Wasi Wasi wa Udini

Wasi Wasi wa Udini

Status
Not open for further replies.
Kama JK ni MDINI Basi Na viongozi wengine ni wadini.....
Nahisi hata alie tuma hii thread ni Mdini!!

Lazima itaonekana Dini wakati wote...
Kwani siasa ni bora zaidi kuliko Dini?

Tuseme ukweli!! Mimi sikumoja Nilikua nina pita-pita mitaani...
nilipofika kwenye hoteli fulani -nikaona Tv- Kama vile Jk anzungumzia kuhusu Madrasa yake!! Ni kaendelea na safari sikuzingatia sana!!! Lakini niliondoka na mawazo...Inakuaje Raisi anafanya hivi?

Mara nikaingia kwenye Mgahawa mwingine-Nikakuta kipindi hichio hicho kwenye TV-Nilipozingatia!!! nikagundua !!!!Yule Alikua sio JK...Ni walimu wa madrasa
Tena Mwalimu huyo alikua ana toa hadi Namba yake ya simu!!!

-Contunue-
 
Tarehe 12/9/2006

MWANANCHI HABARI


'Vigogo' Chadema wamwaga misaada KKKT

Na Ally Sonda

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho, Grace Kiwelu wametoa msaada wa Sh 4,200,000 ili kusaidia miradi ya ujenzi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Majengo mjini hapa.

Mbowe, kwa upande wake alichangia Sh 2.5 milioni na Mbunge Kiwelu akatoa Sh 1 milioni kwa ajili ya maendeleo ya miradi kanisani humo.

Aidha, mwanasiasa huyo (Kiwelu) alitoa msaada wa Sh500,000 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa choo cha shule ya awali ya kanisa hilo.

Akizungumza mjini hapa baada ya kukabidhi sehemu iliyobaki ya misaada hiyo, Kiwelu alisema kuwa, ili kuhakikisha kuwa waumini wanakuwa na maendeleo kiuchumi, amejitolea Sh 200,000 ili kutunisha mfuko wa Ushirika wa Akiba na Mikopo (Saccos) unaojulikana kwa jina la UWAMKI ulioanzishwa na waumini wa kanisa hilo.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, fedha hizo zitatumika kununua baadhi ya samani muhimu za ofisi ya ushirika huo ambao unatarajiwa kuwa mkombozi kwa waumini wa kanisa hilo na wa kata za jirani.

Kwa upande wake, Mbowe alisisitiza kuwa viongozi wa chama hicho, wataendelea kuwasaidia waumini wa madhehebu ya dini nchini ili kujenga taifa la watu waliobobea kwenye imani ya kumjua Mungu kwa kufuata maagizo yake.
 
Kikwete ateua majaji 20



na Irene Mark


RAIS Jakaya Kikwete, ameanza kupangua kero ndani ya mahakama kwa kuteua majaji wapya 20 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.


Taarifa ya uteuzi huo ilitolewa na Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama ya Rufani, Sophia Wambura, jana.


Miongoni mwa walioteuliwa ni mawakili wa kujitegemea, na wanawake sita.


Majaji walioteuliwa ni Augustine Mwarija, ambaye alikuwa Msajili Mahakama ya Rufani Tanzania; na Alice Chingwile, aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Mambo ya Katiba na Sheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu.


Aliyekuwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali, Godfrey Shaidi, naye ameteuliwa kuwa jaji. Atakayeziba nafasi yake hajatangazwa.


Majaji wengine wapya ni Robert Makaramba, aliyekuwa Kamishna Tume ya Haki za Binadamu; Gadi Mjemmas, aliyekuwa Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu; Imani Aboud, aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi, Utawala, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; na Agathon Nchimbi, aliyekuwa Mkurugenzi Mahakama za Mwanzo, Mahakama ya Rufani.


Wengine ni Shabani Lilla, aliyekuwa Msajili wa Wilaya, Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha; Stella Mugasha, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Tume ya Uchaguzi; na Zaiduni Chocha, aliyekuwa Kaimu Naibu Msajili, Mahakama ya Rufani.


Majaji wengine wateule ni Aisha Nyerere, aliyekuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro; Amiri Mruma, aliyekuwa Msajili Baraza la Ushindani; Sekieti Kihiyo, aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar; Aishieli Sumari, aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Mashitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu; na Kakusulo Sambo, aliyekuwa Naibu Mwenyekiti Mahakama ya Kazi.


Wengine ni Mwanaisha Kwariko, aliyekuwa Msajili wa Wilaya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa; Aloyse Mujulizi, aliyekuwa Wakili wa Kujitegemea, na mwandishi wa makala katika safu maalumu ya kila Jumamosi katika gazeti hili la Tanzania Daima.


Wengine ni Augustino Shayo, aliyekuwa Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania; Frederick Werema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Katiba na Haki za Binadamu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu; na Lawrence Uzia, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mahakama za Wilaya hadi Rufani.


Uteuzi wa majaji hao wapya wa Mahakama Kuu unaanza mara moja na taarifa kuhusu tarehe ya kuapishwa kwao, itatolewa baadaye. Wataapishwa na Rais Kikwete.


Miezi kadhaa iliyopita, Tanzania Daima iliandika habari za kuwapo uteuzi wa majaji 20; taarifa ambazo zilithibitishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Mary Nagu.


Kwa miaka mingi, kumekuwapo na upungufu mkubwa wa majaji, na hivyo kusababisha kuchelewesha kesi nyingi.


Ucheleweshaji kesi ni miongoni mwa kero ambazo Rais Kikwete, kabla na baada ya kuingia madarakani, aliahidi kuzipatia ufumbuzi.


Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, uteuzi wa majaji 20 ni mwanzo tu wa uteuzi wa majaji wengine wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.
 
