Wasichana wa kiislamu wamekamatwa wakiwa wamefungiwa kwenye nyumba Dodoma, inayosadikika kupewa elimu ya dini

Mam...
Mimi nimeeleza tatizo hili kama ninavyolijua.
Sikulazimishi kukabaliana na mimi.

Ila najua Sheikh Yusuf Muhammad alikuwa anasomesha Uislam na kuhifadhisha Qur'an.

Haya ni mambo makubwa yenye heshima ya kipekee katika Uislam.
Kuna watoto wa Kiislam wananyimwa elimu kwa dhulma na hakuna anaelisemea.

Leo tunawasomesha watoto wetu elimu nyingine wewe unakuja na hoja ati wananyimwa elimu.

Angalia hapo chini:

Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu.

Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu.

Asilimia 29 ni wengine.

Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21.
Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe.

Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.

Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu.

Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga.

Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha.

(Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999).

 
Mam...
Mimi nimeeleza tatizo hili kama ninavyolijua.
Sikulazimishi kukabaliana na mimi.

Ila najua Sheikh Yusuf Muhammad alikuwa anasomesha Uislam na kuhifadhisha Qur'an.

Haya ni mambo makubwa yenye heshima ya kipekee katika Uislam.
Sheikh Yusuf Mohammad inaonekana ni msomeshaji pasipo elimu.
Haiwezekani mtu timamu kukusanya watoto wadogo zaidi ya mia ili tu kuwahifadhisha Quran.
Hili ni tatizo.
Hao watoto wakiwa watu wazima ni lazima watahisi walibaguliwa.
Maana watakutana na watu wenye age kama zao ambao hawakupita kwa sheikh Yusuf wakiwa na madaraka sehemu tofauti.
Mwisho wa siku tunatengeneza kizazi cha lawama na ubaguzi.
 
kuna wazee wengine ubongo hawana. kwahiyo mitihani hapa Tanzania huwa inasahihishwa na waalimu wakristo pekee? kana kwamba unataka kuuaminisha umma kwamba waislam wanafelishwa hawafaulu? mbona waalimu wanaosahihisha mitihani hiyo ni wa dini zote na wanatoa marks za haki? kweli wanafunzi wa kiislam wangefelishwa kwenye mtihani wa taifa halafu waalimu wasahihishaji walio waislam kwenye kundi la wasahihishaji wasijue? wazee wengine hawana faida yeyote hapa duniani.
 
Mfalme...
Kuna taarifa ya uchunguzi ya mambo yaliyokuwa yakipitika NECTA.

Ushahidi ulipokamilika ndiyo Waislam wakaamua kufanya maandamano na ule ushahidi ukapokelewa na serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani.

Mitihani ilisahihishwa upya na haki ikapatikana.

Itakuwa vyema kama utafanya uchunguzi kabla ya kuandika.
 
kwahiyo hoja yako ni kwamba waislam wanafelishwa makusudi, wanafalishwa na nani wakati wasahihishaji ni watu wa dini zote, mle kwenye chumba cha kusahihisha kuna waalimu wamevaa ushungi kabisa. au tueleze, walifelishwaje, au ndio ile kitu huwa mnalishwa tango halafu mnakuja na mihemko juu? mbona sioni kama una hoja kabisa mzee.
 
We mzee haupo sawa ktk hili,
Hiyo sensa ya kidini ilifanyika lini?
Bado hatujafika huko.
Pia hatupaswi kwenda huko, sisi ni "wamoja' WATANZANIA
kujibagua ni mapenzi yako
 
Mkuu mbona unatutisha?
Kwani waislamu ni special group kwamba tuwa pime kwa wingi wao?
Hii ni hatari sana
 
Mkuu mbona unatutisha?
Kwani waislamu ni special group kwamba tuwa pime kwa wingi wao?
Hii ni hatari sana
Mam...
Hapana Waislam ni raia kama raia wengine.
Tofauti yao na Wengine ni historia yao.

Hapo ndipo anapokuwa makhsusi.

Waislam wamepambana na Wajerumani kwa silaha.
Naamini unaijua historia ya Abdulrauf Songea Mbano.

Naamini unaijua pia historia ya Khadija Mkomanile.

Hawa wamlinyongwa na Wajerumani kama sehemu ya majemadari wa Vita Vya Maji Maji (1905 - 1907).

Naamini unaijua historia ya Abushiri bin Salim na Mtwa Abdallah Mkwawa.

Waislam ndiyo walioasisi African Association 1929 kupambana na Waingereza.

Waislam ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Waislam ndiyo waliomweka Mwalimu Nyerere kuwa kiongozi aongoze harakatiza za uhuru.

Historia hii ilikwepwa hadi mimi nilipoandikia kitabu cha Abdul Sykes.

Ikiwa hujasoma kitabu hiki kisome utashangazwa na mengi ndani ya kitabu hiki.

Kitabu kimebadili historia si ya Julius Nyerere peke yake bali historia nzima ya uhuru wa Tanganyika.

Sasa ukiangalia hizo takwimu katika hotuba ya Kitwana Kondo Bungeni utaona kuna jambo halijakaa vyema.

Au huoni unaona sawa hakuna kasoro?
 
We mzee haupo sawa ktk hili,
Hiyo sensa ya kidini ilifanyika lini?
Bado hatujafika huko.
Pia hatupaswi kwenda huko, sisi ni "wamoja' WATANZANIA
kujibagua ni mapenzi yako
Mam...
Hakuna suala la sensa katika hayo niliyoweka katika makala hiyo.

Kuhusu ubaguzi wa dini hilo ndilo alilotahadharisha Kitwana Kondo katika hotuba yake Bungeni.

Rudia kusoma na soma kwa utulivu.
 
Wanawaogopa! Mbona kule Bagamoyo kwa Ile NGO ya Mjerumani walitoa Maagizo mazito na wamiliki wakachukuliwa kupelekea kituoni police!!??
 
Kwa kuwa walianzisha harakati za uhuru wanatakiwa kuwa treated kama special case?
 
Kwa kuwa walianzisha harakati za uhuru wanatakiwa kuwa treated kama special case?
Nan...
Haiwezekani kutawala nchi kwa kuwafanya wengine ni bora kupita wenzao huo ni ubaguzi na Uislam umekataza ubaguzi wa aina yoyote.

Lakini kama ujuavyo baada ya uhuru mwaka wa 1961 walioshika madaraka ya kuendesha serikali hawakuwa Waislam.

Hili lilitia hofu wale walokuwa madarakani kuwa huenda siku moja Waislam ka juhudi walizoonyesha katika kupigania uhuru kwa nguvu hizo wakachukua uongozi wa nchi.

Historia hii ikawa inawatisha na juhudi zikaanza za kuifuta.

Kwenye Kumbukumbu ya Vita Vya Maji Maji Songea kuna kaburi la halaiki wamezikwa majemadari wa vita vile.

Kabla ya kunyongwa alitumwa Fr. Yohannes Hafliger kutoka Peramiho kuja Songea kuwafanyia ghilba wale majemadari ambao wengi wao walikuwa Waislam kuwaambia kuwa wakikubali kubatizwa na kuwa Wakristo hawatanyongwa.

Ukifika katika mnara wa majina ya hawa walionyongwa utaona majina yao ya Kiislam hayapo Khadija Mkomanile alipewa jina la Yacinta Mkomanile.

Abdulrauf yeye kaandikwa kama Songea Mbano.
Huu ndiyo ukawa mtindo.

Kuifuta historia ya kweli na kuweka nyingine.

Vipi utamfuta Abdul Sykes katika historia ya TANU atajwe Julius Nyerere peke yake?
 
Singida hii hali imeshamili sana na wazaz wao wanabariki hiko kitu , nlimpata mdada mmoja mzur kwel ila aliponiambia wapo msituni wanafundishwa madrasa nkaona hapa kuna ttzo tyr
 
kwa singida nmeona wanasema vpo vyuo vingi sana , kuna siku nlienda kutoa huduma hospital ya mkoa ya zaman nkapata mdada mzur sn nkamuomba namba akanpa ila aliniomba yang nkampa akawa ananipigia akipata muda , alinipa story kuwa wamechukuliwa wapo singida vichakani kbs na wanafundishwa ule msimamo mkali kbs wa dini na kisha wanaozeshwa kwa waislam wenzao kea idhini ya sheikh na sio mzazi
 
acha kupotosha , sio sahihi kukatisha masomo ya watoto , msiwe wapumbav kias hicho hao Iran na saudia wanasomesha wasichana wao kwan nyie mna dini zenu nyingine mbali na hz za wasaudia na Iran?
 
Sasa kwanini hawataki kukosolewa?
tusipende kuilamu serikali kwa kila kitu , hiz mamb hata wasaudia na irab hawawez ruhusu , kwann muwapeleke watoto vichakan tena mnawaacha kwa taasisi haijasajiliwa , baadae yakitokea majanga mnataka ilaumu serikali pia ?
 
Huwa unatetea Usilam hata katika UJINGA na UPUMBAVU

Unaona upande mmoja tu na hutaki kufungua akili yako kuelewa mengine

Huo ndio Udhaifu mlio nao wewe na kipenzi chako Ajuza FaizaFoxy wa Mkuranga
 
Thibitisha kuwa utafiti huu ni ws kweli na haujatokana na UZUSHI na MUHEMKO wa Kidini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…