Mimi napenda lugha bana... mtu anayejua kilatini, kijerumani, kihispanyola na kifaransa huyo si mwenzako bana, tuache utani!! Mimi hapa naongea Kisukuma na kukiandika na ninajisifia ile mbaya sembuse hizo lugha kubwa 5?! Si unakumbuka mama Clinton alivyoanza kujifunza kuongea Kihispanyola ili ajaribu kuvuta kura za wamexicana!!!
🙂 Pia unakumbuka yule waziri wa zamani wa Uingereza, Blair alivyohutubia bunge la Ufaransa kwa Kifaransa jinsi ambavyo alipewa chati kwa hilo... Pia utakuwa unamkumbuka John Kerry alivyo bondwa kwa kujinadi anaongea Kifaransa ambapo Ufaransa time hiyo walikuwa perceived so negatively na Marekani kwa kutosupport uvamizi wa Iraq.
{hebu soma hapa:
Language Log: The Linguistic Abilities of the Presidential Candidates}
Hata hapa JF... wewe mwenyewe hapo ulikuwa unampa tanotano za kisiri mpinzani wako Nyama Hatari kwa structure na grammar yake, hata huyu Kiranga na Pundit wetu unaona watu wanavyosalim amri kwa ujuzi wake... na kwa wengine hata wewe pia wanakuogopa. Sasa leo hii uniambie nisisalimu amri kwa Slaa kwa lugha zote hizo kama heshima ya aina yake?? Acha nitishike kwa namna yangu bana... lol