Washauri wa jukwaa hili mnakatisha tamaa wanaoanza biashara

Shida ni.kwamba humu wanaingia walio potea njia.

Wengi.wanao toa hayo majibu unakuta ni waajiriwa na.hawajawahi hata kumiliki.kibanda cha kuchajisha simu
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kuna thread za Ujenzi hzo utasema humu ndan kila mtu amejenga utasikia hyo milion 20 utajenga banda la kuku nyumba labda uwe na milion 100 kwel jaman????
Yaani JF bhana watu wengi wanapenda kuonekana high class kumbe ni watu wa kawaida tu,mtu akishamiliki vits tu anaanza kuona watembea kwa miguu si lolote si chochote. Mtu akiwa Γ±a ka degree tu form 4 leaver hawapumui! Kwanza wote wanaokatisha tamaa wenzao humu ni malimbukeni tu , kwani ukimpa mtu wazo la kumjenga utapungukiwa nini? Badilikeni bhana nyie mnaokatisha tamaa wenzenu kama huna cha kumshauri Pita tu usicomment chochote! Kumbukeni humu tuko watu tofauti wenye uwezo mkubwa kifedha wamo, wasomi sana wamo, standard 7 wamo na walala hoi pia tumo! So mshauri mtu kulingana na kile anachohitaji kwa maelezo yake usimkashifu na kumkatisha tamaa kwa hali yake!
 
Nawaitaga wapumbavu...na sio tu kwenye issue ya business hata mtu anakuja kuomba mkopo na unakuta amejieleza vizuri
Lakini mtu anakuja na comment unaanza kujiuliza anayendika ana matatizo ya akili ama vipi
 
Nawaitaga wapumbavu...na sio tu kwenye issue ya business hata mtu anakuja kuomba mkopo na unakuta amejieleza vizuri
Lakini mtu anakuja na comment unaanza kujiuliza anayendika ana matatizo ya akili ama vipi
Yaani mkuu we acha,nimeanzisha thread ya kuomba mkopo na nimejielezea fresh,sasa kuna mtu akachangia kuwa anaweza kunipa huo mkopo bila hata riba,nikamfwata PM akaniambia nimtafute Mo dewdi,aisee huyu mtu amenikatisha sana tamaa..sasa unakaa unawaza hivi kulikuwa na ulazima gani wa yeye kuchangia kwenye thread ya mtu mwenye shida na hawezi kumpa hata maelekezo nini cha kufanya..
 
Wala usikatishwe tamaa na hao wajinga ndugu yangu..pambana tu
 
Evelyn Salt
Nakutafuta ujue...nina Mzigo wako
 
Nenda kwenye Uzi wa ujenzi sasa
Utaskia nyumba ya chumba 3 na sebule bila ml70 haijawa nyumba sasa sis huku vijijn mnatuisha sana aisee
 
Nenda kwenye Uzi wa ujenzi sasa
Utaskia nyumba ya chumba 3 na sebule bila ml70 haijawa nyumba sasa sis huku vijijn mnatuisha sana aisee
Japo wanasema za kuambiwa changanya na zako ila hii inakatisha tamaa
 
biashara ni kujitoa kweli kweli humu wapo malimbukeni wengi, graduates wasio na kazi ila wana mihemko ya kuanzisha biashara ni wasomi wachache sana walioingia kwenye biashara na kufika mbali wengi wao darasa la 7 na form 4 tubadilike....
 
hahahahhahaaaaaa,mkuu umeongea kwa hisia sana pole aise...ila nawaza tu jinsi ulivyoenda PM kwa matumaini kibao,mwisho wa siku ushauri ulioambulia ni Umfuate More Dewji...duh,kuna watu wana roho ngumu na utani na maisha ya watu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…