Mkandara said:
Dr. Who,
Nimesoma toka hiyo ya nyuma lakini sikuona huo Uhuru unaozungumzia kuwa walikamatwa masheikh! navyojua mimi wakati wa mapinduzi kuna watu walikamatwa. Well, kwanza hapa lazima tuelewe nini maana ya neno MAPINDUZI!.. hili halina kheri kabisa kwa nchi yeyote ile.
Nadhani hukunielewa nilikuwa namuongelea Nyerere aliyewakamata hao ma sheikh na sikuzungumzia masheikh waliokamatwa zanzibar...Sijui uelewa wako wa hili suala zima la mapinduzi likoje lakini ningependa kukufahamisha kuwa si mapinduzi yote lazima DAMU IMWAGIKE kwa sababu Georgia kulikuwa na velvet revolution na hivi juzi kulikuwa na revolution nyingine THAILAND ambako bwana Thaksin liondolewa bila damu na wananchi wameliridhia hiyo sasa hebu rekebisha hilo...revolution si lazima damu imwagike
Swala la tanganyika kuimeza zanzibar sijui linaweza kuelezeka vipi tofauti kwani hata kama rais akitoka Zanzibar bara wataweka madai kuwa wanamezwa na Kisiwani. Tatizo hapa sii muungano isipokuwa sisi bado tumeweka tofauti baina yetu. Yaani kuna Mume na mke hapa!... Hiyo Sovereign Republic ni maandishi tu ndani ya katiba lakini watu wenyewe hatuyatambui zaidi ya haki ya kuwepo a sovereign state - Zanzibar!.
Kwa hiyo Dr. kama tukiondoa hizi hisia zetu za kutengana sidhani kama tunaweza kubishana hata hili swala la OIC na mengineyo mengi tu. Mbona Marekani sijawasikia wakidai kuwa rais katoka Texas kwa hiyo states nyingine zote zinatawaliwa?...
Well..waasisi wa muungano huu wamekuwa wakieleza kuwa waliamua kuziunganisha nchi mbili hizi, kutokana na sababu za kihistoria. Wanasema wananchi wa nchi mbili hizi wana asili moja na uhusiano wa karibu. Ni kweli Watanganyika na Wazanzibar wote ni Waafrika. Hilo halina ubishi. Na wala Zanzibar kuwa ni kisiwa hakuwezi kuwa ndiyo sababu ya kuvitenganisha visiwa hivyo vya Zanzibar na Bara la Afrika.Kwa vile wahenga wamesema "umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu",Lakini muungano wa nchi ni maridhiano baina ya wananchi wa zile nchi zinazohusika. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa na migogoro mingi tokea ulipoundwa. Nini kilichosababisha migogoro hiyo? Au kwa vile wananchi hawakushirikishwa? na kwa nini huoni umuhimu wa kurudia katika contract kuangalia kuna mamabo gani yamekiukwa na ikishindikana GET OUT CLAUSE inasemaje?
Kisha habari ya Muungano huifahamu na hata hao wanaohadithia hawaifahamu kwa sababu wengi wao walikuwa wanachama wa Hizbu. Na ndio hawahawa wanaodai leo hii kutaka kuona huo mkataba wa Muungano kwa sababu hawakushirikishwa... wamesahau kabisa kuwa wao walikuwa wamepinduliwa serikali yao na baadaye kurudishwa ndani na kuunda chama kimoja. They were not part of Mapinduzi na nakuhakikishia wote hawa hawapenmdi kabisa kusikia baraza la mapinduzi! Lazima tukubali kwamba uhasama kati yao bado upo hadi kesho na bara au CCM ni kisingizio tu.Hizi ni cheche za mgawanyo toka kwao na haiwezekani bila kulimenya chungwa (Tanzania) zima ili upate vipande vyake.
