Washauri wa jukwaa hili mnakatisha tamaa wanaoanza biashara

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
70,916
Reaction score
141,437
Kwanza hongereni kwa michango yenu ya kujenga, huwezi kupita jukwaa hili usipate kitu kipya.

Ila pia kwa upande mwingine baadhi ya washauri, wachangiaji ni wakatishaji tamaa sana.
Mtu anaomba kujua biashara flani labda mtaji anasema ana million 1 majibu yake sasa, milioni si kitu, hiyo biashara huiwezi kwa hela hiyo andaa million kumi chaaa!!! Jamani hivi humu tuna assume kila mtu ana mtaji wa mamilioni?

Nlikua nacheki threads za biashara ya salon za kiume nmechoka na michango, kwamba kiti cha salon andaa million mbili, poda na mashine laki tano, mara kiti cha scrub laki tano yani unapewa hesabu za million kumi,hadi hapo tu nguvu zinaisha. Hakuna options kulingana na mtaji? mwenye mil 1 afanye cha mil 1, mwenye mil 10 afanye cha mil 10. Mfano mtu mwenye salon mitaa ya chuo au uswazi anategemea wateja wa hali ya kawaida tu hayo ya scrub sidhani kama ni ishu.

Kuna salon moja nlikua naenda yani hako kachumba mkiingia watano mmejaa, kana mashine moja, viti vya plastic viwili, vioo viwili na radio, kiti kimoja kunyoa kingine kutengeneza dreads kwa mwonekano utadhani stoo ila wateja sasa, gari zinazopaki hapo ni shida,mtu anakuja kuweka foleni then anaenda kazini atarudi, kila kichwa cha dread ni elf 10 kunyoa elf mbili jamaa wapo busy hadi usiku na hakuna cha mbwembwe za makochi wala nini wengine tunasubiri nje kwenye matofali.

Wadau mnaotaka kuanza biashara msikatishwe tamaa, jikune mkono unapofika, hicho kidogo ulichonacho anza nacho, mchina mwenyewe bidhaa zake zipo kulingana na hali ya kila mtu ukihitaji cha garama utapata na mwenye hela ndogo atapata hicho hicho ila chenye quality sawa na hela yake.

Msitukatishe tamaa wenye mitaji ya kuunga unga, ni hayo tu.
 
sure,, kuna jamaa alikuja hapa alisema anaomba ushauri ana laki moja na nusu,,, kuna mdau wa kwanza akamwambia etii akabetii,,, mwingine et hiyo labdaa kachezee 3 mzuka
😀😀😀
Eti tatu mzuka
Mwingine nae anasema biashara ya boda ni ya watu wavivu make unaingiza buku saba, wakati mi nalala hata jero sina
 
saluni ukishapata hela ya kodi ya chumba na kioo na mashine moja na visprit vichupa viwili na luku ya 20 kuna kingine jamani?
Teh ndo kuna kiti cha million mbili, kiti cha scrub, mwingine kaongeza na tv Samsung inch 32😀
 
Kwa kweli humu kuna kila aina ya watu ambao wengine huwa wanachangia mradi wachangie tu.
Lakini nawe pia unaangalia nani kachangia mchango wenye mvuto kwa mtaji wako
 
Kuna thread za Ujenzi hzo utasema humu ndan kila mtu amejenga utasikia hyo milion 20 utajenga banda la kuku nyumba labda uwe na milion 100 kwel jaman????
Wameanza kasumba ya kuongeza sifuri mwisho.
 
Kuna thread za Ujenzi hzo utasema humu ndan kila mtu amejenga utasikia hyo milion 20 utajenga banda la kuku nyumba labda uwe na milion 100 kwel jaman????
kwakweli ni kukatisha tamaa huku
 
Ulichosema ni kweli kabisa baadhi ya michango inakatisha tamaa sana.Kama unaomba msaada inakubidi uchambue inayokufaa na isiyokufaa unaicha.Lakini kitu cha muhimu ni wewe mwenyewe kutambua unataka saloon ya aina gani hii inategemea na wateja uliowakusudia.Baada ya hapo fanya utafiti kwa kutembelea saloon mbalimbali kwa kuuliza na kwenda katika maduka ya vifaa vya saloo.
Mi nimefunguwa saloon ya kiume ina miaka 2 now.Kabla ya kuanza mchakato wa ujenzi wa saloon nilihakikisha napata taarifa sahihi kwa watu sahihi na kwa muda sahihi.Always remember that;The right thought +the right people in the right environment at the right time and right purpose=the right result. Nilitumia kanuni kama mwongozo.Ukienda kwenye maduka ya vifaa vya saloon utachanganyika na kamtaji kako ka mawazo kuna viti hadi 1.5m single, kuna viti vya scrub hadi 1m+ kuna mashine hadi 200k na vifaa vingine vya gharama kubwa Sana. Lakini jambo la msingi unataka saloon ya aina gani due to you're capita.

