Wasifu wa Imani Kajula, CEO wa Simba SC

Ndio ana CV nzuri ya Mambo ya masoko, management na planning lakini Kuna story zake za zamani za chini chini zilisemwa Sana miaka Fulani .sidhani kama Simba wamefanya vetting ipasavyo...
 
Ebu wekapo yako mkuu
Nimemuelewa jamaa aliposema CV ni nyepesi kwa hoja moja, mleta uzi "ametishia" kwa kuaminisha kuwa bwana C.E.O amefanya kazi katika makampuni mbali mbali na mabenki ya ndani na nje, katika kuorodhesha hizo bank zote ni zetu hapa hapa.
 
Karibu msimbazi kabla hajaja msimbazi alikuwa CEO WA BARCELONA akawa naibu CEO pale REAL MADRID wapinzan kazi wanayo soon tutamuona KIBU BARCELONA kama unabisha uliza samata kama hajacheza Uefa chini ya mikono ya huyu mwamba KAJUNA
 
Sawa mkuu, pamoja na CV hiyo huyu Bwaa mkubwa atachacheza namba ngapi pale Simba ili ichukue makombe naomba kufahamu.
CEO wa Yanga huwa anacheza number ngapi uwanjani?
 
Ngoja kwanza

Simba hawakuona haja ya kuwa na mtu ambaye ni mbobezi kwenye masuala ya mpira zaidi?
Kwa hiyo wangemuajiri Zamoyoni Mogela? Jamani kama hamjui majukumu ya CEO mnyamaze kimya
 
Miezi sita michache sana, hata ofisi atakua hajaijua.
 
Jamaa ni mzuri sana. Pia, Amekuwa akiratibu marathon kadhaa hapa nchini na zimekuwa zikifanya poa sana.
 
Yani simba imekua kama duka la reja reja, huyu nae kapewa mkataba wa miezi sita?
JF ina wajinga wajuaji. Ona huyu, anadhani Kajula ni mchezaji kwa hiyo apewe miaka. Huo ni muda wa matazamio uki perform unaongezewa. Simba ina strategic plan, kinachotafutwa ni mtu wa kuitekeleza.
 
Binafsi huwa sioni kazi ya hawa jamaa. Simba wana tatzo la kuwa na wachezaji wa kawaida, badala la kusajili wachezaji makini wao wana deal na vitu vya hovyo hovyo tu
 
CEO ni decision maker. Kwahiyo CEO mzuri ni yule Anaye Fanya Maamuzi. Hata Barba Mlisema Sanaaa Lakini Ndio Aliye Fanya Hadi Leo GSM sio Mdhamini Mwenza Wa Ligi Kuu Tanzania Bara…. Ndio CEO aliye Fanya Simba Kwenda Kushiriki Super League Ya CAF, Ndio CEO aliye Fanya Al Hilal , TP Mazembe, Mamelod, na Timu zingine Zikija Tanzania Zijione zipo Nyumbani.

Ndio CEO aliye Wakataa Sport Pesa na Leo Yupo na M-Bet kwa Dau kubwa… Japo Barba Alisemwa Hawezi na Kawekwa na Mo

Hata Huyu Ndio mtasema sana lakini ndio Atakuja Kufanya Makubwa. kuwa CEO wa Simba / Yanga Unahitaji Roho ngumu tuuu ya kupambana na Uchawi na Mamuluki kwenye Taasisi Basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…