Wasichana Wanaowaza Mapenzi Tu: Ukweli au Stigma (Unyanyapaa) kwa Jamii?

Wasichana Wanaowaza Mapenzi Tu: Ukweli au Stigma (Unyanyapaa) kwa Jamii?

Last_Joker

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2018
Posts
272
Reaction score
414
Kuna kale ka-sentensi maarufu mitaani:
“Wasichana siku hizi akili zao zote ni mapenzi tu.”
Swali la msingi ni… ni kweli ama tumewatengenezea label tu ya "Love Machines" bila kuwapa nafasi ya kueleweka?

Real Talk…​

Ukisikiliza mazungumzo ya watu, hasa porojo za vijiweni, utaambiwa eti msichana hawezi kuwa single kwa muda mrefu – lazima atafute mtu wa kumtumia good morning, ampeleke Mlimani City au wapigiane stori kwa simu usiku wa manane.

Lakini jamani, si kila msichana yupo hivyo! Kuna wanaochambua CVs, wengine wanajituma na hustle za maana, wanajifunza tech, wanafanya freelancing, wapo bize na goals zao kuliko hata wanaume wanaowa-criticize.

Mapenzi ni Hitaji la Binadamu​

Sasa turudi kwa akili ya kawaida… ni kosa kweli msichana kutamani upendo? Maana tunasahau kuwa mapenzi si udhaifu – ni sehemu ya utu wetu. Mwanaume akilia kwa ajili ya mapenzi, watu wanasema “bro yuko deep.”
Msichana akilia – “mara ooh, hana kazi ya maana… mara mapenzi yamejaa kichwani.” Huu si ubaguzi?

Jamii Inatengeneza Taswira Potofu​

Kuna pressure kubwa inayowekwa kwa wasichana. Ukiwa na mtu – “Huyu anawaza mapenzi tu.”
Ukiwa single – “Huyu ni mgumu, anaringa, atazeeka kwao.”
Unatamani ndoa – “Anakimbilia kwa sababu ya kufata hela.”
Uki-focus na kazi – “Ni feminist, hataki mwanaume.”
Dah! Haya maisha ya wasichana yanataka roho ngumu kweli.

Lakini Tukubali…​

Wapo pia wasichana wanaopotea kwenye mapenzi hadi wanasahau maisha mengine. Wakikutana na "bebi" wa kuwalipia kila kitu, wanahifadhi brain drive. Hakuna plan B, hakuna kujitegemea, kila kitu ni kwa jina la ‘boo’. Hapo ndipo stigma inakaa kimkakati. Lakini si wote wapo hivyo.

Mwisho wa siku…​

Wasichana si robots za mapenzi. Wengine wanapenda, wengine hawana muda, wengine wanafunga ndoa, wengine wana-focus na kazi, na wengine wamejipanga kuwa first female millionaires kwenye familia zao.

Jamii inapaswa kupanua uelewa. Mapenzi ni sehemu ya maisha, si maisha yote – iwe kwa msichana au mvulana.

Unasemaje wewe?​

Hii kauli ya “wasichana wana akili za mapenzi tu” ni ya kweli au ni matusi ya kisasa kwa wanawake wanaotafuta mahaba?
 
Mapenzi wanabidi kuwaza vijana wadogo around 18-25

Huwa nasikitika ninapokuta MTU yupo above 30+ anakaa kuongelea ngono 24/7

So wanawake wanawaza Sana ngono ni vile hawapo occupied na majukumu ya utafutaji wenye tija
 
Back
Top Bottom