wasichokipenda CCM hiki hapa

wasichokipenda CCM hiki hapa

MMASSY

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
290
Reaction score
196
MAONI JUU YA RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2013.
Sehemu yeyote ambayo haijagusiwa katika Rasimu hii maana yake ni kwamba inakubalika na inapita bila kipingamizi chochote(kwa maoni yangu).Hata hivyo,ninashauri pale ambapo Tume inaona yafaa na kwa kuzingatia maslahi mapana zaidi ya taifa na wananchi kwa ujumla,inaweza kuboresha zaidi vifungu hivyo kwa shabaha ya kupata katiba yenye kiwango na ubora wa hali ya juu kwa miaka mingi ijayo mbele.Uchambuzi na maoni yangi yamejikita katika ibara nitakazozitaja hapa na maelezo yake.

SURA YA NNE

Ibara ya 39 kifungu kidogo cha 3 yaani ib 39.(3).Inatamka kuwa "Raia wa Jamhuri Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake".Kifungu hiki hakitakuwa na mantiki katika katiba yetu kwa sababu zifauatazo

i. Katika rasimu hii ,ibara ya 12 inaeleza kuhusu sera ya mambo ya nje na mwelekeo wa sera za nje za taifa huku ikisisitiza Tanzania itakuwa mastari wa mbele kupambana na makosa ya kimataifa ya kijamii angalia ibara ya 12(g).Kwa kuwa Tanzania imeridhia mikataba ya kimataifa kuhusiana na hakiza binadamu,za kisiasa na za kijamii,na kwa kuwa Tanzania ni mwanachama wa Umoja na taifa pamoja na vyombo vingine vya kimataifa,si vyema na wala haitakuwa busara kulinda raia wake kukamatwa,kuhojiwa na hata kujibu mashtaka nje ya nchi kwa kuwa kufanya hivi kutakuwa kunakikua mikataba hii ambayo taifa limeirdhia na kuidhinsha.Kwa mfano,Tanzania ni mwanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC iliyopo the Hague-Uholanzi.Ikitokea raia wake anatakiwa kushitakiwa katika mahakama hii kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu,Katiba yetu itakuwa inamlinda na kwa hivyo itakuwa inakinzana na sheria za kimataifa na pia kama rasimu hii ikipita kama ilivyo,kutakuwa na kujikanyaga kwa katiba kwa kuwa Ibara za 12(g)na hii ya 39(3) kitu ambacho kisheria kinaleta utata mkubwa kimantiki na hata kiutekelezaji.Ikumbukwe kuwa Watanzania ni sehemu muhimu ya jamii ya kimataifa na kwa hivyo nao wanatenda makosa kama raia wan chi nyinginezo,kwa hiyo,hakuna haja ya kuwawekea kinga kwa kuwa tutakuwa tunasaliti juhudi za dunia za kupambana na uhalifu.Kwa mfano katika tukio la kulipuliwa ubalozi wa Marekani hapa Tanzania mwaka 1998,Mtanzania mmoja tayari amefungwa kule Marekani kwa tukio hilo.Je kama tungekuwa na katiba inayotamka hili linalotamkwa katika rasimu hii hatuoni kama tungekuwa tunalinda uhalifu?.Kuna biashara haramu zinafanyika kote ulimwenguni na Watanzania ni wahusika pia,je kama kifungu hiki kikipita si kitachochea biashara ya uhalifu ambayo Tanzania kupitia kuridhia mikataba mbalimbali ya dunia imesaini kukabiliana nayo kwa ushirikiano na nchi nyinginezo?Sikubalianai na hoja kwamba makosa yaliyofanywa na Mtanzania akiwa nje ya nchi ama hapa nchini anatakiwa kushitakiwa tu hapa nchini kwa kuwa kutokana na wadhifa wake ama nguvu zake kwenye vyombo vya haki nchini anaweza kupendelewa.Nashauri na kupendekeza kuwa kama Mtanzania amevunja sheria popote pale duniani akamatwe mara moja na kukabidhiwa katika vyombo vya ngazi husika mara moja nah ii itasaidia sana pia kuheshimiana na mataifa mengine duniani.Mikataba yote iliyoridhiwa na Tanzania ina nguvu kisheria na kwa hiyo kama rasimu hii ikipita na kuwa katiba tayari itakuwa inakizana kwa ukali sana na sheria za kimataifa na mikataba mbali mbali ya kimataifa.Pia ni vizuri kuelewa kuwa sheria ni msumeno na kila mtu yuko chini ya sheria,rasimu kutamka kuwa raia wa Jamhuri hatapelekwa nchi nyingine pale anapofanya kosa kinyume na ridhaa yake,ni sawa na kusema kuwa raia yeyote katika Jamhuri anatakiwa atoe ridhaa yake ndio ashitakiwe kitu ambacho hakipo sehemu yoyote na wala katika mfumo wowote wa sheria duniani.Ni vizuri tukatazama vizuri sehemu hii na kuondoa kifungu hiki kwa kuwa hakina maslahi kwa taifa wala dunia na badala yake kimejaa maslahi binafsi ya washukiwa wa uhalifu na kukinzana na sheria zetu zenyewe na hata sheria za kimataifa.

SEHEMU YA SITA

MUUNDO WA SERIKALI YA MUUNGANO
Ibara ya 57(1a-c) na (2a-c).Inazungumzia kuwa Tanzania kutakuwa na serikali tatu(3)yaani ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania Bara.Hili ni wazo zuri sana na kwa kuwa haya ni maoni ya wananchi wengi na tangia siki nyingi,ni vizuri kifungu hiki kikabaki kama kilivyo kwa kuwa ndio njia sahihi na pekee ya kuendelea kuwa na Muungano hasa kwa mazingira haya ya sasa ya utandawazi. Ni kwanini tuwe na serikali tatu?

i. Uhuru zaidi kwa serikali za Tanganyika na Zanzibar.Kumekuwa na msuguano wa kimaneno na hata mara nyingine kuibuka nguvu katika suala la kutetea Zanzibar kuwa na mamlaka kamili na yote haya yalitokea Zanzibar kwa idadi ya wananchi kutaka kuwa na serikali yao yenye mamlaka.Kuwa na serikali za Tanganyika na ile ya Zanzibar kutawezesha serikali husika kufanya mambo yake kwa uhuru zaidi isipokuwa maswala yale ya Muungano ambayo pia yameainishwa katika Rasimu hii.Kwa kuwa kila upande utakuwa na serikali yake,Mahakama zake na hata Bunge(Baraza la Wawakilishi) lake,itawezesha nchi husika kuweza kuendesha mambo yake kwa uhuru zaidi na kuyaacha yale yaliyo ya Muungano tu ndio yashughulikiwe na mawaziri wa serikali ya Muungano.Hili limefanyika katika nchi za wenzetu kama Marekani na Muungano wao umedumu bila manung'uniko kwa miongo kadhaa na bado upo imara.Kwa hiyo njia pekee na sahihi ya kudumisha Muungano na kuondoa malalamiko itakuwa ni serikali tatu kwa shabaha ya serikali za washirika kuwa na uhuru zaidi.

ii. Usimamiaji mzuri na mgawanyo wa Rasilimali za umma.Kwa sasa kuna maswala yanayogombaniwa japo kwa maneno katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na rasilimali za taifa.Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wamesikika na kuonekana wakilalamika kwamba wananyonywa katika ugawaji wa keki ya taifa,kuna pia baadhi ya maswala kama Gesi na mafuta yana mvutano kama yawe ya Muungano au la.Katika mazingira haya,tunalazimika kuwa na serikali tatu kwa kuwa kila serikali ya upande Fulani itakuwa inasimamia rasilimali zake,ni vyema sasa kwa Rasimu hii kutokanusha uwepo wa serikali hizi tatu ili kutoa fursa kwa kila upande katika Muungano kusimamia ipasavyo rasilimali zao na kuwaletea wananchi maendeleo na kuyaacha tu yale ya Muungano ndiyo yashughulikiwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.Tumeshuhudia baadhi ya wananchi wa Zaznibar wakilalamika kuwa wanataka Gesi na mafuta yaliyosadikiwa kuwa Zanzibar yasiwe mambo ya muungano,na wengine wamewaga damu za watu wakidai kuwa na Zanzibar huru.Tukiwa na serikali tatu,kila serikali ikasimamia mambo yake na rasilimali zake yenyewe,tutakuwa tayari tumesshaondoa janga hili na kuendelea kuwa na nchi moja yenye mshikamamo amani na upendo.

iii. Kuna hoja zinatolewa pia kuwa kuwa na serikali tatu ni gharama kuziendesha.Kitu ambacho wakosoaji wa serikali tatu wanashindwa kukianisiha mpaka sasa ni gharama halisi zitakuwa kiasi gani za kuendesha serikali hizo.Wameshindwa kueleza namna serikali hizi zitakuwa na gharama kuziendesha kwa kuwa kuna ukweli kwamba kuwa na serikali ghali ama nafuu inategemea katiba yenyewe inavyosimamia rasilimali za wananchi na namna inavyowabana viongozi waandamizi wa hizi serikali kutokuwa wabadhirifu na kuendesha serikali kwa anasa(Gharama kubwa).Kwa sasa taifa linasumbuliwa na gharama kubwa za uendeshaji wa serikali japo tuna serikali moja tu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ndogo ya Zanzibar.Kwa nchi za wenzetu kama ile ya Marekani inayoongozwa na majimbo makubwa kuliko hata Tanzania yapatayo 53,kila jimbo linajiendesha lenyewe isipokuwa tu kuna serikali ya Shirikisho(Federal Government anayoongoza Barack Obama ambayo kwa mujibu wa katiba ya Marekani Ibara ya 1(8) inaiwekea serikali ya shirikisho mipaka mikali ya utendaji wa serikali katika matumizi ya fedha za umma katika maswala kama vile Ulinzi wa taifa,mfumo wa mahakama,ujenzi wa barabara,ofisi za posta na kulipa kodi ya taifa.Wenzetu wameiwekea serikali ya Shirikisho mipaka ya matumizi ya fedha ili kuacha mwanya kwa serikali za majimbo 53 uhuru wa kusimamia vizuri maendeleo yao.Hili limefanikiwa sana katika historia ya taifa la marekani kwa kuwa wao hawakutazama uendeshaji wa serikali kama ni gharama kubwa kwa sheria madhubuti walizojiwekea bali walitazama gharama za kulinda muungano.Sisi pia tunaweza kuzuia matumizi makubwa ya serikali hizi kwa kuziwekea mipaka ya madaraka na matumizi ya fedha za walipa kodi.Kuendesha serikali kwa gharama kubwa ama ndogo ni utamaduni tu ambao umezoeleka na tunaweza kama Watanzania kuukataa na fedha au rasilimali nyinginezo za nchi zikatumika kwa maendeleo ya wananchi.Ukifuatilia bajeti za nchi yetu na hata nchi nyinginezo Afrika utagundua kwamba robo tatu ya fedha zinazotengwa kwenye bajei zinaishia kwenye matumizi ya serikali.Sasa tujiulize,kwa mfano wa Tanzania,ni wapi wengi kati ya viongozi na wananchi?kama jibu ni wananchi,je ni kwanini asilimia 75 ya fedha za nchi zinatumika kuwahudumia viongozi?Ukishajibu hili swali unapata jibu kuwa kuendesha serikali kwa gharama ni maamuzi na utamaduni wa watu Fulani ambao watanzania tunaweza kuupinga kupitia Rasimu hii ya katiba na baadaye katiba yetu.

iv. Umoja na ushirikiano;ni ukweli usiopingika kuwa hata wanaopinga serikali tatu wanatambua kwa mazingira ya sasa na huko tuendako, kuna kundi moja linanyimwa haki zake ama la Zanzibar au la Tanganyika.Hii ni kwa kuwa unapokuwa na serikali ya Zanzibar na ile ya Jamhuri manake ni kwamba hawa Watanganyika wao hawana serikali ama unaitumia hii serikali ya Jamhuri ya Muungano kama serikali ya Tanganyika kitu ambacho pia kitakuwa si haki kwa Wazanzibari.Kimsingi kwa mfumo uliopo sasa ni kwamba serikali ya Jamhuri inafanya majukumu ya Muungano na yale ya Zanzibar kitu ambacho kimejengea watu wa Zanzibar taswira kwamba wanaamuliwa mambo yao na watu wa Tanganyika(Wabara).Kwa mazingira haya,tunapaswa kuwa na serikali tatu kama rasimu inavyopendekeza ili kuwe na serikali mbili za pande zote mbili za muungano na serikali moja kuu ya Muungano ambayo itakuwa ndiyo serikali kuu(mama).Likipitishwa hili basi tutakuwa na Muungano imara kuliko sasa kwa kuwa kila upande utakuwa na serikali yake lakini kuna serikali moja kuu ambayo itapatanisha pia serikali za washirika pale wakigombana.Kwa muundo wa sasa, ukitokea ugomvi kati ya Zanzibar na Bara ni ngumu kuumaliza kwa kuwa kuna mlalamikaji mmoja ambaye ni Zanzibar halafu kuna mwamuzi na mlalamikiwa ambaye ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Tumeona siku zote Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kimsingi inahusika kutatua kero za muungano,miaka mingi imeshindwa kutatua na kumaliza kero za muungano kutokana na aina ya muungano tulionao sasa.Njia pekee na bora ya kutatua kero hizi za Muungano ni kuwa na serikali tatu kama Rasimu inavyoeleza.Tusishawishiwe na vikundi ama vyama vyenye maslahi binafsi yasiyotii maslahi ya taifa.