Habari Mpya » Rais Kikwete ateua Makatibu Wakuu

Rais Kikwete ateua Makatibu Wakuu
By Mike Mushi | Published 01/21/2006 | Habari Mpya |

Luhanjo katibu mkuu kiongozi mpya
RAIS Jakaya Kikwete, ameteua makatibu wakuu 28, wakiwemo wanane wapya ambapo Philemon Luhanjo, anayekuwa Katibu Mkuu Kiongozi mpya

Luhanjo anachukua nafasi ya Marten Lumbanga, ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo, Luhanjo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Uteuzi huo wa makatibu wakuu ulitangazwa jana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Kassim Mpenda, kwa niaba ya rais.

Katika uteuzi huo Rais Kikwete pia ameteua naibu makatibu wakuu 14, wakiwemo wanawake wawili. Pia, kati ya makatibu wakuu wapya wamo wanawake wawili.

Makatibu wakuu wapya na wizara zao kwenye mabano ni Maimuna Tarishi (Waziri Mkuu-TAMISEMI), Omar Bendera (Ushirikiano wa Afrika Mashariki), Arthur Mwakapugi (Nishati na Madini) na Saleh Pamba (Maliasili na Utalii).

Wengine ni Profesa Khamis Dihenga (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Kijakazi Mtengwa (Habari, Utamaduni na Michezo), Vincent Lyimo (Katiba na Sheria), ambaye pia anakuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Dk. Charles Nyamurunda (Maendeleo ya Mifugo).

Naibu Makatibu Wakuu wapya ni Sazi Salula (Makamu wa Rais), Michael Mwanda (Ofisi ya Waziri Mkuu), Wilson Mukama (Waziri Mkuu-TAMISEMI), Balozi Patrick Mombo (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) na Joyce Mapunjo (Fedha).

Wengine ni Godfrey Mkocha (Viwanda, Biashara na Masoko), Mohamed Muya (Kilimo, Chakula na Ushirika), Omar Chambo (Miundombinu), Edris Mavura (Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana), Dk. Jonas Melewasi (Maendeleo ya Mifugo), Dk. Stergomena Taxi-Bamwenda (Mipango, Uchumi na Uwezeshaji) na Oliver Mhaiki (Elimu na Mafunzo ya Ufundi).

Makatibu Wakuu wa zamani walioteuliwa tena na ambao wamebadilishwa wizara ni Rose Lugembe (Ikulu), Ruth Mollel (Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Abubakar Rajab (Makamu wa Rais), Vincent Mrisho (Waziri Mkuu), Peniel Lyimo (Kilimo, Chakula na Ushirika).

Wengine ni Patrick Rutabanzibwa (Maji), Injinia John Kijazi (Miundombinu), Dk. Ladislaus Komba (Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana), Abel Mwaisumo (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Bakari Mahiza (Usalama wa Raia), Salmon Odunga (Mambo ya Ndani ya Nchi ), Dk. Naomi Katunzi (Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu), na Mariam Mwaffisi (Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto).

Makatibu wakuu waliobaki katika wizara zao za zamani ni Gray Mgonja (Fedha), Dk. Enos Bukuku (Mipango, Uchumi na Uwezeshaji), Wilfred Nyachia (Viwanda, Biashara na Masoko), Salome Sijaona (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi).
Naibu makatibu wakuu wa zamani walioteuliwa tena na wizara zao katika mabano ni George Yambesi (Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma) na Ramadhan Khijjah (Fedha).

Kabla ya uteuzi huo, Mkocha alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara, Profesa Dihenga (Mrajis Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro), Salula (Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria za Kimataifa na Madai) na Mukama (Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam).

Wengine ni Mwakapugi (Mkurugenzi wa Uchumi Mkuu, Mipango na Ubinafsishaji), Dk. Stergomena (Ofisa Mtendaji Mkuu-BEST), Mapunjo (Kamisha wa Fedha za Nje-Hazina), Pamba (Mkurugenzi wa Utalii), Mhaiki (Mkurugenzi Elimu ya Msingi).
Mpenda alisema Wilfred Ngirwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Chakula na Mary Mushi, aliyekuwa Ofisi ya Makamu wa Rais watapangiwa kazi nyingine.

Alisema Joseph Rugumyamheto, aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Salum Msoma (Katibu Mkuu, Mawasiliano na Uchukuzi) na Bernad Mchomvu (Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), wanastaafu hivi karibuni kwa mujibu wa sheria.

Mkurugenzi huyo wa MAELEZO alisema Rais Kikwete atawaapisha makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu leo saa 3 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.
 
Wako wapi mashujaa wa Uhuru Tanganyika?



HISTORIA ya TANU ingelipotea kabisa kama siyo juhudi za makusudi za Profesa John Illife wa Cambridge aliyekuwa mwalimu wa historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika miaka ya katikati ya 1960.

Illife alipogundua tatizo lililokuwapo katika historia ya uhuru wa Tanganyika na hasa historia ya TANU na nafasi ya Julius Nyerere katika kuanzishwa kwake alifanya azma ya kuitafiti na kuiandika. John Illife aliwaagiza wanafunzi wake kutafiti na kuandika maisha ya wazalendo waliofanya mambo ya kutukuka katika sehemu zao. Zoezi hili lilipokamilika palipatikana historia za wazalendo wengi na kazi hii ikazaa kitabu Modern Tanzanians ambacho Iliffe alikihariri na yeye mwenyewe akiwa mmoja wa watu waliochangia uandishi akaandika maisha ya Martin Kayamba.

Kitabu hiki kina habari za maisha ya Watanganyika 12 ambao waliishi miaka ya mwanzo ya karne ya ishirini wakati wa utawala wa Wajerumani hadi kufika kwa Waingereza. Katika kitabu hiki kitu kimoja kinachojitokeza dhahiri ni kuwa wazalendo wote walioshiriki katika kutafuta Uhuru wa Tanganyika walikuwa Waislam. (Kleist Sykes, Ali Ponda na Hassan Suleiman) wao maisha yao yalijikita katika siasa za ukombozi wa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza wakati wenziwao Wakristo Canon Kolumba Msigala, Pastor Yohane Nyagava na Bishop Jeremiah Kissula) historia ya maisha yao ilikuwa katika nyanja za utumishi wa kanisa.

Hali hii imeendelea hadi ilipofika wakati wa kuasisiwa kwa TANU. Katika ukweli huu ndipo palipo tatizo la wanahistoria kuiogopa historia ya kweli ya TANU kwa kuwa harakati zilichukua mkondo mkali wa Waislam kupinga ukoloni kwa dhati. Kwa ajili hii basi historia nzima ya kudai uhuru imejaa majina ya Waislam. Hili ni moja ya sababu inayofanya historia hii iwe nyeti, iogopewe na isitafitiwe na kuandikwa inavyopaswa. Hili ni tatizo la kwanza.

Tatizo la pili ni watafiti kwa hofu au kwa kutaka kujipendekeza kwa Mwalimu Julius Nyerere kupuuza michango ya wale waliokuwa katika harakati za kupambana na ukoloni ama kabla ya Nyerere au walikuwa pamoja nae. Watafiti hawa pamoja na hata wanasiasa ndani ya TANU kwa wakati ule wakawa wanashindana katika kumjazia sifa Mwalimu Nyerere kuwa kwa hakika kabla yake hapakuwa na harakati zozote za kutaka kuikomboa Tanganyika. Hali hii iliendelea kwa kipindi kirefu hadi kwa mara ya kwanza mmoja kati ya waasisi wa TANU, marehemu Joseph Kasella Bantu alipoandika kueleza mchango wake katika kuunda TANU.

Katika makala ile Kasella Bantu alijigamba kwa kusema kuwa yeye ndiye aliyeitisha mkutano mkuu wa mwaka 1954(New African March 1985). Kassela Bantu ikawa hapa kama vile kafungua sanduku la Pandora kwa kuwa palitokea watu wakampinga kuwa hakusema kweli yote katika nukta ile. Mwandishi wa makala hii akiwa mmojawapo alimpinga Kassela Bantu (New African May 1985) kwa kusema kuwa kama ipo haja ya kutoa sifa kwa mtu mmoja mmoja basi sifa ile alistahili zaidi marehemu Abdulwahid Sykes. Mchango wa familia ya Sykes katika kuiasisi African Association na baadae TANU umejipembua vyema na unafahamika. Huu ndio ukweli wa historia ya TANU na mambo yalivyokuwa kati ya mwaka 1929 ilipoasisiwa African Association (AA) hadi 1954 TANU ilipozaliwa, iwe wanahistoria wanatambua au vinginevyo.

Sasa kwa kujua au kutojua Mwalimu Nyerere ambae maisha yake yote hakupenda kuizungumzia historia ya TANU au habari za wazalendo waliokuwapo katika siasa kabla yake, katika kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Busara mjini Tabora Mwalimu Nyerere alitoa hotuba kuhusu umuhimu wa kuwatambua wazalendo walioijenga TANU kati ya mwaka 1954 - 1958. Sababu ya kusema maneno hayo lilikuwa swali aliloulizwa katika mkutano wa hadhara na Mzee Ramadhani Singo mmoja wa wanachama shupavu wa TANU Tabora. Singo alimkabili Mwalimu Nyerere na kumuuliza ‘Mwalimu mbona umetusahau wenzako?' Swali lile liligusa hisia za Mwalimu na ile hadhira iliyokuwapo pale. Ndiyo katika kujibu swali lile Mwalimu Nyerere akawaadhimisha mashujaa walioingia TANU zile siku za mwanzo.

Kikundi kile cha wapigania uhuru wa TANU waliokuwa pale mkutanoni mbele ya Mwalimu takriban wote walikuwa wazee katika kanzu mbovu na nguo zilizochakaa. Katika hali ile hawakutoa picha iliyompendeza yeyote. Mwalimu Nyerere akiwa hakika katahayari kwa kuwaona wapigania uhuru wenzake walivyokuwa taabani aliona ipo haja kwa wakati na saa ile kuwaadhimisha. Ndipo aliposema waasisi wa TANU waheshimiwe. Sasa basi kwa Mwalimu Nyerere tokeo kama hili lilikuwa la pili kumtokea. Hali kama ile ilimtokea Kizota alipokutana na Dossa Aziz.

Mwaka 1987 katika Mkutano maarufu wa Kizota ndipo Nyerere alikutana na Dossa Aziz uso kwa uso baada ya miaka mingi kupita. Dossa mfadhili mkubwa wa Mwalimu na TANU alikuwa kachoka kwa shida. Dossa sasa alikuwa masikini na hali yake haikuweza kujificha. Kila aliyemjua Dossa na enzi zake alishtushwa na hali yake. Inasemekana hata nguo za kuvaa kuja katika mkutano wa Kizota ilibidi anunuliwe na rafiki yake mpenzi toka utotoni waliosoma darasa moja hapo Shule ya Kichwele (sasa Shule ya Uhuru) Balozi Abbas Sykes. Dossa aliweka mfuko wake wazi kwa Nyerere na TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Kadi yake ya TANU ni namba 4. Dossa ndiye aliipa TANU gari yake ya kwanza – Land Rover ambayo ndiyo iliyomtembeza Nyerere nchi nzima wakati wa kuitangaza TANU kwa wananchi.

