Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Nafurahi kwa sababu zinaonesha uhalisia ambao kila mara unapuuzwa kwa nyimbo na mapambio ya watawala.
Kwangu mimi hizi video ni aina ya protest. Ni kilio cha mamilioni ya wanafunzi waliotelekezwa kwenye mabanda yanayoitwa shule pasipokuwa na uwezo wowote wa kutoa elimu.
Ni ujumbe wa wanafunzi kwa mamlaka na umma kwa ujumla. Ni barua inayosema “mnavuna mlichokipanda. Ukipanda upuuzi utavuna upuuzi na unapovuna upuuzi usiogope kujivunia mavuno yako.”
Kazi ya shule, among other things, ni kutengeneza character ya mwanafunzi. Character inajengwa kwa kum-keep busy mtoto na mambo ya msingi, ikiwemo ufundishaji, vitabu, michezo, vilabu vya fani mambalimbali, kazi za mikono, na mengine mengi ya aina hiyo.
Mtoto aliyepo busy kufanya experiments maabara, kujenga kipaji chake kwa kushiriki michezo mbalimbali, kusoma vitabu maktaba, kujihusisha na mashindano mbali mbali ndani na nje ya shule, etc., kamwe hawezi kuwa na muda wa kufanya jambo lolote linaloonekana kuwa la kipuuzi.
Hawezi kwa sababu amefanywa kuwa busy na mambo ya msingi. Kinyume chake ni sahihi pia. Mtoto anayenyimwa mambo yote haya, ni lazima atafute namna ya kuziba ombwe ikiwemo kwa kufanya mambo ya kipuuzi.
Theory nyepesi ni hii: Mwanafunzi lazima awe busy. Usipomkeep busy na mambo ya msingi na tija, atakuwa kept busy na mambo ya kipumbavu kwa sababu hiyo ni nature yake.
U-busy ndio shule halisi ya mtoto; kinachomkeep busy ndicho kinachomfundisha. Ni bahati mbaya sana kwamba tuna utamaduni wa kufunika kombe mwanaharamu apite. Baada ya hizi video kuonekana, ghafla maaskari wa maadili wameingia kazini.
Mara Waziri Gwajima ametoa tamko; Mara Mkuu wa Wilaya amewaita wanafunzi na wazazi na kuwashurutisha kuomba msamaha. Maelfu ya wanafunzi wa TEMEKE walipopata zero na Div 4 mwaka jana, fasta tukamuona Mkuu wa Mkoa ameita wazazi na walimu na kuanza kulaumu “malezi mabovu.” Jibu lake? “Tutajenga shule za kijeshi zenye walimu wanajeshi….”Yani kwa sababu tu una nyundo, basi kila kinachoonekana kwako kinageuka msumari.
Matokeo yake tunafunika kidonda huku tukiamini tumekiponya. Tunaacha tatizo, tunadeal na product ya tatizo. Uhalisia ni huu: KAMA HATUTOKUBALI KUBADILISHA HAYA MABANDA YA NG’OMBE ILI YAWE SHULE, HAKIKA TUJIANDAE KISAIKOLOJIA.
Niwakumbushe tu kuwa zaidi ya wanafunzi million 3 wanaanza kidato cha kwanza kwa mkupuo January 2028. Wacha tuendelee kujitekenya na kucheka!!