Wasifu wa Bernard Kamilius Membe

Wasifu wa Bernard Kamilius Membe

Mate yanakudondoka kwa mwanaume mwenzio kiasi hicho, uwiii ma delicious mko wengi walahi
Chadrama suruali zitavuliwa walahi uwiii
Hivi huwa unafikiri kabla ya kuandika? Jukwaa hili siyo la watoto waliokosa maadili kama wewe bali ni la watu makini wenye elimu, heshima na staha katika jamii na nchi kwa ujumla wake! Nikuonye tu kishkaji, hebu jifunze jinsi ya kuwasilisha hisia zako badala ya kuandika hivi ambapo hata unayemtetea huwa anasoma tulichoandika humu! Unajua ni kwanini aliamua kuwanunua wapinzani na kwenda kuwapata nyadhifa? Jitafakarishe na badilika sana ili kuitunza heshima yako na ya jukwaa!
 
Kwa muda mchache ambao nimefanikiwa kuwapo Jamii forum nimegundua kuwa jamii forum wamejaa Walio tumbuliwa(vyeti feki),Mafisadi wakubwa,wasio na kazi(oya oya),Wapenda maisha ya mtelezo,Wazee wa kubet,wasaliti wa serikali,wakina delicious,Ma great thinkers(wachache),Wazalendo(wachache),Mazuzukia(kama wote),Wavivu na dharau(hawa wanaonekana ni wafanyakazi wa umma),much know(wakina kajua yote),Matajiri ndoto(wanaojifanya matajiri jf uku kwao choka mbaya),wanzinzi,wapiga nyeto,wanadini(wachache)

Samahani kama nntakuwa nimekuudhi kwa maana mara ya kwanza naingia jf nilijuwa ni `home of the great thinkers' Lakini kumbe kwenye msafara wa mamba kunaweza kuwa na kenge wengi kuliko mamba

nasubiri matusi
 
Sawa mtoto wa mama tumekusoma
 
Hapo ni sawa na kusema 1+1=2
Then mtu aje akutukane.

Hapo nani ataonekana ni mjinga
 
Bernad Kamilius Membe alizaliwa tarehe 9 Novemba, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati wa watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe. Kwa kabila, Bernard Membe ni Mmwera, na kama ilivyo desturi ya Wamwera, watoto hutumia jina la ukoo wa Mama. Hivyo watoto wote saba wa familia hii ya Mzee Kamillius wamekuwa wanatumia jina la upande wa mama yao, Cecilia, yaani Membe.

Elimu:
1962 – 1968: Elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Chiponda, Lindi.
1969 – 1972: Elimu ya Sekondari, (O-level) Namupa Seminary, Lindi
1973 – 1974: Kidato cha tano na sita (A-level) Itaga Seminary, Tabora
1975 – 1980: Aliajiriwa serikalini, ofisi ya rais
1981 – 1984: Alipata Shahada ya kwanza katika tasnia ya Sayansi katika maswala ya Siasa na mahusiano ya kimataifa (Bachelor Political Science and International Relations)
1985 – 1989: Aliendelea na ajira yake serikalini katika katika ofisi ya rais
1990 – 1992: Alipata Stashada ya Uchumi, Mahusiano ya Kimataifa na Sheria za Kimataifa (Masters- Economics, International Relations and International Law)
1993 – 1994: Alirudi serikalini kuendelea na kazi kama mchambuzi za mambo ya ulinzi na usalama

Mafunzo:
Kati ya mwaka 1975 na 1976 Ndugu Bernard Membe alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Oljoro, Arusha. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ambapo vijana wote waliohitimu kidato cha Sita walitakiwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya Jeshi, Ndugu Membe aliajiriwa katika Ofisi ya Rais, Utawala bora.

Mwaka 1978, Ndugu Membe alipata Mafunzo ya sheria za Jinai na usalama wa nchi, nchini Uingereza. Aidha, mwaka 1980, Ndugu Membe alipata mafunzo ya siasa, katika Chuo cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Kivukoni, Dar es Salaam.

Familia:
Mwaka 1986, Ndugu Bernard Membe alifunga ndoa Takatifu na Dorcas Richard Masanche, katika Parokia ya Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam. Ndugu Membe na mama Dorcas wamejaliwa kupata watoto watatu, Cecilia, Richard na Denis.

