Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,290
- 2,468
Habari za Eid pili wandugu
Kama kawaida yangu ninapitulia ndipo jambo hunijia kama hivi halafu natafuta pakukitolea.
Nimekumbuka tu mbali kidogo miaka hiyo ya ubarubaru. Kipindi ambacho kwa bahati mbaya vijana wa kiume hukitumia ndivyo sivyo, pengine ni kwa kukosa misingi thabiti toka kwa jamii inayowazunguka.
Miaka ya 27 hadi 32 kwa vijana wa kike na wa kiume. Katika umri huu ni vijana wa kike ndio aghalabu huwa na focus ya maisha. Pengine huwa wamepevuka zaidi kuliko wa kiume.
Ni kipindi hiki ambapo vijana wa kike (wasichana) huchagua wanaume wa ndoto zao kwa maana ya kujenga maisha na familia. Huwa haitokei bahati mbaya ila wao kwa muda wao hufanya chunguzi zao na muda ukifika wewe kijana wa kiume uliyetunukiwa chaguo hilo utaona baadhi ya dalili na ishara.
Hapa naomba niweke bayana. Naongelea zaidi vijana wale ambao 'umande' kwao ulikuwa rafiki. Wale wengine hata miaka 18, 22 poa tu.
Dalili na ishara hizi hawa wanaume huziona bayana, tatizo linakuja, aidha hajamalizana na viruka njia au anaona huyo binti sio sahihi kwake. Tatizo la tatu huwa ni kipato. Hili la kipato likae pending kwanza.
Nasema haya kwa kuwa nimepita huko. Kama kuna makosa vijana wa kiume hufanya, ni kipindi hiki. Mwanamke aliyekuchagua kati ya wengi ndiye alipaswa kuwa mke wako. Bahati mbaya huwa tunawapuuzia na kwenda kuwatafuta wale wa vigezo vyetu.
Nawaasa vijana wa kiume. Mwanamke anayekuchagua kati ya wengi huyo mpe nafasi