maisha na kutegemea kua maarufu .duuh asipokua maarufu anakula dawa...hayaa...nawasilisha sababu moja wapo ya kutumia ngada ni stress za umaarufu
 
Ray C

Mdada aliye jiingiza katika madawa ya kulevya na kupelekea kuharibu ndoto zake zote kimuziki na maisha kwa ujumla

Chidy benz

Ni msanii wa hip-hop aliye tokea lupendwa sana hapa tanzania …sasa kajiingiza katika madawa ya kulevya japokuwa alisaidiwa na babu tale ila yaonyesha karudia tena na khali yake kwa sasa ni mbaya sana

Loyd eyes

Kijana wa kiarusha toka kundi la weusi ,aliondolewa katika kundi kutokana na tabia zake za madawa ya kulevya ,ray c alimshutumu kuwa yeye ndiyo chanzo cha kumfanya ray c atumie madawa ya kulevya ..Huku yeye akijitahidi kurudi kimuziki,wenzake ndo wako juu kwa sasa na washapenya hadi anga za kimataifa.

Young D

Mtoto mdogo ambaye ameathiliwa na makundi anayo ambatana nayo pia kuiga maisha ya wasanii wa nje ndiko kuliko mpelekea young d msanii mwenye kipaji kikubwa kujiingiza katika kundi la watumiaji wa madawa ya kulevya na kufanya kuporomoka kimuziki kwa kiasi kikubwa.

Fanani

Huyu ni moja ya wakongwe wa muziki wa bongo akitokea katika kundi la hbc akiwa pamoja na professor j ambaye kwa sasa ni mbunge wa mikumi.Fanani mwenye kipaji kikubwa alijiingiza katika madawa ya kulevya na kupelekea kuharibu ndoto zake zote za maisha kiujumla.

Daz baba

Msanii toka kundi la daz nundaz aliyewika na ngoma ya umbo namba nane enzi hizo na kuweza kuteka kabisa tasnia ya bongo fleva tanzania nzima ,leo hii naye khali yake sio nzuri kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya

20 percent

Huyu ni mshindi wa tuzo 5 za kilimanjaro kutokana na uimara wake katika utungaji pia katika kuimba nyimbo zenye ujumbe mzito kwa jamii,leo hii kapotea kabisa kutokana na madawa ya kulevya.

Ferooz

Ferooz msanii aliyeweza kupewa zawadi ya gari na mheshimiwa rais wa awamu ya tatu mkapa kutokana na uimara wake wa kuimba nyimbo ya ukimwi akimshirikisha professor j.Hakika ni mtu ambaye hakujipanga ipasavyo leo hii ilibidi awe ni mtu mwenye mali zaidi hata ya diamond lakini kutokana na kuto angalia mbali leo hii ferooz ni mtu ambaye ukimuona huwezi amini hakika madawa hayafai katika jamii.

KR

Kr mullar mwanzilishi wa style ya mapanga katika uchezaji,leo hii kr ni mtu wa kumuonea huruma kutokana na jini alivyo chezea nafasi aliyo kuwa nayo kipindi kile ,madawa ya kulevya yasemekana kuwa chanzo cha yote haya.Hivi juzi picha zake zilisambaa zikionyesha akiwa kalewa hajitambui mchana kweupee.
 
Wanataabika na mateso ya muda mrefu kwa raha ya karaha kwa fedha zao wakati wauzaji waanaishi maisha ya anasa
 
Wapambane na hali zao.
Ila aisee ukimuona mla ngada akiwa na arosto utamonea huruma.
 
Nogesha na tupicha apdated mkuu
 
Next one is Kiba mana yeye shisha anatumia sanaa hadi anashindwa kupigia promo kazi zake-
 
Katika hii list sitaki kuthibitisha kua wote ni watumiji lakini kwa kiasi kikubwa Wengi wamepotea kwenye gani kwa sababu ya haya matatizo.
  1. Chid Benz
  2. Ray c
  3. Feroz
  4. Mangwea(R.I.P)
  5. Maloo
  6. 20%
  7. Nature
  8. Misosi
  9. Inspekta Harpoon
  10. Side Mnyamwezi
Let's go in a right way to eradicate this disaster.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…