Siasa:
Ndugu Membe ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Kamanda wa Vijana wa Mkoa wa Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, na Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Mwaka 2000, aliingia Bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtama, kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya uchanga wake bungeni, akiwa kama mbunge wa kawaida (back bencher), Bernard Membe alikuwa mchangiaji mkubwa wa mijadala inayohusu Amani, Ulinzi na Usalama pamoja na Utawala Bora.

Mwaka 2005, Bernard Membe alichaguliwa tena na wananchi wa Jimbo la Mtama kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Tofauti na kipindi cha nyuma, Bernard Membe alianza muhula wa pili wa Ubunge, Januari 2006, kama ‘front bencher’ baada ya kuteuliwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Kufuatia mabadiliko ya baraza la Mawaziri mnamo mwezi Oktoba, 2006, Bernard Membe alihamishwa Wizara na kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati na Madini – moja ya wizara ngumu na nyeti kwa Taifa.

Hata hivyo miezi michache baadae, yaani January 2007, rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Bernard Membe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa baada ya aliyakuwa anashikilia wadhifa huo - Dr Asha Rose Migiro - kuteuliwa na Katibu Mkuu Baraza la Umoja wa Kimataifa na kuwa Naibu Katibu mkuu wa baraza hilo. Bernard Membe amehudu katika nafasi hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu 2007 hadi 2015, akiwa ni Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo kwa miaka mingi mfululizo, akitanguliwa na Rais Kikwete ambaye alidumu katika Wizara hiyo kwa miaka 10 mfululizo.

Mafanikio:
Bernard Membe ameongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kipindi ambacho Tanzania na dunia, kwa ujumla, ilikabiliwa na changamoto kubwa katika mambo mbalimbali yanahusiana na ulinzi na usalama, uchumi na ajira (hasa kwa vijana). Changamoto hizo zimepelekea hali ya amani kwa ujumla kutetereka katika maeneo mengi ya dunia.

Hata hivyo, chini ya uongozi wa Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa, Tanzania imeendelea kuwa mtetezi na mshirika mkubwa wa ulinzi na usalama ndani ya Ukanda wa Afrika na duniani. Tanzania imeshiriki kuleta amani katika nchi za Maziwa makuu yaani, DRC, Burundi na Malawi, lakini pia Tanzania imeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za Comoro, Madagasca, na Sudan ya Kusini. Aidha, Tanzania imekuwa mshiriki mzuri katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika mataifa ambayo yalipata machafuko kisiasa.

Uchumi: Bernard Membe amesimamia vema utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya uchumi ili kuwezesha Tanzania kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kuininua hali za wananchi wake. Ni katika kipindi chake, nchi imeshuhudia uwekezaji mkubwa katika eneo la viwanda, gesi, makaa ya mawe, kilimo na utalii. Chini ya uongozi wa Ndugu Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilipata tuzo ya utendaji bora iliyotolewa na sekta binafsi kwa kutambua mchango mkubwa wa Wizara katika kukuza sekta binafsi Tanzania.

Kudumisha mahusiano kimataifa: Katika kipindi chake, Tanzania imefanikiwa kuipaisha Diplomasia yake katika Jumuiya ya Kimataifa kwa kutembelewa na viongozi mbalimbali mashuhuri kama, Marais George W. Bush na Baraka Obama wote wa Marekani, Xi Jinping wa Uchina, Joachim Gauck wa Ujerumani, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Piere Nkuruzinza wa Burundi, Joseph Kabila wa DRC, Philipe Nyusi wa Msumbiji, Mwana wa Mfalme wa Malkia wa Uiengereza, na Mwana wa Mfalme wa Japan.

Pia chini ya uongozi Ndugu Bernard Membe Tanzania imefanikiwa kupanua wigo wa mahusiano yake Kaimataifa kwa kufunguwa Balozi mpya katika nchi za Malaysia, Brazil, Comoro, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait. Aidha, Wizara imefanikiwa kufungua upya Ubalozi wa Tanzania the Hague, Uholanzi uliofungwa mwaka 1994. Kadhalika Balozi Mpya za Brazil, Oman, Uturuki, Kuwait, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Namibia zilifunguliwa hapa nchini.