Waliomjua Dossa na ukarimu wake walilia kwa kwikwi wakati wa mazishi yake. Waliona uchungu kwa kuwa Dossa hakuwa mtu wa kupanga foleni kungoja tiba Hospitali ya Tumbi. Hali ya Dossa ilimgusa sana Mwalimu Nyerere na haikupita muda Mwalimu alimnunulia Dossa gari imsaidie.

Turudi kwa Baba wa Taifa. Sasa kwa mara ya pili katika kipindi kisichozidi mwaka hali kama ile ya Dossa aliyoiona Kizota alikuwa anaiona tena kwa wazee wa Tabora – wapigania uhuru wa Tanganyika waliochoka na kupigwa sawasawa na ufukara. Ilikuwa lazima Mwalimu aseme kitu kuhusu hawa wazalendo aliowasahau au waliosahauliwa na historia na wakati. Mwalimu kwa kuwatukuza waasisi wale alisema kuwa siku za mwanzo za TANU zilikuwa ngumu na chama lazima kiwaheshimu wale wanachama wa mwanzo. Kwa kauli ile Mwalimu Nyerere akawa kanifungulia mimi njia ya kupita kwa kuunga mkono maneno yake. Nikaandika makala ambayo kwa mara ya kwanza nikasema kuwa historia ya TANU haiwezi kukamilika bila kutaja mchango wa Waislam na bila ya kumtaja Abdulwahid na Ally Sykes, Saadani Abdu Kandoro, John Rupia na Dossa Aziz (In Praise of Ancestors: Africa Events March/April 1988).

Mwalimu alichukua uongozi wa TAA toka kwa Abdulwahid Sykes. Uchaguzi huu una kisa kirefu cha kusisimua wakati mwalimu wa shule asiyejulikana Julius Nyerere kutoka Musoma alipomuangusha kwa kura chache sana ndani ya Ukumbi wa Arnatouglou Abdulwahid Sykes, kijana maarufu wa mjini na mtoto wa mmoja wa waasisi wa African Association ambaye baba yake, Kleist Sykes alifanya mengi katika maendeleo ya Waafrika kati ya vita kuu mbili za dunia. Inasikitisha sana kuona kuwa kipande hiki cha kupokezana uongozi kati ya marehemu Abdulwahid Sykes na Nyerere ni katika historia inayofanywa nyeti.

Wanasiasa wetu na hata Nyerere mwenyewe katika umri wake wote wa siasa aliijenga fikra yake vyema kiasi kuwa alifanikiwa kufuta katika ubongo wake ni vipi alikuja kupata uongozi wa TAA. Katika maisha yake yote hakupata hata siku moja kutamka majina ya wazalendo wenzake aliokuwa nao kati ya mwaka 1953 hadi 1961 Tanganyika ilipojikomboa.

Katika kupuuza historia ya siasa kabla ya kuja kwa Mwalimu Nyerere viongozi wetu imewalazimu kubadilisha msamiati. TAA chama ambacho kilidumu kwa miongo miwili kikipigania haki ya Mwafrika kikawa baada ya kuundwa TANU kinakejeliwa na wanasiasa wapya na watafiti wa historia ya uhuru wa Tanganyika. Ikawa kila inapotajwa TAA ile sura yake ya chama cha siasa huvuliwa kikaitwa ‘chama cha starehe.' Kwa maana ya kuwa TAA haikuwa lolote hadi Nyerere alipofika na wasemavyo wenyewe kuanzisha TANU.

Kwa mantiki hii ikawa lazima ilazimishwe kuwa TANU iliasisiwa na Mwalimu Nyerere peke yake bila ya msaada wa yeyote. Huu ndio ukawa mwelekeo hata wa Mwalimu Nyerere. Historia yote ya nyuma hadi kufikia mwaka 1954 ilipoundwa TANU ikazikwa na ikawa kama vile ni usaliti kuwataja wazalendo wengine waliokuwa katika siasa kabla ya Mwalimu Nyerere.

Leo hii wangapi wanajua kuwa siku ya mwisho walipokubaliana kuunda TANU mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAA New Street kwenye chumba kidogo kilichukuwa na samani duni? Ndani ya chumba kile walikuwapo wanakamati ya ndani ya TAA - Abdulwahid, Ally, Dossa, Mzee Rupia na Nyerere. Baadhi yao katika chumba kile walikuwa wamepindua masanduku ya bia na kuyakalia kwa kuwa viti vilikuwa havitoshi. Vyumba katika ofisi ile ya TAA vilikuwa vimepangishwa Muhindi aliyekuwa akifanya kazi ya kufua nguo (dobi).

Hiyo ndiyo siku walipokubaliana kuwa hapana sababu tena ya kusubiri. Wakati wa kupiga mbiu ya mgambo kuanzishwa TANU umefika. Baada ya uamuzi huu kufanyika Dar es Salaam, mjini Tabora Salum Abdallah na wazalendo wengine mmojawapo akiwa marehemu Abubakar Mwilima, George Magembe na wengine walikutana kwa siri kupanga mipango ya kumsafirisha Germano Pacha aliyekuwa katibu wa TAA Western Province kuja Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa kuanzishwa kwa TANU Julai 7 1954.

Salum Abdallah hatajiki popote katika historia ya TANU lakini ana kisa cha kusisimua katika maisha yake ya siasa kuanzia mwaka 1947 hadi alipowekwa kizuizini mwaka 1964 akiwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway Africa Union (TRAU). Salum Abdallah amekufa akiwa ameacha nyuma hazina kubwa ya kumbukumbu ya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Vipi leo tuambiwe bila hata ya chembe ya aibu ati African Association iliyokuja kubadilishwa jina na kuitwa Tanganyika African Association kilikuwa chama cha starehe?