Huhitaji kuwa mwanachama wa HIZBU kuona CONTRACTS za muungao after all hili linawagusa wananchi milioni 40 sasa iweje mikataba muhimu kama hii iwe siri? hivi leo hii 2006 uko moto juu kuhusu mkataba wa RICHMOND lakini hutaki kusikia kuhusu mkataba wa muungano hii haingii akilini sasa watoto wetu mashuleni wanafundishwa nini...uozo au propaganda? kwa nini wasifundishwe kuhusu katiba yao au mambo ya muungano na mojawapo ni hiyo contract? labda kwa kukupa ushauri wa bure nadhani ungeanza na kuangalia huo muungano waliufikia vipi kwa kusoma kitabu kilichoandikwa na Amrit Wilson kiitwacho "Uhasidi wa Marekani kwa Mapinduzi ya Zanzibar"
Muungano wa Zanzibar ulipangwa kama yalivyopangwa mapinduzi! Plan ilikuwa moja na wahusika wakuu wa mapinduzi ndio waliokuwepo ktk muungano. Kwa hiyo huo muda wa miezi ni wewe una uona sio wanamapinduzi wenyewe. Hizo habari za CIA na mengineyo yote vichombezo tu kwani Okello hakutokea Marekani na pia unafahamu vizuri marekani wakitaka kitu hufanya nini. Tuliyaona Congo kwa Patric Lumumba, Nuriega na hivi sasa Saadam. Lazima marekani apandikize mtu wanayemtaka na Nyerere asingewashinda kwani walijua vizuri kuwa ni Mjamaa.... Hotuba zake za mwanzo kupinga Kutawaliwa na uchumi kumilikiwa na wageni ni ushahidi tosha kwa Marekani kuelewa Nyerere alikuwa kundi gani.
Mzee Mkandara unazidi kujionyesha jinsi gani suala hili linavyokuchanganya kwa sababu kama akina marehemu ABDUL RAHMAN BABU kutaka kuthibitisha kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitokana na mpango wa Marekani wa kutaka kulinda maslahi yake dhidi ya nchi za Kikoministi BABU alimquote mwandishi wa Kitabu hicho hapo juu , Bibi Amrit Wilson anaeleza, "siku ya tarehe 5 Machi (1964), Dean Rusk (Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, katika kipindi hicho) alituma simu kwenye ofisi za ubalozi wa Marekani Dar es Salaam, Nairobi na Kampala, kuwaagiza maafisa wa Marekani kuwasihi Nyerere, Kenyatta na Obote wamfahamishe Karume kuhusu hatari ya chama cha ASP kumtegemea BABU na hatari anayoleta Babu..... kwa usalama wa Zanzibar na Afrika Mashariki kwa jumla....." soma ukurasa 51.
Simu hiyo ya Dean Rusk ililenga katika kuwashawishi viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wawatanabahishe Nyerere na Karume juu ya hatari iliyokuwa inaweza kuletwa na Babu na makomredi wenziwe katika nchi zao. Kwa mujibu wa maelezo yaliyomo ndani ya simu hiyo inaonesha Marekani ilikuwa ikimwona Kenyatta kuwa alikuwa akiuelewa vyema ubaya wa Babu. Ndiyo Marekani ilipoona jitihada zake za kuwataka Nyerere aiunganishe Tanganyika na Zanzibar zimegonga mwamba ikaona imwombe Kenyatta awashawishi Nyerere na Karume juu ya kuziunganisha nchi zao, kwa usalama wao wenyewe.
Simu hiyo iliendelea kusema, "Haitakuwa jambo la busara kuifufua tena kwa Nyerere, mbali ya kukataa kwake kwa awali, fikra ya shirikisho la Zanzibar -Tanganyika kama njia mojawapo ya kumpa nguvu Karume na kupunguza mamlaka ya Babu? Hatua kama hiyo kwa wakati huu itasaidia pia kuimarisha nafasi yake mwenyewe Nyerere.
