wasichana wengi wanaomaliza vyuo vikuu hawaolewi

Candid, mbona unatuonea? ina maana sie kina MwanajamiiOne ni wanaume? mbona tunaichangia hii mada au ndio sie ulotupa sifa ya kuingia kama mwizi????

hebu bwana.

Kuna thread ilianzishwa na Mbu juu ya ndoa za sasa hivi na za kale kuna element ya contribution ya elimu na hali ya wanawake kujitambua ambayo wengi walisema kuwa imechangia kwa wao kutokudumu katika ndoa zao lakini pia kuna maelezo mazuri sana ambayo yalieleza jinsi ambavyo makosa hayako kwenye wao kuwa wasomi au kuzitambua haki zao bali kwenye namna mtu binafsi anapoitafsiri elimu au kitendo cha yeye kuwa msomi au kuzijua haki zake.

mbona bado wapo ambao wanaelewa nafasi zao kama wanawake, wake pamoja na kuwa na elimu kubwa??
 
Nimependa sana uchambuzi wako, na furaha ilioje kutupa mengi mazuri kutokana na elimu na uzoefu wako kwani utawafaa walengwa katika mada hii kwa manufaa ya kujenga kizazi cha leo.

Elimu ni jambo zuri ambalo si kila aliye darasani ananufaika kwani wengine wapo kupata tu idadi ya miaka ya mahudhurio vyuoni, na wanaonufaika ni wale wanaopindua sarafu pande zote. Elimu tupatayo ni sawa na mshika jembe anayelima shamba, si wote wanatakonufaika na upatikanaji wa mazao, wacheche werevu ndio watasheheni mazao mazuri.

Tatizo la wengi wetu ni kuchukulia elimu kama ilivyo vitabuni bila kuchanganya na yako, maana walioweka hizo elimu vitabuni ni kama wewe na wala hazikutelemshwa kutoka ahera, ndio maana zina mapungufu, kwa maana kwamba ili kujenga hoja nzuri unatakiwa kuwa na nukuru kadhaa kujiridhisha.

Tukubali kwamba mara kadhaa tumechepuka kwenda nje kwa kufuata tu mikumbo au tamaduni nyingine kufikiria kwamba ndio maendeleo, lakini uwapo katika kipindi cha ujana inaashiria kutupa utabiri wa mafanikio na raha stahiki, lakini kwa jinsi unavyozidi kuingia ndani ya ulimwengu na kukutana na walimwengu utakuja kugundua uko mbali na ukweli na kushuhudia umepoteza nafasi ambayo ingekufikisha kwenye unafuu ingawa uvumilivu nao ungekusababishia unafuu huo.

Ukweli ni huu mwanaume kwa hulka yake ni mwanaume na mwanamke kwa hulka yake ni mwanamke. Kama kila mmoja akijiweka katika nafasi ya nature yake ndio ukamilifu wa maisha ya ndoa, la sivyo hakuna kitakachowekwa sawa. Biblia inasema wake waheshimuni waume zenu na wanaume wapendeni wake zenu hiyo ndiyo siri moja kubwa sana ya ustawi wa maisha katika ndoa.

Lazima kila mmoja mwanamke na mwanaume ateremke kutoka alipo au apande kutoka chini alipo wakutane ndipo mambo huwa sawia. Kubaki kung'ang'ania tu ulipo si suluhisho maana kila binadamu na kila gender wana mapungufu yao yanayohitaji kuvumiliana ili kujenga familia yenye kuimarika kwa upendo kamili.

Mpaka hapa tunakubaliana na tupo ukurasa mmoja. Ila sasa swali langu ni je elimu hii unayozungumzia inamfundisha mwanamke kutoka katika hulka yake ya uanamke? Kuna somo specific ambalo linafundisha mwanamke kumdharau mumewe?