Historia ya TANU yenyewe inakataa hili achilia mbali historia ya mzalendo mmoja mmoja na michango yao katika kudai uhuru. Kumbukumbu hizi zina uwezo wa kumsisimua mtafiti yeyote. Inasikitisha na kutia hofu kuwa nyaraka nyingi za TANU na nyingine zinazomuhusu Mwalimu Nyerere na uhuru wa Tanganyika kumbukumbu ambazo ni muhimu kwa historia ya nchi hii ziko mikononi mwa watu binafsi na nyingine hazitopatikana kabisa.

Mathalan wangapi leo wanajua habari za Erika Fiah au Ramadhani Mashado Plantan. Hawa ndio wazalendo wa mwanzo kufungua magazeti yaliyokuwa sauti ya Waafrika. Fiah alikuwa mmoja wa wanasiasa wa mwanzo kabisa wa mrengo wa kushoto na kalamu yake katika gazeti lake Kwetu alilolianzisha mwaka 1937 ilikuwa ikitema cheche kali dhidi ya ukoloni.

Nani anajua kuwa gazeti la kwanza kumpa Mwalimu sauti na kueneza sera za TANU lilikuwa Zuhra mhariri akiwa Plantan? Makala za Fiah katika gazeti lake la Kwetu ingawa zimeandikwa zaidi ya nusu karne sasa bado zina msisimko kwa msomaji kama vile kaziandika jana.

Au nani leo anamjua Mzee Yusuf Olotu maarufu Yusuf Ngozi wa Moshi na jitihada zake za kuipa TANU ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Kura Tatu mjini Moshi. Au mchango wa Sheikh Yusuf Badi wa Lindi au mchango wa Dk Michael Lugazia, Dk Luciano Tsere, Dk Joseph Mutahangarwa, Dk Vedasto Kyaruzi, Dk Wilbard Mwanjisi na wengineo?

Kizazi kilichopo sasa kina wajibu mkubwa wa kutafiti habari zao, kuzihifadhi na kuwapa heshima wanayostahili.

Alipokufa Dossa Aziz ilipofika wakati wa CCM kutoa rambirambi zao hawakujua waseme nini kwa kuwa viongozi waliokuwapo hakuna hata mmoja aliyekuwa anajua mchango gani Dossa alitoa kwa Nyerere na TANU na kwa bahati mbaya sana Mwalimu Nyerere hakuhudhuria mazishi yale.

Juma Volter Mwapachu katika tanzia aliyomwandikia Dossa, ‘Dossa Aziz a Fallen Hero' (The African 12 May 1998) alimlaumu Mwalimu kwa kukaa kimya kuhusu wapigania uhuru wenzake kiasi kuwa hakuna chochote kinachojulikana kuhusu mchango wao.


Mohamed Said ni mwanahistoria, mwandishi wa vitabu na makala.
samitungo@yahoo.com
 
Nadhani tatizo la teuzi za JK sio dini za wanaoteuliwa bali uwezo wao.Kuna ukweli usiopingika kwamba in TZ Wakristo wameendelea kielimu zaidi ya waislam,NA SABABU ni nyingi zikiwemo legacy ya colonial education.As a Chrstian myself,I'm least worried na informal affirmative action ya JK kuwaingiza Waislam serikalini.Suala sio quantity bali quality,na ndo maana technical posts nyingi serikalini including kwenye taasisi za ulinzi na usalama zinaendelea na zitaendelea kuwa chini ya wakristo...piga ua.Political posts ni vitu vya kupita,na kwa wenye wasiwasi na JK wafahamu kuwa between the two blinds (JK na PM wake) the latter ndio anaendesha nchi.So,latently,bado tuna Christian president.Mada ngumu hii,lkn nimei-approach kwa style ya mtaani.
 
Naam Mlalahoi,

Kwa kweli kama wateuliwa hawana quality ni tatizo, lakini wasiangaliwe wa upande mmoja tu linapokuja suala la quality, wako mabomu walioteuliwa wa dini zote. Na pia kama kuna muislamu bomu alieteuliwa na JK basi si lazima kuwa sababu pekee ya yeye kuteuliwa ni dini yake ... kuna factors nyingine... just like mkristo bomu alieteuliwa na JK si kwa sababu ya dini yake tu.

Technical posts kuwa chini ya wakristo wenye elimu nazo, as long as it is not at the expense of watu wa dini nyingine wanaoqualify, ni perfectly OK. Wasiwasi wangu ni huo msisitizo wa kuwa '..na zitaendelea kuwa chini ya wakristo.. piga ua', maana as the days go by, waislam na wale wa dini nyingine nao wanaelimika .. wanapata hizo technical qualifications na kuwa eligible, kwa hiyo sioni kwa nini posts hizo zisemwe zitaendelea kuwa chini ya wakristo, piga ua.

Alaa, kumbe JK ana informal affirmative action? nakumbuka uliwahi kuandika kuwa JK aliahidi hii affirmative action, sijui aliahidi wapi but may be you have your reliable sources on it. Kama ni kweli, nikicomment kwa style ya mtaani ntasema: an informal problem calls for an informal solution

Kama bado tuna rais mkristo in disguise kama ulivyoashiria... na nlivyowahi kuwasikia wengine wakidai hivyo.. , basi kumbe wakristo hawana sababu ya kuwa na wasiwasi wa udini, au wamlaumu mkristo mwenzao anaeendesha nchi.

