Pole, inaonekana yashakukuta. Lakini nafikiri hii mentality wanaume tunatakiwa tuiondoe. Kinachosumbua hapa ni tu kwamba msichana liyesoma anazijua haki zake za msingi, kwa hiyo hatakubali kutumiwa kama duludoza. Na hapo ndo tatizo linapoanzia, maana wanaume wengi tunapenda tuonekane kama miungu watu. Lakini ukichukulia poa, ukawa unafanya naye mambo yote kwa kuzingatia usawa; (I mean unafua, unapika, unadeki unafagia uwanja pale unapoona inawezekana) hakuna utakachoona kigumu. Kwa kawaida mwanamke msomi ana kazi sawasawa na wewe. Kwa hiyo kama ambavyo wewe usivyo na nafasi, yeye pia hana. Kwa hiyo hawezi kuwa na muda mkubwa sana wa kukutumikia wewe tu. Kwa kiasi kikubwa mnahitaji mfanye kazi kwa usawa. Ndo maana wazungu wanawekeana zamu kwa kila kitu.