kulikoni,
ZNZ walijaribu kujiunga na FIFA kwa misingi hiyo hiyo ya uanachama wa CECAFA, lakini wakakataliwa kwasababu hawatambuliki kama nchi. FIFA inaitambua Tanzania. kwa msingi huo huo, ZNZ haiwezi kujiunga na vyombo vingine vya kimataifa kama UN, OAU, EA,SADC,COMESA, etc.
Mapendekezo yangu ni kwamba Tanzania ijiunge na OIC. kama kuna misaada au miradi yoyote tutakayopata kutokana na uanachama wetu, basi ielekezwe kule ambako inahitajika.
Bara nzima yenye wananchi 34,000,000 hatuwezi kuvutwa kama gari bovu na wananchi 950,000 wa Visiwani, kwenda kuingia hiyo kitu mbovu,
Referrendum? Ya nini kwani ulipoanzishwa ilifanywa? Sasa Why Now? Unless kama kwenye hii forum kuna wanaoelewa sababu za kimsingi za kuendeleza huu Muungano, faida yake so far toka uwepo maana wote tunajua hasara zake tayari,
Jamani wazee wanaofahamu faida zake waziweke hapa zijadiliwe, maana hasara zake tayari tunazifahamu?
Ndugu yangu Mkandara,
Unajua kinachonisikitisha juu ya maoni ya watu kama dakta Who ni kwamba kama huu mwungano ungetengenezwa na Waingereza, mathalan, leo kusingekuwa na malalamiko. Lakini kwa kuwa Wabantu wawili, Nyerere na Karume, walidiriki kufanya ambayo Wabantu hawakutarajiwa kufanya, kuna kuhoji, kukebehi, kulalamika, ad infinitum, juu ya huu mwungano. Unajua nini? Marekani walivamia Hawaii. Wakamwua mfalme wao, wakawaingiza kwa nguvu katika mwungano. Texas na Mexico zilichukuliwa kwa mtutu wa bunduki. Do I need to say more?