Kwa wanabodi wengine, naweka links hapa za articles za Askofu Sylvester Gamanywa akianalyze huu wasiwasi wa udini walionao akina Augustine Mushi na wenziwe. Ameweka takwimu kukanusha hilo, na katoa ushauri kuwa wakristo wasikubali kusababisha wao kueleweka kuwa ndio wenye udini kwa kutoa shutuma zisizo na msingi, wasijenge hofu isiyo na ushahidi, wasijenge chuki za ubaguzi wa kidini, wasiwape wakati mgumu waislamu walioko madarakani ... kwani shutuma zikizidi zinaweza kuathiri utendaji na maamuzi yao, na pia ameshauri 'Tusichotaka kutendewa tusiwatendee wengine"

Je, ni kweli Serikali ya awamu ya nne ina udini?
Sehemu 1: http://www.wapotz.org/Serikali_Dini.html
Sehemu 2: http://www.wapotz.org/Makala_Bishop2.html
Sehemu 3: http://www.wapotz.org/Makala_Bishop3.html
Sehemu 4: http://www.wapotz.org/Makala_Bishop4.html
 
Tukumbuke tu kuwa CUF walibambikizwa kuwa chama cha kiislamu kwa sababu tu viongozi wake wengi walikuwa waislamu. Katika hili hatukujali kama wale viongozi walikuwa wana uwezo au la. Ila walikuwa waislamu! Inapotokea kuwa wateuliwa wengi katika uongozi wa CCM na serikali kwa nini tusitumie logic hiyohiyo iliotumika kwa CUF? Au mkuki kwa nguruwe?
 
Mwanasiasa.

Mkuki huo kwa nguruwe umeutiza chadema? hao majaji 20 kuna waislam?
wakuu wa wilaya walichaguliwa na JK, Idadi inaonyesha wakristu wengi sana tena hawana hata sifa.

makatibu tawala walichaguliwa na waziri Pinda kuna idadi kubwa ya wakristu,
juzi juzi tu wamechaguliwa makatibu wakuu wakiwa na BALOZI Mombo hakukuwa na muislam, tuambie ukabila, udini wa chadema hadi kutoa missada makanisani? acheni majungu.

Mlalahoi.
Betty Mkwasa ana elimu gani? ambayo waislam hawana na akapewa ukuu wa wilaya?
 
naitwa MUNCHALI plus, ni mgeni ktk uwanja huu hivyo nabisha hodi.Hodi jama!
leo nina swali: kwanini wa tz tunakubali kulizalilisha bunge ltu tukufu kwa kuendekeza uteuzi wa washenzi kama kina kifupa? tunapeleka wapuuzi bungeni, wakifanya upuuzi tunalaumu ama kusikitika!!! hamjui kuwa mchimba kisima huingia mwenyewe?

taifa hili lina vijana wengi makini, wenye elimu safi, upeo mkubwa wa kufikiri, na maadili yaliyotukuka lakini hawajitokezi na wachache wanaokijitokeza kugombea ubunge wanapigwa chini eti kwasababu tu hawana pesa,majina ama "back ups"! Baada ya hapo wanapatiwa nafasi watu ambao hata chizi anajiuliza kilichomvutia huyo mteuaji hadi akamteua mtu kama kifupa kuwa mbunge! hivi mnadhani bunge letu ni sawa na kwenda rusha roho lango la jiji?

inafikia hatua jengo la bunge linashushwa hadhi kiasi hiki?! utadhani si bunge bali kikao fulani tu cha walevi au danguro! mambo yakianza kwenda mrama tunaanza kulaumu lakini nani hasa alaumiwe haonekani! hivi kweli watanzania tuko serious na mstakabali wa taifa hili? imagine mtu kama kifupa kupewa ubunge!!kwa sifa zipi? au tunahitaji kuvaa miwani ya aina gani ndio tuweze ona kuwa hana sifa?

nchi yetu ina matatizo mengi ya kujadili jinsi ya kuyatatua, sio kutuletea watu wapuuzi bungeni na badala ya watu kuwaza apeleke hoja gani ambayo ni endelevu bungeni anawaza jinsi ya kupangua kashfa za ngono na kina kina kifupa!

baada ya kifupa subirini rose bangi 2010 anakuja! kama sasa hivi ameanza kujifua kwa kwenda kujitangaza kwenye TV na kuelezea umma jinsi alivyohangaika kumtongoza yule kijana wa kihuni mvuta bangi wa bongo flava, huko bungeni itakuwaje? badala ya kuchangia mswaada fulani si ataanza kueleza madaraka aliyowahi kushika kwa kuhonga...! Hawa wahuni mnawaleta bungeni ili iweje? kama wanataka kujulikana sio lazima waje bungeni si waende huko huko kwenye majukwaa ya bongo flava wacheze uchi wa Shigongo awaandike kwenye magazeti yake watafahamika sio watuletee upuuzi bungeni ala! eti rose bangi, ktk kipindi cha live redioni anasema presidaa mstaafu (ben) anamfahamu kwa jina! ajabu aliyoiona hapo ni ipi?

jamani tumeachwa nyuma kimaendeleo, tuwe makini tukatae wahuni wachache wanaotaka bunge liwe bongo flava au chipolopolo! ifike mahala hata kama watu kama rose bangi ameteuliwa na jk tukatae, yes tukatae kwani nchi hii si ya jk bali ya wa tz wote!
ni hayo tu.
BY MUNCHALI+
 
Swala la udini hupandikizwa kwa watu. Baada ya kusoma makala nyingi nadhani ni ukweli tu kuwa rais atachagua watu atakaoweza kufanya nao kazi kulingana na sera za chama chake. Itakuwa ajabu kama hao wanaoteuliwa ni wa chama cha upinzani. Nafasi zinazolalamikiwa ni chache sana kiasi takwimu zilizotolewa na zilizopo hazionyeshi upendeleo wa kidini au kikabila.
Nimeguswa sana na historia ya uhuru wa Tanganyika na mchango wa waasisi kutaka kugeuzwa kuwa wa kidini. Tusiingize dini huko, waasisi walitaka uhuru wa Mwafrika wa Tanganyika na wala si muislamu au mkristo wa Tanganyika. Wingi wa watu wa dini katika harakati za kugombea uhuru isiwe kigezo cha kuona kuwa walipigania dini.Ni ukweli wa kijiografia kuwa enzi hizo waislamu walikuwa wengi mijini na walikuwa shupavu kudaihaki ukilinganisha na wakristo.(Labda hotuba ya Lynch ilikuwa imeshawakumba). Laiti nasi wa kizazi hiki tungelichukua busara, uzalendo wao wa kutanguliza maslahi ya Tanzania, malumbano na hisia za udini zisingelikuwapo, hata mmomonyoko unaoonekana sasa ungalikuwa hadithi katika jamii. Tumwache rais achague timu yake, maksi zake atapewa kwenye uchaguzi.
 
