Washambuliaji wengi wa Tz hawana uwezo wa kuamua mechi

Mshambuliaji timamu lazima pia uwe unabakiza pumzi ya akiba kwa ajili ya kufanya shambulizi la kushtukiza, tumeona Okrah na Mzize walipata nafasi ya counter attack wako wawili na beki mmoja wa mwisho engo tofauti lakini wakashindwa kutumia nafasi hiyo kwa kuzidiwa kasi na mabeki ina maana hawana uwezo wa ziada kufanya maajabu kwenye maeneo hayo ya mwisho.

Mwaka 2010 baada ya mshambuliaji Fernando Torres wa Hispania kufunga bonge la bao dhidi ya Ujerumani dakika za lala ulaliwe alihojiwa aliwezaje kufanya maajabu yale dakika mbaya ambazo kikawaida wachezaji wengi wanakuwa washachoka akasema yeye huwa anabakiza pumzi ya tukio maalumu iwapo ikitokea mpira uliokufa aweze kufanya shambulizi la kikatili kwa kasi ya ajabu kuwashinda mabeki wa upinzani. Jamaa alimlamba chenga beki kisiki Philip Lahm kisha golikipa Manuel Neur akalambishwa nyasi nyavu zikatikisika Hispania ikatwaa kombe la Euro.

Washambuliaji wote wa Yanga na simba wana tatizo hilo la ubutu, hawana uwezo wa kuamua mechi ngumu wakibanwa wanakuwa wa kawaida kabisa

Kama unafatilia soka la dunia utakubaliana nami mfano Didier Drogba aliyokuwa anafanya chelsea hata ile fainali ya UEFA mwaka 2012 ingekuwa hawa kina Mzize au Kibu Denis chelsea isingetwaa UEFA ile mbele ya Bayern Munich

Straika lazima uwe na kitu cha ziada usiwe yori yori

Hiyo ndio sifa inayowapa mishahara minono kina Karim Benzema, Luis Suarez, Haaland, Victor Boniphace nk
Kwenye uchambuzi wako ungetuwekea na timu za Africa zenye washambuliaji wenye uwezo wa kumaliza mechi. Hakuna timu hiyo kuna uhaba wa Washambuliaji. Huko Ulaya penyewe pale Chelsea, Arsenal, Madrid wanaotamba ni viungo.
 
Sasa hivi hatuzalishi.wachezaji, tuliobahatika kumwona Zamoyoni akicheza pale angefunga goli nyingi
 
Mshambuliaji timamu lazima pia uwe unabakiza pumzi ya akiba kwa ajili ya kufanya shambulizi la kushtukiza, tumeona Okrah na Mzize walipata nafasi ya counter attack wako wawili na beki mmoja wa mwisho engo tofauti lakini wakashindwa kutumia nafasi hiyo kwa kuzidiwa kasi na mabeki ina maana hawana uwezo wa ziada kufanya maajabu kwenye maeneo hayo ya mwisho.

Mwaka 2010 baada ya mshambuliaji Fernando Torres wa Hispania kufunga bonge la bao dhidi ya Ujerumani dakika za lala ulaliwe alihojiwa aliwezaje kufanya maajabu yale dakika mbaya ambazo kikawaida wachezaji wengi wanakuwa washachoka akasema yeye huwa anabakiza pumzi ya tukio maalumu iwapo ikitokea mpira uliokufa aweze kufanya shambulizi la kikatili kwa kasi ya ajabu kuwashinda mabeki wa upinzani. Jamaa alimlamba chenga beki kisiki Philip Lahm kisha golikipa Manuel Neur akalambishwa nyasi nyavu zikatikisika Hispania ikatwaa kombe la Euro.

Washambuliaji wote wa Yanga na simba wana tatizo hilo la ubutu, hawana uwezo wa kuamua mechi ngumu wakibanwa wanakuwa wa kawaida kabisa

Kama unafatilia soka la dunia utakubaliana nami mfano Didier Drogba aliyokuwa anafanya chelsea hata ile fainali ya UEFA mwaka 2012 ingekuwa hawa kina Mzize au Kibu Denis chelsea isingetwaa UEFA ile mbele ya Bayern Munich

Straika lazima uwe na kitu cha ziada usiwe yori yori

Hiyo ndio sifa inayowapa mishahara minono kina Karim Benzema, Luis Suarez, Haaland, Victor Boniphace nk
Nikweli wanakimbia Kama mende
 
Kuna watu mnafikiri kufunga goli ni rahisi sana. Ukiangalia mpira ukichezwa, unaweza kushangaa inakuwaje mchezaji anakosa goli la wazi kiasi kile!! Ingia wewe sasa uone utakavyotoka ulimi. 🥵

Halafu kumlinganisha mchezaji mkubwa kama Fernando Torres na Clement Mzize, nadhani siyo sahihi. Maana hao wachezaji wawili wako dunia mbili tofauti.
Hapana mkuu,nafasi nyingine ni za wazi sana tusiwatetee wachezaji wazembe,hawatajifunza kamwe.

Zile nafasi za Saido na Kibu zilikuwa ni za wazi kabisa,utulivu ulikosekana
 
Back
Top Bottom