Kutambuliwa:
Kwa kutambua mchango wake katika kurejesha hali ya amani na utulivu katika Visiwa vya Comoro, mwaka 2008, Bernard Membe alikuwa miongoni mwa watanzania waliotunukiwa Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro na rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Uozefu:
2006 – hadi sasa: Mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2008 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Africa, Addis Ababa, Ethiopia.
Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kutoka muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini, SADC
2006 – 2011: Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM
2006 – 2011: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.
2006 – hadi sasa: Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Taifa
2013 – hadi sasa: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Madola Commonwealth
2014 – hadi sasa: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amekuw mjumbe wa kamati za usuluhishi katika migogoro kwenye nchi za Sudan ya Kusini, Madagascan na katika mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi.
Pia Tanzania imefanikiwa kushiriki katika zoezi la Uangalizi wa chaguzi kwa niaba ya SADCC katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Madagasca, Kenya, Comoro na Afrika ya Kusini
Mimi na Magufuli tu, huyu hata simuwazii kabisa
 
1565270317707.png

Bernard Kamilius Membe alizaliwa tarehe 9 Novemba, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati wa watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe. Kwa kabila, Bernard Membe ni Mmwera, na kama ilivyo desturi ya Wamwera, watoto hutumia jina la ukoo wa Mama. Hivyo watoto wote saba wa familia hii ya Mzee Kamillius wamekuwa wanatumia jina la upande wa mama yao, Cecilia, yaani Membe.

Elimu:

1962 – 1968: Elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Chiponda, Lindi.
1969 – 1972: Elimu ya Sekondari, (O-level) Namupa Seminary, Lindi
1973 – 1974: Kidato cha tano na sita (A-level) Itaga Seminary, Tabora
1975 – 1980: Aliajiriwa serikalini, ofisi ya rais
1981 – 1984: Alipata Shahada ya kwanza katika tasnia ya Sayansi katika maswala ya Siasa na mahusiano ya kimataifa (Bachelor Political Science and International Relations with Hons, First class, University of Dar es salaam)
1985 – 1989: Aliendelea na ajira yake serikalini katika katika ofisi ya rais
1990 – 1992: Alipata Stashada ya Uchumi, Mahusiano ya Kimataifa na Sheria za Kimataifa (Masters- Economics, International Relations and International Law, John Hopkins University Marekani)
1993 – 1994: Alirudi serikalini kuendelea na kazi kama mchambuzi za mambo ya ulinzi na usalama

Mafunzo:

Kati ya mwaka 1975 na 1976 Ndugu Bernard Membe alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Oljoro, Arusha. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ambapo vijana wote waliohitimu kidato cha Sita walitakiwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya Jeshi, Ndugu Membe aliajiriwa katika Ofisi ya Rais, Utawala bora.

Mwaka 1978, Ndugu Membe alipata Mafunzo ya sheria za Jinai na usalama wa nchi, nchini Uingereza. Aidha, mwaka 1980, Ndugu Membe alipata mafunzo ya siasa, katika Chuo cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Kivukoni, Dar es Salaam.

Familia:

Mwaka 1986, Ndugu Bernard Membe alifunga ndoa Takatifu na Dorcas Richard Masanche, katika Parokia ya Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam. Ndugu Membe na mama Dorcas wamejaliwa kupata watoto watatu, Cecilia, Richard na Denis.

Siasa:

Ndugu Membe ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Kamanda wa Vijana wa Mkoa wa Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, na Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Mwaka 2000, aliingia Bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtama, kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya uchanga wake bungeni, akiwa kama mbunge wa kawaida (back bencher), Bernard Membe alikuwa mchangiaji mkubwa wa mijadala inayohusu Amani, Ulinzi na Usalama pamoja na Utawala Bora.

Mwaka 2005, Bernard Membe alichaguliwa tena na wananchi wa Jimbo la Mtama kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Tofauti na kipindi cha nyuma, Bernard Membe alianza muhula wa pili wa Ubunge, Januari 2006, kama ‘front bencher’ baada ya kuteuliwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Kufuatia mabadiliko ya baraza la Mawaziri mnamo mwezi Oktoba, 2006, Bernard Membe alihamishwa Wizara na kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati na Madini – moja ya wizara ngumu na nyeti kwa Taifa.

Hata hivyo miezi michache baadae, yaani January 2007, rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Bernard Membe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa baada ya aliyakuwa anashikilia wadhifa huo - Dr Asha Rose Migiro - kuteuliwa na Katibu Mkuu Baraza la Umoja wa Kimataifa na kuwa Naibu Katibu mkuu wa baraza hilo. Bernard Membe amehudu katika nafasi hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu 2007 hadi 2015, akiwa ni Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo kwa miaka mingi mfululizo, akitanguliwa na Rais Kikwete ambaye alidumu katika Wizara hiyo kwa miaka 10 mfululizo.

Mafanikio:

Bernard Membe ameongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kipindi ambacho Tanzania na dunia, kwa ujumla, ilikabiliwa na changamoto kubwa katika mambo mbalimbali yanahusiana na ulinzi na usalama, uchumi na ajira (hasa kwa vijana). Changamoto hizo zimepelekea hali ya amani kwa ujumla kutetereka katika maeneo mengi ya dunia.

Hata hivyo, chini ya uongozi wa Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa, Tanzania imeendelea kuwa mtetezi na mshirika mkubwa wa ulinzi na usalama ndani ya Ukanda wa Afrika na duniani. Tanzania imeshiriki kuleta amani katika nchi za Maziwa makuu yaani, DRC, Burundi na Malawi, lakini pia Tanzania imeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za Comoro, Madagasca, na Sudan ya Kusini. Aidha, Tanzania imekuwa mshiriki mzuri katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika mataifa ambayo yalipata machafuko kisiasa.

Uchumi: Bernard Membe amesimamia vema utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya uchumi ili kuwezesha Tanzania kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kuininua hali za wananchi wake. Ni katika kipindi chake, nchi imeshuhudia uwekezaji mkubwa katika eneo la viwanda, gesi, makaa ya mawe, kilimo na utalii. Chini ya uongozi wa Ndugu Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilipata tuzo ya utendaji bora iliyotolewa na sekta binafsi kwa kutambua mchango mkubwa wa Wizara katika kukuza sekta binafsi Tanzania.

Kudumisha mahusiano kimataifa: Katika kipindi chake, Tanzania imefanikiwa kuipaisha Diplomasia yake katika Jumuiya ya Kimataifa kwa kutembelewa na viongozi mbalimbali mashuhuri kama, Marais George W. Bush na Baraka Obama wote wa Marekani, Xi Jinping wa Uchina, Joachim Gauck wa Ujerumani, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Piere Nkuruzinza wa Burundi, Joseph Kabila wa DRC, Philipe Nyusi wa Msumbiji, Mwana wa Mfalme wa Malkia wa Uiengereza, na Mwana wa Mfalme wa Japan.

Pia chini ya uongozi Ndugu Bernard Membe Tanzania imefanikiwa kupanua wigo wa mahusiano yake Kaimataifa kwa kufunguwa Balozi mpya katika nchi za Malaysia, Brazil, Comoro, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait. Aidha, Wizara imefanikiwa kufungua upya Ubalozi wa Tanzania the Hague, Uholanzi uliofungwa mwaka 1994. Kadhalika Balozi Mpya za Brazil, Oman, Uturuki, Kuwait, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Namibia zilifunguliwa hapa nchini.

Kutambuliwa:

Kwa kutambua mchango wake katika kurejesha hali ya amani na utulivu katika Visiwa vya Comoro, mwaka 2008, Bernard Membe alikuwa miongoni mwa watanzania waliotunukiwa Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro na rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Uozefu:

2006 – hadi 2015: Mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2008 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Africa, Addis Ababa, Ethiopia.
Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kutoka muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini, SADC
2006 – 2011: Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM
2006 – 2011: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.
2006 – 2015: Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Taifa
2013 – 2015: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Madola Commonwealth
2014 – 2015: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amekuw mjumbe wa kamati za usuluhishi katika migogoro kwenye nchi za Sudan ya Kusini, Madagascan na katika mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi.

Pia Tanzania imefanikiwa kushiriki katika zoezi la Uangalizi wa chaguzi kwa niaba ya SADCC katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Madagasca, Kenya, Comoro na Afrika ya Kusini.
 
Manaake alioa akiwa na umri wa miaka 33

Yes, Watu wa Kitengo zamani walikuwa wakichelewa kuoa kutokana na majukumu pamoja na vetting kali ya wenza wao

Lakini hebu cheki CV ilivyoshiba, huyu mtu kapitia kwenye mifumo yote ya kuandaa viongozi, yaani kapikwa haswaa, Sijui CCM walimpata wapi huyu mkazi wa Magogoni wa sasa!. Wametuletea disaster katika nchi!
 
Back
Top Bottom