Wasanii wetu wangekuwa kama Michael Jackson ingekuwaje?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Usiku huu nimewaza tu kama wasanii wetu wangekuwa na Ukwasi na Umaarufu kama alio na aliokuwa nao Michael Jackson wangekuwaje na ingekuwaje?

Mtu ambaye wimbo wake mmoja kwenye You tube unaweza kuangaliwa na zaidi ya watu milioni 650 duniani . Hawa wetu wanaoishi maisha bandia lakini ndiyo hawashikiki kwa minato na tambo za mitandaoni!!
 
Alie muelewa anieleweshe [emoji3]
 
Yaani wewe si mzima unafananisha Music industry ya USA na TZ,unafananisha zama za analog amabapo mitandao haikuwepo na digital.
 
Mbona baadhi ya wasanii wetu wamepiga hatua kubwa tu za Sanaa zao acha kuwashusha hadhi hiv ulitegemea siku moja msanii wa tz mfano diamond kutangaza utalii wa south Africa,je ulitegemea siku moja diamond anafanya kazi na rickross?,je ulitegemea msanii wa Tanzania kufikisha viewer mil 50 mfano wimbo wa diamond Nana una viewer 50+,je umewahi kutegemea msanii wa tz kuwa balozi kwenye kinywaji Cha Rickross mf diamond,je umewahi kutegemea siku moja label ya tz itakujaje kuwa kubwa Africa mf.label ya wcb,je ulitegemea siku moja wasanii watz km diamond, Vanessa, rayvanny,mboso,harmo kupata mapokezi makubwa nje ya nchi kama vile wapo home,je umewahi kutegemea ngoma ya Vanessa kuchezwa kwenye uwanja wa NBA?je umewahi kutegemea siku moja wasanii wetu watasigniwa na label kubwa km vile universal na rockstar?je uliwahi kutegemea Papa wemba kumuomba collabo diamond? au sweezbeat kumuomba collabo diamond?.Mtoa mada acha dharau kwa wasanii wetu kila mtu ana njia zake za mafanikio usilazimishe awe Kama mtu unayemtaka wewe.
 
Hahaha sikupingi..Je ashawahi kuwaza Omario,NeYo,Rick Ross kutokea kwenye ngoma za mTz?ashawaza siku moja Rayvanny atamiliki tuzo ya BET mkononi?Je ashawaza Beyonce' atakuja kumpost binti mdogo mTz akiimba ngoma yake iliyokwenye albam yake ya Lion King?Ashawaza Jason Derulo kumshirikisha Rayvanny?Ashawaza Nandy kuchukua tuzo Afrima?Je ashawaza Idris Sultan kushiriki movie uko Hollyweed?Noo et weed ni Hollywood?
 
Safari ni hatua.Sehemu walipofikia sasa hivi ni sehemu ya safari kuelekea mafanikio makubwa zaidi.
 
Daaaah ahaaaaah wacha nicheke sasa kutazamwa Mara 650 million,nacho ni kitu cha ajabu wakati now kuna nyimbo zimetazamwa mara billion na uchafu alaaaaaaah.
 
Mitandao USA imeanza karne ya 18,may be wewe ni immature OK.

Wangapi walikuwa na access ya hiyo mitandao,kwa upande wetu wa Africa?

Alafu usipende kumzungumzia mtu kama unamjua eti "immature" nina knowledge kubwa sana kuhusu hiyo mitandao,internet na IT.Huwezi linganisha upashanaji wa habari kipindi cha 18 na sasa na hivi sasa ktk mfumo digital.

We ndiye level of maturity ipo low unataka kufananisha industry ya US na ya bongo we mzima kweli?.

Alafu sijui umezaliwa mwaka gani,kwa hiyo ww unamsupport huyo anayesema MJ hakuwa na minato,wakati alivyokuja bongo,alisema bongo inanuka (kasikilize wimbo wa Fid unaitwa professional ).
 
Ahaaaaah umedhihirisha uimmature wako,yaani huyo unamlinganisha kweli na wasanii wakubwa wakati hata level ya Bob Marley bado ajafikia.
 
Ahaaaaah umedhihirisha uimmature wako,yaani huyo unamlinganisha kweli na wasanii wakubwa wakati hata level ya Bob Marley bado ajafikia.
Kweli walimu mashuleni wana kazi,aliyesema akili ni nywele kila mtu anazake,sijajua alikuwa ana refer nywele zipi kuna wengine kama sio za kwapani basi zitakuwa za chini.Kumbe comparison ni topic ngumu sana kwa baadhi ya watu.
 
Kwa mujibu wa Guinness Book of Records Michael Jackson ndiye mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi tokea kuumbwa kwa Dunia.


Nadhani umechagua sample kubwa sana kwa wasanii wetu wa hapa Bongo, maana hata Us na kwingineko Michael Jackson anapambanishwa na vikundi kama The Beatles sio mtu mmoja mmoja , unawaonea wasanii wetu wa Bongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…