Washikaji tusome tuache kudeka, huyu muhadhiri tumemuonea

Washikaji tusome tuache kudeka, huyu muhadhiri tumemuonea

Nimeskitishwa sana kama kweli basi nyie ni vilaza wa mwisho,NICAS ni jembe tulio maliza BBA 2011 tunalijua hilo. Pili he was my supervisor on my research. Madogo pigine shule sio kuchukia walimi wenu bila sababu. Uongoz wa SAUT huwa unawasikilizasana wanafunzi so dont take it as loop
 
Mimi ni mwanafunzi wa , mwaka wa 3 St. Augustine Mwanza, darasa letu tumefanya kitu kibaya sana yaani najuta kwa kushiriki, tumemfukuzisha kazi mhadhiri anayeitwa Nicas, kwa what i call hate, tuliunda tume ya kizushi kwenda kwa kDr. Charles Kitima kumwambia kwamba huyu mhadhiri hatumuelewi na anatutukana darasani kumbe kisa ni kwamba anafundisha somo fulani ambalo linaendana na hesabu halafu darasa zima tunaliogopa hilo somo ingawa ticha alikuwa anajitahidi kwa namna yake kutuelewesha. sasa ticha huyo amefukuzwa kazi na chuo. hapa chuoni kwetu sisi tunasikilizwa saana yaani tukimwambia tu mkuu wa chuo hatumtaki lecturer fulani basi ndani ya dkk kadhaa anafukuzwa kazi. tofauti na vyuo vingine mpaka sasa tumeshawafukuzisha lectureres 6 kazi, hivyo basi nawaomba wanajamii wenzangu mjaribu kuwashauri wanafunzi wenzetu tunachofanya si kizuri kwa sababu haya nia maisha na hii si namna nzuri ya kujifunza kwani walimu wa hapa SAUT wanajitahidi sana kufundisha na kuwa panctual tatizo ni sisi wanafunzi sometimes tunakuwa hatupo poaaaa.

imeniuma sana, kwa sababu hamjajua kwamba maisha ni magumu, kupata kazi ni ngumu, kwa style hii daah! mnawafukuzisha kazi walimu wenu kwa nn? chukulieni angekuwa kaka yenu mngefanyaje? ajira hakuna mnawaachisha wenye ajira, haya karibuni mtaani...Mizinga haikubaliki hapa bongo
 
Huo ndo ufedhuri ambao unalirudisha hata taifa letu nyuma. Tatizo lililopo ni wanavyuo wengi kupenda kufauru bila kusoma na wengi wao ni wale wanaokariri na kwenda kutapika kwenye paper. Akipigwa technical question tu basi chini halali kwake.

Kumfanyia fitina Mhadhiri ni uchuro..... KUENI muwe binadamu hapo baadaye....
 
Nadhani hukunielewa nililomaanisha mkuu, naomba nitumie mda kidogo kukuelewesha kama utachagua kuelewa nililokua namaanisha.

Hii quote hapa chini ndo iliyonivuta kutoa jibu hilo


Nilitoa jibu hili hapa chini.



Kila siku watu wanapoona ufaulu umeshuka ama matokea ya mtu yamekua mabaya, watu wamekimbilia kuilaumu NECTA kwa utunzi wa mitihani migumu ama Katibu wa baraza la hilo kwa kusimamia utunzi wa mitihani 'migumu', bila kujishughulisha na chanzo cha tatizo kilipo. Kilichotokea miezi michache iliyopita sote ni mashahidi.



So niliweka hiyo quote kama kibwagizo tu kureflect mawazo mafupi mengi yanayolizunguka taifa hili, kuanzia ule upumbavu wa ku'standardize tena kwa kulitangazia taifa bila aibu (nadhani ndiyo maana nimeita ni upumbavu) hadi ule ujinga wa kushusha grades ili madaraja yapande katika matokeo na wazazi wafurahi.

Nadhani umenielewa.
Mkuu samahani unajua awali sikuelewa ujumbe wako, kumbe ulikuwa unapeleka ujumbe kwa wale wanaolaumu NECTA bila kufahamu undani wa matatizo.

Naomba nipokee taarifa na ninaipokea kama ilivyo. Tuko pamoja mkuu Bob Lee Swagger
 
Wewe utakua LAW au PR.. Mnafanya chuo chenu,..!! Mbona faculty zingine hamna mambo ya hivi?
 
ngoja mje mtaani ndo mtajua upuuz mliokuwa mnaufanya.. hakuna Kitima huku, kama ni mburula ndo ivo tena., jitaidini vjana huku mtaani hakuna wa kumchongea, labda kama mnasomea BED COMMERCE. ndio haina tatzo.. ila mchelea mwana kulia hulia yeye(mpe DR.kitima hu ujumbe)
 
Back
Top Bottom