Umesema vema uliposema kuwa kunahaja ya kuchukua elimu hii uchanganye na za kwako,.... UCHANGANYE NA ZA KWAKO! sasa je hii uchanganye na za kwako nayo inafundishwa darasani?
 
Wachezaji na wasanii wanapokuwa mazoezini hujengewa mbinu na hali ya mwili kuwa mwepesi afanyapo mambo jukwaani. Baada ya mazoezi awapo jukwani au mcheza mpira awapo uwanjani kwenye mpambano, anahitaji ziada ya akili yake kutokana na kutumia elimu aliyopata wakati wa mafunzo, akitegemea tu kutumia ile mbinu tu aliyofundishwa katu haitamnufaisha kupata ushindi. Ndio maana manju wa jukwaani huibua maajabu jinsi tu umati unavyohamasika na umahiri wake.

Tunaposema uchanganye akili yako na ya vitabuni tuna maana kutotumia tukisomacho kwamba ndio msingi wa kuishia, ila elimu hiyo hutusaidia kutufungua akili ifanye kazi vizuri kujenga maisha. Elimu si msingi wa kuishia bali ni njia ya kutufungua zaidi akili na kupanua bongo lifanye kazi yake vizuri, vinginevyo kufikiria elimu tuipatayo ndio msingi wa kuishia matokeo ndio kubaki kisiwani ambako wengi wanashindwa kukufikia kutokana mwenye kuishi kisiwani kutokuwa na upenyo wa kuangalia wengine wanaishije na nini afanye ili ulimwengu umfahamu na kumpokea alivyo.

Kuna masomo mengi tu ya kijamii amayo husaidia kumwelimisha mwamke katika ulimwengu wake, huko unaweza kuchota mengi tu, ila sijakuta elimu ya mwanake iliyofanya amdharau mwanaume. Tatizo la baadhi ya akina dada kuingia katika jina hizi hilo ni wale wanaochukulia ya vitabuni kama ndio maisha yanavyotakiwa.Vigumu kupa mtu aliye mkamilifu kwa kila jambo, na kigezo kikiwa hivyo ndio kinachotupeleka kukosa tunayemtazamia, na ipo siku tunaangukia kwa mtu tutakayewashangaza wengi. Ndivyo maisha yalivyo.

Kwa vyo vyote uvumilivu kwa pande zote ndio siri ya mafanikio na njia ya kukubalika, ila kuweka upekee ni tatizo linalowakwamisha wengi na kuishia kuamua kubaki walivyo kumbe ni kwa ajili ya kuficha dhana fulani yenye ukweli wa kutokukubali kuteeremka au kupanda kidogo.
 
katika utafiti niliofanya kwa miaka 2 wasichana wengi wanaosoma hadi vyuo vikuu huwa wankuwa na umri mkubwa , wachambuaji wa wachumba hali ambayo huwafanya wavulana wengi kuwakimbia(kuwapiga chini) hivyo kuishia kupigwa mimba na kuzaa watoto wasio na baba kitu ambacho huwa ni tatizo baadaye .Ili kukabiliana na tatizo hilo wasichana wa vyuo wamegundua mtego wa kuwanasa wanaume hasa wanachuo wenzao ambao ni mimba

Huo utafiti umefanyia wapi Mkuu!! mboni wengi tu huku wameolewa!! sema hao wanaokimbia wadada waliosoma ni wale wanaume wasiosoma na wenye ule utamaduni wa stone age kwamba baba ndio mwenye nguvu na sauti ndani ya nyumba!! (to brief it, These dudes are threatened)
 
Not true. Utafiti aliofanya hata mie nakubaliana nao, tusikwepe kuongea ukweli wakati hayo aliyoongelea tunayashuhudia kila leo. Na ndoa nyingi zinazovunjika ni zile za wasomi kwa vile hawana hulka ya kuvumiliana ila arguments ambazo hatima yake ni kuzidi kufarakana tu. Ukiona ndoa inadumu haina maana kwamba mambo ni tambalare la hasha, kuna kuvumiliana kati yao au mmoja wapo ameamua kuteremsha ili mambo yaende sawia. Kila mmoja akipandisha hakuna suluhu.
 