Kwa upande wangu nilianza mdogo mdogo kwa viti viwili vya laki3@kimoja mahali pa kuoshea kiti chake ilicost kitu kama 6.5laki.Baada ya kuanza kuingia pesa kutoka saloon nikaagiza baadhi ya vifaa kutoka Zanzibar. Zanzibar vitu bei cheee sana kuliko huku bara.Nitaweka picha badae uone nilipoanza na nilipo.
Asante
 
Tatizo naona lipo kwa muulizaji suali, mfano unasema nina laki na nusu nataka kuanzisha biashara ya saloon au kuuza fruit. Lakini unasema nina laki na nusu hujui uanze kufanya nini hapa lazima watatokea watu zero brain kukuvunja moyo. Huwezi kwenda benki na kusema nataka mkopo bila ya kutoa sababu za kuomba mkopo. Pia hapa jf kuna watu hujifanya kama wana hela wakati mfuko umetoboka tokea kamaliza shule. Nakumbuka kuna siku baba alitaka kumpa mdogo wake mama hela ya biashara kama millioni 10 bure sio mkopo. Basi akamuuliza utafanya biashara gani? Jibu lake alisema apewe hela ya mahari kwanza aowe halafu ndio aje apewe tena hio millioni 10 ya biashara. Mzee palepale alimwambia sahau msaada kutoka kwangu.
 
Hao nao wapo wana mtaji hawajui wafanye nini, na wapo wenye mawazo ya biashara tele mtaji hamna, anaeuliza afanye nini hata simshangai
 
Humu JF ukileta ishu yako ushauriwe aisee unaweza kutana na utumbo mtupu mpaka kuna wakati niliwaza, membership iwe na vipimo vya sifa Fulani ili si kila MTU awe ni great thinker... Wengine hawana sifa hizo...kuna haja ya kuanzisha forum nyingine...au akina maxlian wareview utaratibu na kanuni.
 
Kwanza hongereni kwa michango yenu ya kujenga, huwezi kupita jukwaa hili usipate kitu kipya.

Ila pia kwa upande mwingine baadhi ya washauri, wachangiaji ni wakatishaji tamaa sana.
Mtu anaomba kujua biashara flani labda mtaji anasema ana million 1 majibu yake sasa, milioni si kitu, hiyo biashara huiwezi kwa hela hiyo andaa million kumi chaaa!!! Jamani hivi humu tuna assume kila mtu ana mtaji wa mamilioni?

Nlikua nacheki threads za biashara ya salon za kiume nmechoka na michango, kwamba kiti cha salon andaa million mbili, poda na mashine laki tano, mara kiti cha scrub laki tano yani unapewa hesabu za million kumi,hadi hapo tu nguvu zinaisha. Hakuna options kulingana na mtaji? mwenye mil 1 afanye cha mil 1, mwenye mil 10 afanye cha mil 10. Mfano mtu mwenye salon mitaa ya chuo au uswazi anategemea wateja wa hali ya kawaida tu hayo ya scrub sidhani kama ni ishu.

Kuna salon moja nlikua naenda yani hako kachumba mkiingia watano mmejaa, kana mashine moja, viti vya plastic viwili, vioo viwili na radio, kiti kimoja kunyoa kingine kutengeneza dreads kwa mwonekano utadhani stoo ila wateja sasa, gari zinazopaki hapo ni shida,mtu anakuja kuweka foleni then anaenda kazini atarudi, kila kichwa cha dread ni elf 10 kunyoa elf mbili jamaa wapo busy hadi usiku na hakuna cha mbwembwe za makochi wala nini wengine tunasubiri nje kwenye matofali.

Wadau mnaotaka kuanza biashara msikatishwe tamaa, jikune mkono unapofika, hicho kidogo ulichonacho anza nacho, mchina mwenyewe bidhaa zake zipo kulingana na hali ya kila mtu ukihitaji cha garama utapata na mwenye hela ndogo atapata hicho hicho ila chenye quality sawa na hela yake.

Msitukatishe tamaa wenye mitaji ya kuunga unga, ni hayo tu.
Shida ni.kwamba humu wanaingia walio potea njia.

Wengi.wanao toa hayo majibu unakuta ni waajiriwa na.hawajawahi hata kumiliki.kibanda cha kuchajisha simu
 
Back
Top Bottom