ndg ni vizuri waswas wako kushare na sisi,but how do this may come to affect the general management of the party,just an advice pendelea kuwazia positive rather than negatives and avoid pressumptions.
 
Haya mawazo hapa chini niliyaposti kwenye Maoni.org, lakini kwa vile haifukuti, hakuna aliyejibu. Kwa vile nataka mawaidha kuhusu hili dukuduku langu, nimeona niposti hapa. Kumradhi kama nimefanya kosa.
====================================
Naona viongozi wa ngazi za juu za CCM sasa ni used soldiers. Mwenyekiti ni Kanali Kikwete, Katibu Mkuu ni Luteni Makamba na Naibu Katibu Mkuu ni Kapteni Mwanri. Haina neno.

Nina duku duku kuu: JK anapoteua viongozi, lazima aangalie asije akafanya watu wadhani ni mdini. Au JK ni mdini? Mbona safu karibu yote ya viongozi wa CCM alioteua ni wa dini moja? Kwa sasa, Mwenyekiti (JK) ni Muislamu, Katibu Mkuu (Makamba) ni Muislamu, Naibu Katib wakuu wawili (Jaka Mwanri na Saleh Feruz) ni Waisalamu, Mweka Hazina (Rostam Aziz) ni Muislamu, Organizing Secretary (Kidawa Hamad) ni Muislamu, Publicity Secretary - Internationa Affairs (Asha-Rose), nadhani naye ni Muislamu.

Huenda JK sii mdini, bali amejikuta tu akiteua watu wa dini moja. Na alipochagua mabalozi wapya alijikuta vile vile anakumbuka tu zaidi watu wa dini moja?

Si vema JK akaleta hisia za kidini. Huenda hakukusudia kupendelea dini moja, lakini ameleta hisia hizo. Ni vema akawa makini, ili hisia hizo zisiendelee.

Naamini kwamba ni vema kusema matatizo yanaweza kutokea wapi, kabla hayajatokea. Lazima tulinde amani tuliyo nayo kwa kusema yale ambayo tunadhani yanaweza kuleta matatizo baadaye.

Augustine Moshi

Moshi:

Katiba ya CCM inakwenda nusu Zanzibar na nusu Tanganyika. Ikifika ngazi ya kamati kuu uwiano wa kidini unakuwa mgumu kupatikana. Labda angefanya jambo la maana kumpiga kibuti Makamba nakumpa mtu mwingine.
 
hizo mada zako mzee umekosea katie kwenye mada ya siasa kwa mambo ya serikali na dini ni tofauti.

kama unataka kuzungumzia swali ya uislam kama kuna kitu umesikia msikitini au kwa wailam wengeuliza unakuaje? au ilikuaje? au hivi ni haki kwa uislam ? au ivi lakini mambo ya serikali hii sio uislam na wala haina uingiliano na uislam.

hapo umechemsha

kama una mambo ya ukiristo basi pia hapa unaweza ukaeleza kwenye mada hii pia tunaweza kuchangia hata mie nikachangia ninalolijua.

nafikiria hujaona ile mada issemayo mambo ya siasa.

kama hujatosheka unaweza kuungana na mrema kwenye chama chake mukajadili hoja zenu.

hiyo sio dini hiyo ni siasa.
sijakasirika wangu nakueleza kama umeona nimekukesa nisamehe
 
Mkandara,

Ni vema ukawa unajitahidi kuelewa kilichosemwa. Sikumlaumu Nyerere kwamba aliwaonea Wakristu. Nilitoa huo mfano wa Nyerere kunyanganya shule za Wakristu ili kupinga hoja iliyotolewa kwamba Mwalimu aliwanyima Waislamu kusoma.

Nyerere alifanikiwa sana kwenye kujenga umoja. Hakuonea dini wala kabila lolote. Alijaribu kumaliza ukabila kwa kufuta umangi, na kusaidia Waislamu wasome kwa kukamata shule binafsi, ambazo nyingi zilikuwa za za Wakristu, na kuzifanya mali ya serikali.

Na hao Wahindi unaosema wamesoma kuliko sisi wako wapi? Wahindi wa Tanzania huendeleza tu biashara, sio kisomo. Hawaendi vyuoni. Wakishafuta ujinga, basi, wanaondoka zao shule.

Augustine Moshi

Hata mimi Mkandara amenichanganya. Ulichokijadili kinaeleweka halafu yeye anakuja na kitu 'compleletly new' na sijui yeye ameelewa nini kwa kile ulichosema. Achana naye, umeeleweka vizuri ndugu yangu. Asitake kupotosha hoja hapa!
 
