Muziki wa Nigeria hauna mashairi mazuri na wala hauna maudhui bali ni wajanja wa melodic flows na beats.
Kikubwa zaidi wanachozizidi nchi zote za Africa na aggressiveness kwenye kuusukuma mziki wao kwenye masoko, Davido nimemsikia juzi kati akihojiwa(he was in the US) akasema shukrani zao kubwa ziwaendee diaspora wao kwani ndiyo wanaosambaza muziki wao zaidi ya timu zao za promotion wanazozilipa kwa kazi hiyo, yaani hata kwenye clubs hao diaspora wanatoa pesa kwa DJs kupiga nyimbo za kwao, alisema ameshuhudia mtu akimpa DJ 15grand ili apige nyimbo za Kipopo hapo NY hivyo factors ni nyingi ambazo zinawapa advantages.
Beefing ipo sana tu, juzi tu hapa kulikuwa na kutokuelewana Davido na Burna Boy walipoachia nyimbo kwa siku moja. Kikubwa Wabongo wapambanie kuu-promote muziki nje ya mipaka(internationally) kwa wenye bajeti ndogo na wameshindwa kupata wawekezaji basi wajikongoje tu mdogomdogo kwani hata hao wenye bajeti kubwa wametokea huko wakakua kidogokidogo mpaka wakafika walipo.
Malengo, strategies na kuwa focused ndiyo vitu muhimu.