Mimi ni mwanafunzi wa , mwaka wa 3 St. Augustine Mwanza, darasa letu tumefanya kitu kibaya sana yaani najuta kwa kushiriki, tumemfukuzisha kazi mhadhiri anayeitwa Nicas, kwa what i call hate, tuliunda tume ya kizushi kwenda kwa kDr. Charles Kitima kumwambia kwamba huyu mhadhiri hatumuelewi na anatutukana darasani kumbe kisa ni kwamba anafundisha somo fulani ambalo linaendana na hesabu halafu darasa zima tunaliogopa hilo somo ingawa ticha alikuwa anajitahidi kwa namna yake kutuelewesha. sasa ticha huyo amefukuzwa kazi na chuo. hapa chuoni kwetu sisi tunasikilizwa saana yaani tukimwambia tu mkuu wa chuo hatumtaki lecturer fulani basi ndani ya dkk kadhaa anafukuzwa kazi. tofauti na vyuo vingine mpaka sasa tumeshawafukuzisha lectureres 6 kazi, hivyo basi nawaomba wanajamii wenzangu mjaribu kuwashauri wanafunzi wenzetu tunachofanya si kizuri kwa sababu haya nia maisha na hii si namna nzuri ya kujifunza kwani walimu wa hapa SAUT wanajitahidi sana kufundisha na kuwa panctual tatizo ni sisi wanafunzi sometimes tunakuwa hatupo poaaaa.