Washauri wa jukwaa hili mnakatisha tamaa wanaoanza biashara

Washauri wa jukwaa hili mnakatisha tamaa wanaoanza biashara

Kuna thread za Ujenzi hzo utasema humu ndan kila mtu amejenga utasikia hyo milion 20 utajenga banda la kuku nyumba labda uwe na milion 100 kwel jaman????
Yaani JF bhana watu wengi wanapenda kuonekana high class kumbe ni watu wa kawaida tu,mtu akishamiliki vits tu anaanza kuona watembea kwa miguu si lolote si chochote. Mtu akiwa ña ka degree tu form 4 leaver hawapumui! Kwanza wote wanaokatisha tamaa wenzao humu ni malimbukeni tu , kwani ukimpa mtu wazo la kumjenga utapungukiwa nini? Badilikeni bhana nyie mnaokatisha tamaa wenzenu kama huna cha kumshauri Pita tu usicomment chochote! Kumbukeni humu tuko watu tofauti wenye uwezo mkubwa kifedha wamo, wasomi sana wamo, standard 7 wamo na walala hoi pia tumo! So mshauri mtu kulingana na kile anachohitaji kwa maelezo yake usimkashifu na kumkatisha tamaa kwa hali yake!
 
Nawaitaga wapumbavu...na sio tu kwenye issue ya business hata mtu anakuja kuomba mkopo na unakuta amejieleza vizuri
Lakini mtu anakuja na comment unaanza kujiuliza anayendika ana matatizo ya akili ama vipi
 
Yaani mkuu we acha,nimeanzisha thread ya kuomba mkopo na nimejielezea fresh,sasa kuna mtu akachangia kuwa anaweza kunipa huo mkopo bila hata riba,nikamfwata PM akaniambia nimtafute Mo dewdi,aisee huyu mtu amenikatisha sana tamaa..sasa unakaa unawaza hivi kulikuwa na ulazima gani wa yeye kuchangia kwenye thread ya mtu mwenye shida na hawezi kumpa hata maelekezo nini cha kufanya..
 
Wala usikatishwe tamaa na hao wajinga ndugu yangu..pambana tu
 
Kwanza hongereni kwa michango yenu ya kujenga, huwezi kupita jukwaa hili usipate kitu kipya.

Ila pia kwa upande mwingine baadhi ya washauri, wachangiaji ni wakatishaji tamaa sana.
Mtu anaomba kujua biashara flani labda mtaji anasema ana million 1 majibu yake sasa, milioni si kitu, hiyo biashara huiwezi kwa hela hiyo andaa million kumi chaaa!!! Jamani hivi humu tuna assume kila mtu ana mtaji wa mamilioni?

Nlikua nacheki threads za biashara ya salon za kiume nmechoka na michango, kwamba kiti cha salon andaa million mbili, poda na mashine laki tano, mara kiti cha scrub laki tano yani unapewa hesabu za million kumi,hadi hapo tu nguvu zinaisha. Hakuna options kulingana na mtaji? mwenye mil 1 afanye cha mil 1, mwenye mil 10 afanye cha mil 10. Mfano mtu mwenye salon mitaa ya chuo au uswazi anategemea wateja wa hali ya kawaida tu hayo ya scrub sidhani kama ni ishu.

Kuna salon moja nlikua naenda yani hako kachumba mkiingia watano mmejaa, kana mashine moja, viti vya plastic viwili, vioo viwili na radio, kiti kimoja kunyoa kingine kutengeneza dreads kwa mwonekano utadhani stoo ila wateja sasa, gari zinazopaki hapo ni shida,mtu anakuja kuweka foleni then anaenda kazini atarudi, kila kichwa cha dread ni elf 10 kunyoa elf mbili jamaa wapo busy hadi usiku na hakuna cha mbwembwe za makochi wala nini wengine tunasubiri nje kwenye matofali.

Wadau mnaotaka kuanza biashara msikatishwe tamaa, jikune mkono unapofika, hicho kidogo ulichonacho anza nacho, mchina mwenyewe bidhaa zake zipo kulingana na hali ya kila mtu ukihitaji cha garama utapata na mwenye hela ndogo atapata hicho hicho ila chenye quality sawa na hela yake.

Msitukatishe tamaa wenye mitaji ya kuunga unga, ni hayo tu.
Evelyn Salt
Nakutafuta ujue...nina Mzigo wako
 
Nenda kwenye Uzi wa ujenzi sasa
Utaskia nyumba ya chumba 3 na sebule bila ml70 haijawa nyumba sasa sis huku vijijn mnatuisha sana aisee
 
Nenda kwenye Uzi wa ujenzi sasa
Utaskia nyumba ya chumba 3 na sebule bila ml70 haijawa nyumba sasa sis huku vijijn mnatuisha sana aisee
Japo wanasema za kuambiwa changanya na zako ila hii inakatisha tamaa
 
biashara ni kujitoa kweli kweli humu wapo malimbukeni wengi, graduates wasio na kazi ila wana mihemko ya kuanzisha biashara ni wasomi wachache sana walioingia kwenye biashara na kufika mbali wengi wao darasa la 7 na form 4 tubadilike....
 
Yaani mkuu we acha,nimeanzisha thread ya kuomba mkopo na nimejielezea fresh,sasa kuna mtu akachangia kuwa anaweza kunipa huo mkopo bila hata riba,nikamfwata PM akaniambia nimtafute Mo dewdi,aisee huyu mtu amenikatisha sana tamaa..sasa unakaa unawaza hivi kulikuwa na ulazima gani wa yeye kuchangia kwenye thread ya mtu mwenye shida na hawezi kumpa hata maelekezo nini cha kufanya..
hahahahhahaaaaaa,mkuu umeongea kwa hisia sana pole aise...ila nawaza tu jinsi ulivyoenda PM kwa matumaini kibao,mwisho wa siku ushauri ulioambulia ni Umfuate More Dewji...duh,kuna watu wana roho ngumu na utani na maisha ya watu!
 
Back
Top Bottom