Asiyejua historia, basi atajikuta anairudia! Sikutaka kulizungumzia jambo hili la udini lakini kwa kutokufanya hivyo nimejikuta dhamiri yangu ikinisuta. Wakati watu wako matatani, au wakati wa shida au maangamizi, si ukatili wa adui utakaokumbukwa sana, bali ukimya wa rafiki zetu. Ni kwa sababu hiyo nimezungumza kwa kirefu juu ya nini Mhe. JK afanye ili kunyamazisha hii minong'ono ya udini. (Sikiliza: www.mwanakijiji.podomatic.com). Hata hivyo, nimeamua kuandika pia kwa wale ambao hawana uwezo/hawapendi kusikiliza KLH News. Kabla sijasema sana nitawanukulia hapa sehemu ya hotuba aliyoitoa Mwalimu katika kuadhimisha sikuu ya Uhuru Dec 9, 1968. Alizungumzia sana kuhusu "vitu ambavyo hatuna budi kuvisahihisha" (Soma: Freedom and Development Uk.74) Wakati Mwl. anatoa hotuba hii kulikuwa na minong'ono ya Ukabila iliyoanza kuingia na Mwl. hakulipuuzia hilo bali alilizungumzia mara moja. Ninainukuu hotuba moja kwa moja:

"First, I have begun to hear whispers about tribalism. Just after independence we got complaints that people were being appointed to government work on the basis of tribalism, and we immediately appointed a Commission to look into these allegations. The commission proved without any doubt that there was no tribalism in the allocation of jobs in government. But just recently I began to hear this complaint again. I did not treat this grumbling lightly. We called some of these people who were saying that there is tribalism, and told them to give their evidence either to me or to Chief Mang'enya. We promised to in investigate it immediately. But they have not given us one shred of evidence.

There are two things I want to say. The first is to ask any citizen who has some evidence of tribalism, to pass that evidence in confidence to anyone whom he trusts and who will be able to get the information either to me, to the First or Second Vice-President or to Chief Mang'enya. I promise you that we shall deal with anyone who practices tribalism.

But the second thing, and more important, is that the man who talks about tribalism being practiced without having any evidence for his statement is often a man who wants to stir up tribalism. Even if that is not his purpose, the result can be just the same. People will begin to think that there is tribalism and, once people begin to think in these terms, then tribalism has begun to enter into our society.

My purpose in bringing this matter out into the open is so that you may all be on your guard against people who want to stir up tribalism here. The work of civil servants is different from that of politicians. In order to be a political leader, a man does not have to have any particular educational qualifications. But the work of the civil servants and people in the parastatal organizations does require education - indeed, year after year we spend large amounts of money on education just so that later on our young people will be able to do the work of government and public institutions. For the time being we use foreign experts and those few Tanzanians who had the good fortune to go to school during the colonial times.

It so happened that the Tanzanians who had the opportunity for higher education under the colonialists were mostly Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa. And because most of the education was provided by missionaries, most of these people are also Christians. That was our inheritance. These conditions will change, but they have not changed yet. And for these reasons, when we get rid of the Europeans who were doing responsible jobs, and give these jobs to Tanzanians, the people who get them come mostly from one or other of these three tribes.

Therefore, if you ask me why Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa have most of the jobs, which require education, the answer is very obvious. They were the one who received higher education during colonial times. I'd say: investigate the position in politics where a man is not asked about his educational qualifications. Look at the parliament, the National Executive and Central Committee of TANU, and the Cabinet. How many Wanyakyusa, Wahaya, or Wachagga are members? You will find that perhaps there aren't any, or there are one or two. This is the truth.

Anyone who refuses to accept a very obvious truth like this, and says that the reason is tribalism, must provide us with the evidence for his statement. If he cannot provide any evidence, we must conclude either that he is a fool, or that he is stirring up tribalism deliberately. He is the sort of a person who begs work on a tribal basis, and when he is refused because he does not have the capabilities, he pretends he was refused on tribal grounds.

It is the job of the government to help, and even to favour, the more backward parts of the country, especially as regards education. We are doing this and will continue. But if a Mchagga, a Mhaya, or a Mnyakyusa young man were refused work simply because of his tribe-when he is capable and there is no other Tanzanian with the qualification- then we would be practicing a very stupid and very evil kind of tribalism such as that which caused the establishment of Biafra. I beg you, my brothers, avoid anything, which could bring our country into this kind of disgrace."


Sasa ukisoma hotuba hiyo, badilisha maneno ya Ukabila na weka neno la Udini. Halafu jaribu kufikiria kama Kikwete anaweza kuitoa hotuba hiyo na changamoto aliyotoa Nyerere (leteni ushahidi!). Sasa Kikwete afanye nini... mfano uko wazi!!!!

Mzee Mwanakijiji, asante sana kwa homilia yako. Imenikumbusha enzi za Mkapa. Wakati ule kukitokea manunung'uniko Mkapa alikuwa akidai mhusika alete ushahidi wa kina - kwa maana kwamba kama hakuna huo ushahidi basi hakuna kilichokuwa kinanung'unikiwa.

Na watu walioweza kuficha nyendo zao wakati wa Mkapa walikula nchi kwelikweli. Ukweli ni 'multi-dimentional' na kuweza kutoa evidence ni sehemu tu ya kujaribu kutafuta ukweli. Na isije ikaeleweka kuwa kutotoa evidence ni sawa na kusema ubaya fulani haujatendeka. Ukabila unaoukataa upo. Kama usingekuwapo hata msamiati wenyewe - 'ukabila' - usingekuwepo.

Sawa enzi za Nyerere ulikuwa umepungua kwa sababu ya watu kuchanganyikana katika kusoma na Jeshi la Kujenga Taifa. Baadhi ya sera za Nyerere zilipoanza kuupuuzwa ukabila ukaanza tena kujengeka. Na sehemu nyingi hapa Tz ukabila ni rafiki mkubwa sana wa NEPOTISM na UDINI. Kama wewe siyo mshikaji, dini au dhehebu fulani basi hupati kitu.

Mimi ninapata shida sana na reasoning ya kufikiri kuweza kutoa 'evidence' ndiyo kusema ukweli. How about cooked evidence?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom