Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,956
Kipeperushi ni kizuri lakini kina makosa madogo madogo ya uchapaji yanayoweza kupunguza utamu. Dr. Slaa ni mtu makini sana na anapenda usahihi katika mambo yake. Naomba Mod ukiondoe kwa muda na kuhariri inapowezekana, mfano, neno "umakini" limeandikwa "umaskini".
Mkuu nadhani limeandikwa 'Uamakini'. Hii ni error ambayo nami nimekuja kuiona sasa hivi, lemme contact him (kama atajibu mail)
Na wewe unatishikaga kirahisi mno bana aaah...
Hata ilani ya CHADEMA nayo ilikutisha....Stivu vipi bana wewe?
=======Hii ni safi sana, unasambaza bure taarifa ya kujieleza wewe ni nani na utafanya nini. Ustaarabu wa hali ya juu. Sio kama kule Arusha tunakoambiwa eti kagazeti kamoja sijui kanaitwa CHANGAMOTO, kameandika kashfa kwa Slaa na kusambazwa bure kama kopi 3000 eti kummaliza Dr. Aibu tupu, Wakazi wa kule Arusha wamefurahi kupata karatasi za kufungia maandazi bure sio maudhui yaliyomo.
Tatizo lako nini si na wewe usambaze udaktari wa Kikwete kwanza mkwere anaongea lugha ngapi anakijua kispanyola au yeye ni ki kwere tu.Kumbe huyu jamaa hana degree ya kwanza (Bachelor) na ya pili (Masters? Na sheria anayoijua ni ya kanisa?! Nimeelewa mengi sana yaliyokuwa yanitatiza sasa
Mimi napenda lugha bana... mtu anayejua kilatini, kijerumani, kihispanyola na kifaransa huyo si mwenzako bana, tuache utani!! Mimi hapa naongea Kisukuma na kukiandika na ninajisifia ile mbaya sembuse hizo lugha kubwa 5?! Si unakumbuka mama Clinton alivyoanza kujifunza kuongea Kihispanyola ili ajaribu kuvuta kura za wamexicana!!! 🙂 Pia unakumbuka yule waziri wa zamani wa Uingereza, Blair alivyohutubia bunge la Ufaransa kwa Kifaransa jinsi ambavyo alipewa chati kwa hilo... Pia utakuwa unamkumbuka John Kerry alivyo bondwa kwa kujinadi anaongea Kifaransa ambapo Ufaransa time hiyo walikuwa perceived so negatively na Marekani kwa kutosupport uvamizi wa Iraq.
{hebu soma hapa:Language Log: The Linguistic Abilities of the Presidential Candidates}
Hata hapa JF... wewe mwenyewe hapo ulikuwa unampa tanotano za kisiri mpinzani wako Nyama Hatari kwa structure na grammar yake, hata huyu Kiranga na Pundit wetu unaona watu wanavyosalim amri kwa ujuzi wake... na kwa wengine hata wewe pia wanakuogopa. Sasa leo hii uniambie nisisalimu amri kwa Slaa kwa lugha zote hizo kama heshima ya aina yake?? Acha nitishike kwa namna yangu bana... lol
Chagua Mabadiliko,
Mchague Dk Slaa ili arudishe tunu za taifa letu:
Uzalendo, Maadili, Uadilifu na Umakini.
Wenye degree kama akina Chenge, Mramba, Lowassa wamefanyia nini Taifa letu kama siyo kuliingiza kwenye utata wa matatizo?!
Huu ni ujumbe ambao umetoka kwa Dr. Slaa, endapo utaupenda basi usambaze kadiri unavyoweza.
Kwanza kuwa na C.V ndefu au kubwa siyo kigezo cha kuwa kiongozi mzuri,pili je SLAA yupo kwenye chama makini? kinachoweza kuleta mabadiliko? Naamini na watu wengi wanafahamu kuwa SLAA yupo kwenye chama ambacho bado hakina uwezo wa kuiongoza Tanzania kwa sasa labda katika miaka ya huko mbeleni
Nadhani itakuwa jambo la busara kwanza kuondoa ufa uliopo kwenye chama baina ya Zitto na Uongozi ili Chadema ikichukua nchi mnakuwa mmesahau yaliyotokea awali au mnaonaje? ni mtizamo tu kila mmoja ana wake...
Kwenye uzoefu wake kiasiasa, kasahau kuandika alivyopigwa chini na CCM hadi kuamia chadema
Yes unaanza kutisha... walau kidogo kidogo. Kama ni mtisho wa mnyama, basi ni ule unaokifanya kipanya kikimbie... ukiongeza Kijerumani, utakuwa mtisho wa kuweza kufukuza paka... ukiweka Kispanyola na Kilatini basi hapo unaweza kumtimua hata mbwa!!! u get me??!! lolKama ndiyo hivyo basi ngoja na mimi nijisifu. Naongea Kisukuma kwa ufasaha kabisa. Naongea Kisukuma cha Ntuzu, cha Mwanza, na cha Shinyanga. Ingawa vyote ni Visukuma lakini vina tofauti kama ilivyo kwenye Kiingereza cha Marekani, cha Uingereza, Australia, n.k.
Naongea Kiswahili safi kabisa. Naongea Kiingereza cha Kimarekani vizuri kabisa. Kiingereza cha Uingereza nacho nakimudu barabara tena nakiongea kwa 'received pronounciation'.
Pia naongea Kifaransa na tasinifu yangu chuoni niliiandika kwa lugha hiyo na kutoa presentation ambayo ilihudhuriwa na mkuu wa chuo pamoja na watu wengine walioalikwa.
Oh nilitaka kusahau....
..................hablo español muy
Vipi sasa, na mimi natisha?
..................hablo español muy
Yes unaanza kutisha... walau kidogo kidogo. Kama ni mtisho wa mnyama, basi ni ule unaokifanya kipanya kikimbie... ukiongeza Kijerumani, utakuwa mtisho wa kuweza kufukuza paka... ukiweka Kispanyola na Kilatini basi hapo unaweza kumtimua hata mbwa!!! u get me??!! lol
Hamuwezi kukipa wewe na nani, kuna PONA au SAFINA labda havina ufa maana CCM, CUF, TLP vyote vina nyufa.Vyama venye ufa kama CHADEMA,hatuwezi kuvipa kura ya kuongoza nchi kwa sababu kama tukivipa kura na vikapata ushindi, kazi yoa ya kwanza itakuwa ni kutatua matatizo na migogoro yao badala ya kutatua matatizo ya wananchi (wapiga kura)
Lo siento, te ignore! No hablo su idioma. lolDuh naona nilikuacha solemba kidogo hapo....au hukuiona hiyo? Au uliiona lakini hukujua maana yake? Au bado hujui maana yake?
Habla espanol?
Huu ni ujumbe ambao umetoka kwa Dr. Slaa, endapo utaupenda basi usambaze kadiri unavyoweza.