Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Majina kamili ni Profesa Mohamed Yakub Janabi ni mtaalamu wa magonjwa ya moyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Mshauri wa Rais katika masuala ya afya.
Profesa amekua mtafiti mkuu wa majaribio ya chanjo ya VVU (HIV Trial vaccine), Amehudumu kama daktari bingwa hospitali ya taifa Muhimbili, Amekua country director wa Madaktari Afrika, amekua Daktari Binafsi wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete tangu mwaka 2005 mpaka sasa, amekua Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) tangu mwaka 2014 mpaka mwaka 2022, amekua Mkurugenzi Mtendaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) tangu Oktoba 2022 mpaka sasa na juzi ameteuliwa kama mshauri wa raisi katika masuala ya afya.
Profesa alipata shahada ya kwanza ya udaktari wa binadamu mwaka 1989 kutoka Kharkov Medical Institute huko Ukraine, Kisha masters ya Tropical Medicine mwaka 1994 kutoka chuo kikuu cha Queensland, Australia na baadae PhD ya Cardiology (magonjwa ya moyo) akiwa nchini Japan katika chuo kikuu cha Osaka ambako pia hapo hapo aliongeza Postdoctoral Fellowship ya Cardiology (magonjwa ya moyo).
Ni Profesa wa magonjwa ya moyo tangu mwaka 2003, mpaka sasa ni Mwenyekiti wa bodi ya THPS tangu 2022, mjumbe wa bodi ya chuo kikuu cha afya Muhimbili tangu 2022, Mjumbe wa bodi ya JKCI tangu 2022, mjumbe wa bodi SUA tangu mwaka 2016, mlezi wa Taasis ya lishe na kisukari Tanzania, mjumbe wa baraza la madaktari Tanzania, mjumbe wa TPHA, mjumbe wa Royal society of tropical medicine and hygiene, mjumbe wa Japanese society of vascular medicine, mjumbe wa American Heart Association na Mjumbe wa Japanese society of echocardiography
Profesa amepata tuzo za heshima kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), American College of Cardiology (FACC) lakini pia ni mwanachama wa Kudumu wa Medical University of South Carolina, Marekani. Profesa Janabi ameanzisha na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na mashirika makubwa kama Mending Kids (USA), Open Heart International (Australia), Save the Child's Heart (Israel), Sharjah Children’s Charity (UAE).
Profesa anaongea lugha 4 ambazo ni Kiswahili, Kiingereza, Kijapan na Kirusi.
Profesa ameshiriki kwenye utafiti na kuandika scientific papers zaidi ya 77.
Andiko hili nimelikopi mahali na kuwaleteeni hapa na siyo andiko langu Binafsi.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.