Wasichokitaka Tanesco ukijue hiki hapa, pitia uzi huu utanishukuru baadaye na utajipanga na hili

Wasichokitaka Tanesco ukijue hiki hapa, pitia uzi huu utanishukuru baadaye na utajipanga na hili

Dr Matola PhD

Platinum Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
62,453
Reaction score
111,795
TAARIFA

HALI YA UPATIKANAJI HUDUMA (UMEME)

Katika kipindi cha huu mwezi November tuna hali isiyoridhisha ya utoaji huduma kwa mujibu wa haki, wajibu na taratibu za utoaji huduma kwa wananchi ( wateja) kama mikataba yetu ya huduma kwa wateja inavyoelekeza

Takribani 23% ya wateja wetu wamekuwa wakiathrika Kila siku .

CHANGAMOTO
Tumekuwa na changamoto ya upungufu wa nguvu ya umeme ktk mifumo yetu ya Grid ya taifa.

CHAZO CHA UPUNGUFU
Mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyopelekea ukama (famine& drought) ktk sehemu kubwa ya nchi yetu yamepelekea mitambo yetu inayofua nishati ya umeme kwa kutumia nguvu ya msukumo/ mtiririko wa maji( kidatu,mtera,kihansi,hale,na nyumba ya mungu) kupoteza uwezo wake wa awali kwa 87%.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA
Ili Kukabiliana na upungufu huu,shirika limechukua hatua kadha wa kadha ili kuepukana na athari za kadhia hizi ambazo zinaweza kusababisha nchi kuingia ktk vipindi vya Giza totoro kama ifuatavyo
1: Kuongeza kiasi Cha uzalishaji kwa kutumia gas asilia.
2: Kupunguza masaa ya upatikanaji umeme kwa baadhi ya wateja from 24hrs to 12hrs kulingana na hali ya siku husika.

MBINU NA NJIA ZA UTEKELEZAJI
1: Kuhakikisha maeneo yote yanayotoa huduma za jamii hayaathiriki kwa kiasi kikubwa( shule,vyuo,Kambi za majeshi,viwanda vya dawa, ofisi za umma nk.

Hali hii imeleta changamoto kwa wateja wetu waliopo karibu na maeneo yenye taasisi hizo kuonekana wanapendelewa sana kwa kupata Umeme 24hrs.... hapana hii nikutokana na wateja hao kuhudumiwa pamoja na njia moja ya umeme na taasisi hizo tajwa.

2: Kupanga utaratibu na ratiba za katizo la umeme kwa baadhi ya maeneo kuendana na hali ya upungufu ktk mifumo yetu ktk siku husika.

CHANGAMOTO
Kwa kuwa hali ya upungufu mara kadhaa huwa haitabiriki ktk mifumo yetu kwa sababu inategemeana na matumizi ya umeme kwa wateja ktk siku husika, hivyo kupelekea kuzima umeme ktk baadhi ya maeneo kwa hati ya dharula pasipo taarifa za awali kwa wateja. Tunaomba radhi na uvumilivu wenu ktk hilo.

Pamoja na changamoto hizo kwa vyovyote vile tunahakiksha hakuna mteja au wateja kukosa umeme kwa zaidi ya 12hrs ktk siku husika.

Kipindi hiki Cha upungufu wa nishati tunakitumia kama favour in the disguise kwa maana ya kufanya matengenezo toshelezi ili hali ikitengamaa kusiwe na hati za kuzima umeme tena kwa ajili ya matengenezo au visingizio mbalimbali vya kukatika kwa umeme ktk maeneo yetu.

Tanesco ni yangu, yako, yule,yeye, na wewe kama watanzania kwa pamoja tutaweza na kushinda vita hii.

Ahsanteni,
 
Kipara anafaa achapwe chuma hadharani. Karne ya 21 utumbo huu?
 
[emoji23] unaambiwa majenereta yamepanda bei!.kukaa na ndoo za maji chumbani.

Hivi tanzania ina viongozi wa kuchekesha alafu tunatumiwa sms kuambiwa tumeongeza ila walikuwa hawa fahamu vyanzo vengine vya kuzalisha umeme kama mbadala
 
[emoji23] unaambiwa majenereta yamepanda bei!.kukaa na ndoo za maji chumbani.

Hivi tanzania ina viongozi wa kuchekesha alafu tunatumiwa sms kuambiwa tumeongeza ila walikuwa hawa fahamu vyanzo vengine vya kuzalisha umeme kama mbadala
Halafu eti rais mtarajiwa ni Kipara!!! hivi Tanzania ni nchi iliolaaniwa ???? Maana viongozi wamelala toka 1990s kutafuta vyanzo vya maji na umeme kweli??? Mwendazake kidogo akaja na wazo la bwawa la Nyerere, ila sasa huyu mama yetu sijui yeye kajipanga na nini au ndio na yeye akimaliza muda wake bado shida ni ile ile. Siku rais akiwa kipara nitaukana utanzania mazima na nitadeclare mimi ni mkenya 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom