Washiriki shindano la Watanzania wenye umri mdogo na wenye ushawishi watajwa

Haf jokate na wema ni waigizaji wa aina gani? Hope sio bongo movie!!! Wangefafanua zaidi
 
Haf jokate na wema ni waigizaji wa aina gani? Hope sio bongo movie!!! Wangefafanua zaidi
Bora wema. Ila Jokate sijui anaingiaje, labda angepewa kipengele cha udananda na kujipendekeza CCM ili apate Ubunge.
 
Haya ni matatizo ya kujifungia vyumbani na kuja na majina yenu, hivi Hashim Thabit na Juma Kaseja,Ngassa wameingiaje humo? Si bora mgetuwekea hata jina la Saimon Msuva. Mtu kama Mama Alaska unamuachaje kwenye Business category?
 
Hiyo list ya hovyo
 
Mnashindwa kumuweka Ontario mnawaweka wapuuzi ambao hawana direct implication kwenye jamii!!!

Hivi huyo Jokate ana movie ipi na ipi??!

Juma kaseja ana influence gani???? Msuva anavyotupia magoli huko Morocco ina maana hamjamuona???! Amekuwa na misimu mizuri yangu yupo yanga.

Huyo wema nae ni walewale.

In Short ni Tuzo nzuri ila kuna baadhi ya vipengele wamezingua
 
Eti Salim Kikeke naye ni kijana! Mbona sijamuona 'kijana' Le Mutuz? Wapi Makonda? Pia huyo Ian Ferrao ni Mtanzania? Kachukua uraia lini?

umri mdogo kwa mtanzania ni upi? kama lifespan yetu ni miaka 55 kaseja anaingiaje ?
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Eti?
 
Mbona Magu hayumo? waache utani.
 
Bila Le Mutuz basi shindano ni fake. Au wanamaanisha umri mdogo kivipi?
 
Business- Patrick Ngowi,

Entertainment- Jokate Mwegelo,

Law&governance- Bonnah Kaluwa,

Lifestyle- Jacqueline Mengi,

Media- Millard Ayo,

Science&Technology- Lilian Makoi,

Sports- Mbwana Samatta,

Social Ent.&Civil Society- Faraja Nyalandu.
Huyu Bonna Kaluwa Mbunge wa Segerea, ana influence gani kwenye siasa za nchii hii?
 
Unaijua kampeni ya Jokate inavyoinfluence wasichana mashuleni na vyuoni
Unajua product zake zimetoa ajira kwa watu wangapi?
 
Eti Salim Kikeke naye ni kijana! Mbona sijamuona 'kijana' Le Mutuz? Wapi Makonda? Pia huyo Ian Ferrao ni Mtanzania? Kachukua uraia lini?

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Eti?

Eti Kikeke mwaka jana alisema ana miaka 30!! Jamaa huwa hapendi kuonekana mtu mzima ila ndio hivyo tena sura na upara vinamuumbua!! Anapenda ujana sana yule mzee!!.. kwenye kipindi cha mkasi aliulizwa nini ushauri wake kwa vijana akakomaa eti "namimi pia ni kijana"
 
Mchango wa Jokate kwa vijana ni mkubwa sana kuliko hata huyo uliyemtaja sema wamekosea kumuweka katika kitengo cha muigizaji, Jokate anajitolea sana kwa hawa vijana wa sekondari mfatilie upate kumuelewa achana na media zinavyomuandika sijui mara leo kapiga picha hii mara kesho katoka na yule wanasahau kazi kubwa anayoifanya kwa vijana wetu.

She Deserve it.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…