Hii ni kwasasababu jamii ya watanzania inaamii ukioa mwanamke liye kuzidi umri na elimu atakuendesha. Kubari uktae ukweli dio huo.
 
sababu wanakuwa wameharibiwa sana mitazamo wakiwa chuoni na mapezseee waliowafadhili kusoma /////baadhi yao///
 
Umenikumbusha nyimbo ya majirani wetu: musichana murembo hutaki kuolewa,hata university umwekenda umerudi, wasichana wa form four wanaolewa, wanakuacha wewe ukiangahika" Trouble is we, may be.
 
Napata ugumu kulikubali hili, kwanza utafiti wenyewe, na umehusisha sample size ya watu wangapi, pili, unaposema umri mkubwa ni relative term, lazima utaje unamaanisha miaka mingapi, hii pia inanipa shaka ya utafiti wako km hata ku-quantify tatizo, tatu najaribiwa kusema kwamba hujafanya utafiti ila umeangalia wanaokuzunguka, kwa sababu hujatoa uthibitisho wa aina yeyote ila umezua hoja inayotakiwa kufanyiwa utafiti.....toa detail tusome.
 
Hii mada huwa inakuja mara ngapi kwa mwaka?

Different versions of the same story
 
katika utafiti niliofanya kwa miaka 2 wasichana wengi wanaosoma hadi vyuo vikuu huwa wankuwa na umri mkubwa , wachambuaji wa wachumba hali ambayo huwafanya wavulana wengi kuwakimbia(kuwapiga chini) hivyo kuishia kupigwa mimba na kuzaa watoto wasio na baba kitu ambacho huwa ni tatizo baadaye .Ili kukabiliana na tatizo hilo wasichana wa vyuo wamegundua mtego wa kuwanasa wanaume hasa wanachuo wenzao ambao ni mimba

Miaka miwili tu then ikatosha kusema HAWAOLEWI?..na pia SAMPULI ulizofanyia utafiti wako zilikuwa na IDADI inayotosheleza?..na Je si mahali ulipo Mkoa/wilaya/tarafa/kijiji au mtaa vikakupelekea useme hivyo kwa kuwaona hao wachache unaoishi nao?..Je ulizingatia UMRI ambao dada zetu huwa nao wakati wa kumaliza chuo?..Vipi kuhusu ndoto na mahitaji ya dada mmoja baada ya mwingine juu ya mipango na matamanio ya ndoa, manake huenda nao wanafahamu kuwa si wanaume wote tulioko huku nje ni WAOAJI..nina mengi ningependa niyaone kwenye huu utafiti wako atleast yanithibitishie kwamba pana kitu UMESEMA, kinyume chake SIJAUONA UKWELI WOWOTE hapa, jipange tena urudie utafiti wako, Tafadhari zingatia mda, taja eneo la utafiti na lifanane na haja yako na idadi ya Sampuli iwe ya kutosha..thanks
 
katika utafiti niliofanya kwa miaka 2 wasichana wengi wanaosoma hadi vyuo vikuu huwa wankuwa na umri mkubwa , wachambuaji wa wachumba hali ambayo huwafanya wavulana wengi kuwakimbia(kuwapiga chini) hivyo kuishia kupigwa mimba na kuzaa watoto wasio na baba kitu ambacho huwa ni tatizo baadaye .Ili kukabiliana na tatizo hilo wasichana wa vyuo wamegundua mtego wa kuwanasa wanaume hasa wanachuo wenzao ambao ni mimba

Wanakuwa na UMRI MKUBWA kiaje?..(kwa taarifa yako kuna mabinti wengi chuo wengi wao ni around 1986-1991 na kwa miaka miwili ya utafiti wako dada zangu walonitangulia bado wangeangukia hapa between 1984-1987 kwa mtindo wa elimu ya nchi yetu hata wale wanotoka makazini hawawi wengi kuwazidi hawa dogodogo kwanza wao wanakuja tayari wakiwa wameolewa)..ko nisaidie UMRI MKUBWA wakati gani?...
 