SURA YA SABA

UCHAGUZI WA RAIS

Katika sehemu hii kuna kifungu/Ibara namba 76(3)ambayo inatamka kuwa "mtu aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania Bara au Zanzibar hatapoteza sifa za kugombea na kuchaguliwa kuwa rais wa jamhuri ya muungano kwa sababu aliwahi kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa Tanzania Bara au Rais wa Zanzibar".Kifungu hiki kina utata kwa kuwa ni ngumu kwa raia wa kawaida asiyeelewa maswala ya kisheria kujua urais ambao hautamnyima mgombea nafasi ni ule utakaokuwa umepatikana baada ya kuanza kutumika katiba mpya,ama hata Rais aliyewahi kuongoza Tanzania kabla ya 2015?.Ni vizuri Rasimu ikaweka wazi hili kwa lugha laini inayoeleweka vizuri kwa mwananchi wa kawaida.Kama inamaanisha kuwa ni mtu aliyewahi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kabla ya 2015 kwa maoni yangu si vyema kwa kuwa ukiisoma vizuri rasimu hii tokea ibara ya 75(a-i)na pia ukiisoma pamoja na ibara ya 76(4-5),utagundua pia kuwa kuna Watanzania wengi wenye sifa za kuchaguliwa kuwa Rais hivyo si vyema sana kwa mtu mmoja kuendelea kuwa Rais kwa muda wote huo.Ikumbukwe kuwa mtu aliyewahi kushika madaraka ya Rais ana nguvu kubwa na hata mabavu ya kufanya mbinu zozote halali na zisizo halali ili kuendelea kutawala.Ni vizuri sasa kwa kuwa Tanzania inao watu waliosoma vizuri,wenye ujuzi katika maswala ya Utawala,wakapewa pia mwanya wa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaachia waliomaliza muda wao kupumzika mara wamalizapo uongozi wao. Ibara ya 83(1)inaelekeza kuwa wakati Rais akiwa madarakani,hatashitakiwa wala mtu yeyote hataendesha mashtaka yoyote dhidi yake kwa ajili ya kosa la jinai.Pia ibara ndogo ya pili(2)inapiga marufuku kwa mtu yeyote kufungua kesi ya madai dhidi ya Rais.Ibara ndogo ya tatu yaani 83(3) inazungumzia kuwa kama mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais na sasa sio Rais tena kwa sababu nyinginezo ukiondoa ile ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa na Bunge na kusababisha mtu huyu kuachia ngazi ya Urais.Kwa maoni yangu na hata yetu sisi kama wananchi wa taifa hili,tunapingana na vipengele hivi na hasa kipengele kidogo cha tatu kwa kuwa kufanya hivyo kutamfanya Rais wa nchi awe Mungu pale awapo madarakani na hata pale anapokuwa ameacha madaraka ya Urais.Tumejifunza katika nchi yetu kuwa kuna viongozi waandamizi wa serikali wanaiba rasilimali za nchi kwa maslahi yao binafsi,wengine wanaweka fedha za watanzania nje ya nchi(kama USWIZI).Tumeona pia katika mataifa ya wenzetu viongozi wakiwa na madaraka ya Rais wanatumia vibaya madaraka yao kuwaangamiza wananchi wao hasa wale wanaotofautiana Kisiasa na Rais.Kumwekea Rais kinga mara awapo madarakani na hata akimaliza muda wake ni kama kukiuka sheria na msemo maarufu kwamba kila mmoja yuko chini ya sheria.Kuacha kipengele hiki kiende kama kilivyo,kuna uwezekano mkubwa wa kutopata katiba mpya kwa kuwa katiba hiyo itakuwa inaendelea kulinda viongozi zaidi kuliko maslahi ya taifa.Kwa mazingira ya siasa za ushindani wa ndani ya vyama na hata nje ya vyama,ni hatari kubwa sana kumwachia Rais kinga kubwa kwa kiasi hiki.Ikumbukwe kuwa Watanzania mara nyingi tumekuwa tukipigia kelele kuhusu kinga ya Rais na kupendekeza ifutwe kwa kuwa viongozi wengi hasa wa Kiafrika wanatumia mwanya huu kama njia ya kuwanyanyasa raia na hata kusababisha maasi makubwa kama yaliyotokea katika nchi za kaskazini mwa Afrika imesababishwa na viongozi kuwa na madaraka makubwa kiasi cha kuwanyima wananchi haki ya msingi ya kuwaadhibu viongozi wao wa nchi pale wanapokuwa katika nafasi za juu ya uongozi na hata pale wanapomaliza muda wao wa utawala.Ninashauri pia tume inayoratibu katiba mpya kutupilia mbali sababu za vyama vya siasa vinavyopendekeza kinga hii ibaki kwa kuwa havina dhamira ya dhati ya kusimamia wanachokisema badala yake wanafahamu kuwa mara kiongozi hasa wa ngazi ya Urais anapokuwa madarakani anafanya matendo yasiyo ya kibinadamu na ufisadi wa kupindukia na ndiyo siri kuu ya kuchomeka kifungu hiki.Kama mtanzania ninayeipenda nchi yangu na kwa kuwa pia jamii ya Watanzania ina watu wengi wenye mtazamo kama wa Kwangu,ninaomba sana kifungu cha kinga hasa anapokuwa amemaliza muda wake kisiwekwe na kikiwekwa kiwe kinatoa fursa kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi.Nitaeleza kwa kifupi athari za kinga ya Rais kutoshitakiwa.
Moja,itamfanya Rais atumie vibaya madaraka yake
Pili,itamfanya Rais asiwaheshimu wananchi wake na hata vyombo vingine kama Mahakama na Bunge.
Tatu,itamfanya Rais asizitumie kwa uadilifu rasilimali za taifa na kufanya ufisadi wa hali ya juu,
Nne,Rais anaweza kusababisha taifa kuingia kwenye migogoro kama ya kidini na kikabila kama rasimu hii haitatengeneza Katiba inayomwondolea kinga Rais.Kwa mfano,rais anaweza kusababisha maafa makubwa kwa matumizi mabaya ya madaraka yake na akafanikiwa kuvitumia vibaya vyombo vya dola na hata vya kisiasa kama Bunge kuzima hoja za wanaompinga.Lakini kukiwa kuna chombo huru ambacho ni mahakama na kikawa na nguvu kisheria kumsikiliza mlalamikaji(mwananchi)dhidi ya Rais na madaraka yake na baadaye kikaamua kutokana na sheria iliyowekwa,kitakuwa tayari kimeepusha taifa na viongozi wabovu na kusaidia kutatua migogoro kwa njia ya kisheria zaidi.


MSHAHARA NA MALIPO YA RAIS

Kifungu cha 85(1-2)vinazungumzia kuhusu mshahara wa Rais lakini kifungu cha pili kinamta kuwa "Mshahara na malipo mengine ya Rais hayatapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii".Watanzania tunauliza hivi!je,ikitokea Taifa limepata mtikisiko wa kiuchumi na tukataka mishahara ya viongozi akiwemo Rais ipunguzwe ili tujenge shule,tupate madawa hospitalini,tununue chakula,tugharamie chakula ili kulilisha taifa,je itakuwa haitusaidii?ni vizuri tuliangalie taifa letu kwa muono mpana zaidi.Kwa mfano,katika mataifa ya Ulaya yaliyokumbwa na mtikisiko wa kiuchumi(World Financial Crisis)viongozi walikuwa wa kwanza kupunguza mishahara yao na marupurupu mengine ili kunusuru taifa.Mimi naona tufute kipengele hiki na tuweke kipengele cha ulazima wa serikali kuboresha huduma za msingi za jamii badala ya kumlinda mtu mmoja anayeitwa Rais huku mamilioni ya wananchi wakikumbana na ugumu wa maisha.Ni kweli cheo cha Urais ni kikubwa na kinahitaji heshima lakini heshima hiyo isitokane na fedha za mlipa kozi maskini wa taifa hili,bali kitokane na utaratibu wa kumpatia huduma stahiki Rais na heshima katika kutekeleza majukumu ya Urais.Ni vizuri tukampatia Rais wetu mahitaji ya lazima na anayostahili lakini sio kuweka maswala ya kutopunguziwa mshahara na marupurupu kwa sababu kulipwa vizuri kwa Rais kutategemea pia uchumi wa nchi na juhudi za Rais huyo katika kuinua uchumi wa nchi ndizo zitakazoamua pia kama alipwe ghali ama kidogo.

SURA YA TISA

BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

Katika ibara ya 105(3) inatamka kuwa kila mkoa wa Tanzania bara na Wilaya upande wa Zanzibar itakuwa ni jimbo la uchaguzi.Kama kweli tunataka muungano udumu,hii sio njia sahihi ya kuutetea kwa kuwa,Zanzibar yenye watu wasiofikia miilioni tatu,itakuwa ina wabunge wengi mara kumi ya mkoa wa Dar es salaam ambao una wakazi zaidi ya Millioni tano.Tukumbuke kuwa,baadhi ya wilaya za Zanzibar ni ndogo na zina watu wachache kuliko hata baadhi ya Kata za Bara.Sasa ni mantiki gani itatumika hapa kwa uwakilishi bungeni?Utafutwe utaratibu mwingine wa kuwapata wabunge hawa kwa kuwa mikoa kama Shinyanga ambayo ni mikubwa kuliko hata Zanzibar itakuwa na wabunge wawili tu(mwanaume na mwanamke)wakati Zanzibar itakuwa na utitiri wa Wabunge.Tukitaka kuuenzi muungano kama kweli tunaongozwa na dhamira zetu,tuweke mazingira ya usawa katika maswala ya rasilimali na utawala,lakini usawa huo pia utokane na idadi ya wananchi wanaowakilishwa bungeni,na ukubwa wa eneo linalowakilishwa na Mbunge.Kwa sasa hakuna malalamiko mengi kutoka kwa watu wa bara lakini kama rasimu hii itapita kama ilivyo bila kurekebisha kipengele hiki,tutarajie malalamiko mengi sana kutoka bara ya kutaka usawa katika masuala ya muungano,au tutazamie basi watu wa bara kudai muungano uvunjike.

MMASSY JEROME
0786141643
aikaruwafm@yahoo.com
 

Attachments

Well analysed,usemi wa kiswahili "wakati ukuta..." ccm inazuia mkuki kwa viganja...
 
wajue kuwa hiyo siyi katiba ya ccm, wengine si wanachama wa chama chochote ccm wanataka tufuate yao
 
Summerise kamanda au

Kamanda soma acha uvivu ndio maana tunashindwa kuleta hoja za msingi kama mkuu Mmasy sababu tu ya kuwa wavivu wa kusoma. Mimi nashauri tuzitafute rasimu tuzisome tutoe maoni ya msingi kwenye rasimu hizo. Tukumbuke kuwa wengi wa waliochaguliwa kwenye mabaraza ya katiba upeo wa..........mh! Sasa kama tutawaachia hao tu basi katiba itakidhi matakwa ya kikundi fulani tu na sio nchi yote!
 
Well done Jerome; CCM wanaelekea kuwa kama hawajui wanachokitaka kwa kupinga muungano wa serikali 3. kama kweli wanataka muungano wa aina yoyote uwepo basi shurti wakubali muungano wa serikali 3 ambao utawaruhusu Zanzibar kuwa na uhuru zaidi ndani ya muungano na kwa hiyo kupunguza kile kinachoitwa "kero za muungano".
Kwa kuusoma upepo wa kisiasa kule visiwani na kuzingatia kauli za baadhi ya viongozi waandamizi wa Zanzibar kwa maana ya sauti za watu wasioweza kupuuzwa kama vile Mzee Hassan Nassoro Moyo na makamu wa rais Shk Sharrif Hamad unagundua kwamba kama CCM watapata watakacho kwa maana ya Muungano wa serikali 2; basi moja kwa moja casualty wa kwanza wa hatua hiyo itakuwa kuparaganyika kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar (SUK); kwani hauhitaji shahada ya uzamili kutambua kwamba CUF watajitoa katika SUK na kuturudisha enzi na Ngangari na Ngunguri na kwa hiyo kupelekea kuvunjika kwa serikali ya Muungano wa Tanzania.

CCM you better wake up to demands of the times; tunajua CCM ni chama cha zamani na huenda kimechoka kifikira; CCM wanatakiwa kujua kwamba katika maisha one can not have it both ways; To eat your cake and still have it!!? ni kichekesho to say the least!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
CCM mnan'gan'gania kubaki zamani ambayo zamani hiyo imeshapita at your own peril!

Wana CCM wenye akili ambao ninaamini ni wengi tu japo nashangaa kwa nini hawataki kutumia akili zao ipasavyo?! wanajua kwamba CCM na CUF are strange bedfellows in a marriage of convinience; the so called SUK which was neccessitated by the demands of the times. CCM; IF YOU CAN NOT CHANGE; REST ASSURED THAT CHANGE ITSELF WILL CHANGE YOU! and that is the rule of nature; not me a mere mortal!
Only time will tell.
 
Pamoja kaka.jana maeneo ya mwenge niliona rav 4 yenye logo za chadema bendera ya chama.baadae ikaja tena cruser ile ya chama saa kumi na moja wakapaki bar wanapiga tungi na madada wengine ambao hawakuwa na sare.ile tabia honest ile sikuipenda kabisa ..naomba watakaosoma hii post wawaonye wahusika wapaki magari huko waje kama wao..pls tunatumia muda na rasilimali kujenga image ya chama popote tunapokuepo .pamoja na kushawishi watu.sasa kwa mazingira hayo.not gud
 
Pamoja kaka.jana maeneo ya mwenge niliona rav 4 yenye logo za chadema bendera ya chama.baadae ikaja tena cruser ile ya chama saa kumi na moja wakapaki bar wanapiga tungi na madada wengine ambao hawakuwa na sare.ile tabia honest ile sikuipenda kabisa ..naomba watakaosoma hii post wawaonye wahusika wapaki magari huko waje kama wao..pls tunatumia muda na rasilimali kujenga image ya chama popote tunapokuepo .pamoja na kushawishi watu.sasa kwa mazingira hayo.not gud

heshima kwako mkuu....Natumaini chadema wamepata ushauri huo
 
Pamoja kaka.jana maeneo ya mwenge niliona rav 4 yenye logo za chadema bendera ya chama.baadae ikaja tena cruser ile ya chama saa kumi na moja wakapaki bar wanapiga tungi na madada wengine ambao hawakuwa na sare.ile tabia honest ile sikuipenda kabisa ..naomba watakaosoma hii post wawaonye wahusika wapaki magari huko waje kama wao..pls tunatumia muda na rasilimali kujenga image ya chama popote tunapokuepo .pamoja na kushawishi watu.sasa kwa mazingira hayo.not gud
Siku nyingine ukiwaona unawafuata na kuwaambia.
Waelelze waka-park magari ya chama ndio warudi kuendelea na mapumziko ya jioni kwa kulipa kodi (kunywa bia uiendeleze Taznania kwa kodi)
 
Back
Top Bottom