Mimi ni shabiki wa DP, naona kabisa anayo nafasi ya kufanya makubwa zaidi kwenye career yake ila ni kama ameridhika alipofika. Maana akifanikiwa kupenya soko la Marekani hata mapato yake yatakuwa makubwa hasa kwenye upande wa deals. Tems sasa hivi anapata deals za Reebok. A Boy from Tandale deals zake ni za Serengeti na Niceone na makoto ya chama.
Connections muhimu, Tems ashajisogeza kwa Rihanna, Dua Lipa, Drake. Wakati DP ana-post Travis Scott akicheza wimbo wa Komasava, Tyla ameshafanya kazi na Travis. Diamond aondoke Tandale, soko la nyumbani na Africa ameshalipata bado huko Duniani.