Inawezekana kuna link imekosa kwenye utafiti wako mkuu, kwamba wanawake/ wasichana wanakua haraka kuliko wanaume yaani kwa mfano age mate wako kama wewe ni mvulana na yeye ni msichana atakua haraka kuliko wewe. Ndio maana hata majumbani ni nadra sana mtoto wa kiume kuoa kabla ya wa kike hajaolewa endapo mliongozana katika kuzaliwa hata kama ni mara mbili au tatu katika kufuatana huko.

Sasa tuje kwenye suala la kutoolewa ni kwamba wasichana wanaograduate wanakuwa wengi na pengine wamefikisha umri wa kuolewa au kupitiliza, sasa tuje upande wa kiumeni utagundua walio na uwezo wa kuoa yaani kuwa responsible ni wachache sana kwakuwa bado umri unawaruhusu kujirusha. Pia wanaume wanaangalia au wanajipima kama watayamudu majukumu ya ndoa watakapooa, cha kusikitisha idadi ya wanaoitwa wanaume nayo inapungua sana siku hizi kwani kuna wanaotaka kuolewa pia!
 
Not true. Utafiti aliofanya hata mie nakubaliana nao, tusikwepe kuongea ukweli wakati hayo aliyoongelea tunayashuhudia kila leo. Na ndoa nyingi zinazovunjika ni zile za wasomi kwa vile hawana hulka ya kuvumiliana ila arguments ambazo hatima yake ni kuzidi kufarakana tu. Ukiona ndoa inadumu haina maana kwamba mambo ni tambalare la hasha, kuna kuvumiliana kati yao au mmoja wapo ameamua kuteremsha ili mambo yaende sawia. Kila mmoja akipandisha hakuna suluhu.

Mtoa mada kasema WENGI HAWAOLEWI na sio NDOA kuvunjika upo hapo?..na kaa ufahamu sio sababu za mwanamke NDOA kuvunjika (wanandoa yani MME na MKE ndo huvunja ndoa)..usomi wa mwanamke si sababu ya kutofikia muafaka/makubaliano..kama kwako USOMI ni chanzo cha matatizo then utayaishia mapenzi mpaka kiama..
 
Yote uzushi, kwani huyu jamaa alifanya utafiti au alikuwa anapiga chabo tu? hili somo la udaku kujua umri wa kuolewa kwa wanawake wanaomaliza elimu ya juu lipo, vyeti vya kuzaliwa aliviona? Naona mabinti wengi hupenda kula vyakula vyenye mafuta mengi na kuwa na ****** (makalio) makubwa na kumchanganya umri. Anyway langu ni jepesi kwamba hata usome vipi hadi ukala chaki huna ubavu kwa wazee ulikotoka; hapa lazima upeleke mtoto freshkwenu kijijini na siyo bibi Kidude.
 
Hivi ukisema umri mkubwa unamaanisha miaka mingapi??
Issue iko hivi: wanaume mnaogopa wanawake wasomi kwa sababu baadhi yenu mnajijua kabisa hamna vigezo vya kuwaoa..
Mnaogopa wanawake wasomi kwa sababu wamewazidi ujanja economicaly&socialy..
Mnaogopa wanawake wasomi kwa sababu hawapelekeshwi hovyo cause hawamtegemei mtu...na wengi wao wanapenda kuishi independent lives bila kua na mume..
Lakini pia karibia kila baada ya miezi miwili hua nahudhuria harusi za marafiki zangu ambao ni wasomi nashindwa kuelewa utafiti wako ni wa sehemu gani specificaly!
 
Back
Top Bottom