Siku hiyo ikamalizia kwa kusema, "vinginevyo, ukichukulia mwenendo wa Kenyatta kwa Babu, itakuwa vizuri kujaribu kwanza kumshawishi yeye atoe ushauri kwa Nyerere juu ya manufaa ya shirikisho la Zanzibar na Tanganyika, kama hatua ya kwanza kuelekea kwenye shirikisho kubwa la Afrika Mashariki naamini kuwa UKO UNITED STATES na hivyo kama unahitaji information zaidi basi angalia documents zilizokuwa declassified na jamaa wa STATE DEPARTMENT kuhusu huu muungano wa Tanganyika na Zanzibar utapata nyeti zaidi kisha utaelewa kilitokea nini
Hata hivyo, binafsi swala la OIC naamini ni haki yenu kuamua mnavyotaka kwani Zanzibar ni mke mwenye imani yake ya kidini. Hiyo katiba inasema Tanzania hakuna dini lakini ukweli utabaki kuwa - Zanzibar kuna DINI....
Kwa mantiki hiyo mimi naamini kuwa nyumba (Tanzania) inaweza kabisa kutokuwa na dini lakini mume na mke wakawa na imani zao tofauti, yet maintain relationship bila kuingiza maswala ya dini kwa nia mbaya. Yes, kila mmoja wao anaweza kutokuwa na imani na dini ya mwenziwe lakini swala hapa ni uhusiano wao ndio muhimu. Na nyumba zote zinazoweza kudumu ktk ndoa ya dini tofauti huwa zinaliweka swala hili kama swala la mtu pekee!..
Kwa hiyo Zanzibar kama wanataka kucheza Upatu na OIC wacheze but not on our expense!..
Our expense itakuja pale tutakapo jua pale hii mikataba itakapo wekwa wazi sasa tunakuwa kama wendawazimu tunakuwa tunanegotiate kitu ambacho wengi hawakijui kwani ni TOP SECRET!!!! The bottomline ni kuwa mgogoro mkubwa, ambao umekuwa ukijitokeza, mara kwa mara, ni ule wa kila upande, katika pande mbili za Muungano, yaani Tanganyika na Zanzibar, kudai kuwa unapunjwa na upande wa pili. Wakati Wazanzibari wanadai kuwa Tanzania Bara inataka kuimeza Zanzibar, na Watanganyika wanadai kwa nini Zanzibar iwe na serikali yake ndani ya Muungano wakati ile ya Tanganyika imeuawa?
Hapo ndipo inapochipuka ile hoja ya kuwa na shirikisho la serikali tatu - serikali ya Tanganyika na serikali ya Muungano; jambo ambalo Marehem Mwalimu Nyerere, katika uhai wake, alilivalia njuga kwa kulipinga kwa nguvu zake zote. Na aliyejitokeza kutetea serikali tatu alimnyamazisha kwa gharama yo yote ile MAFANO: Kitendo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar, wa Awamu ya Pili, Mheshimiwa Aboud Jumbe, kumwandikia barua Nyerere kumweleza kuwa kwa mujibu wa waraka wa makubaliano ya Muungano ya 1974, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ulikusudiwa uwe ni wa shirikisho lenye serikali tatu, na siyo mbili, au moja, kama inavyodaiwa na CCM -Bara, kilimsababishia Jumbe ajiuzulu nyadhifa zake zote, katika chama na serikali.
Na lile kundi la Wabunge 55 wa Bara, G55, walipotaka iwepo serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano, Nyerere wakati huo akiwa amekwisha ng'atuka Urais wa Tanzania na uenyekiti wa CCM, alisimama kidete kuwapinga wabunge hao na kulisambaratisha kundi lao. Aliandika na kitabu kuwasema na kuwakosoa aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamo Mwenyekiti wa CCM, Mzee Malecela na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Hayati Kolimba, kwa kile alichodai, kumshauri vibaya Rais Mstaafu, wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.
Lakini hilo halijaweza kuinyamazisha ile hoja ya kuwa na muungano wenye mfumo wa serikali tatu. Kama Mwalimu Nyerere alistahiki kupewa pongezi kwa kufanikisha kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, basi pia, anastahili kulaumiwa kwa kuweka mfumo wa muungano wenye kero nyingi? Na usiokubalika!
Sasa namalizia kwa kuuliza jamani what ever hapened with SOCIAL CONTRACT TANZANIA? mana noana tunapelekwa tuuu huku tunaambiwa hilo siri, hilo halifai kuuliza,hilo dhambi sasa tunalea jamaiii ya namna gani?